Sunday, April 6, 2014

MATUKIO KATIKA UCHAGUZI WA CHALINZE

Gari aina ya Toyoya Land cruiser lenye namba za usajili T 630 BFJ ambalo lilidhaniwa kuwa ni la CCM likiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukutwa na silaha mbalimbali zikiwemo mapanga, mishale, binduki na mikuki lililokuwa likifuatilia nyendo za mgombea wa ubunge katika Jimbo la Chalinze, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Torongey jana.

Moja ya vituo vya kupigia kura (Ofisis ya Maji Changa 1.) katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze, kikiwa katika nyumba ya kada wa CCM, Issa Mbogo, iliyopo Kijiji cha Changa, kilivyokutwwa jana. Hayo ni moja ya malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wagombea.

Mgombea wa ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mathayo Torongey akizungumza na mawakala wakati alipokuwa akitembelea vituo katika zoezi la upigaji kura jana.

Mmoja wa wapiga kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze, Sabina akitumbukiza karatasi ya kura kumchagua mbunge wa jimbo hilo, katika uchaguzi uliofanyika jana

No comments:

Post a Comment