Saturday, April 5, 2014

MATUKIO YA KAMPENI ZA UBUNGE CHALINZE KUPITIA CHADEMA

Mzee wa kimila wa jamii ya Wamasai, Ole Kanjoro akimwombea Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Issa Said Mohamed ili kuendeleza na kukitakia ushindi chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Chalinze, katika hafla iliyofanyika mjini Chalinze jana. 

Mgombea wa ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Torongey akiombea kimila na mzee wa mila ya jamii ya Wamasai, Meriani Moreto kwa lengo la kumtakia ushiondi katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo, katika hafla iliyofanyika mjini Chalinze jana.

Mgombea wa ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Thorongey akivishwa mgolole na ijana wa kiongozi wa kimila wa Wamasai (Laigwenani), Almasi Jani, wakati wa tambiko maalum la kimila kumatakia ushindi mgombea huyo, lililofanyika mjini Chalinze jana.

No comments:

Post a Comment