Sunday, February 9, 2014

Yaliyojiri katika Uchaguzi wa Udiwani kata 27 na Matokeo - Feb 9, 2014

Kama ilivyo kawaida yetu kuwahabarisha kupitia hapa, tutaendelea kuwaletea kila kinachojiri, kuanzia kufunguliwa vituo vya kura, upigaji kura, flow ya wapiga kura, matukio yoyote yatakayokuwa yanajitokeza wakati wa upigaji kura, matukio yoyote yatakayojitokeza wakati wa kuhesabu kura, kutangazwa matokeo, pamoja na matukio yatakayotokea wakati wa kutangaza matokeo.

Tutaleta updates kadri zinavyopatikana kutoka maeneo mbalimbali, ili kuhabarisha umma juu ya shughuli hii muhimu ya kidemokrasia.

Tutashirikiana na makamanda wengine walioko katika kila kata ya uchaguzi au wanaopata taarifa za uhakika kutoka maeneo hayo.

Updates:
Mwananchi Breaking News....

MBUNGE CCM ASHAMBULIWA: L. Mwanjali Mbeya Vijijini apigwa na kujeruhiwa asubuhi hii kwenye uchaguzi kata ya Santilya, polisi yakamata 7 wa Chadema kuhusika.

More Updates;

- Huko Bagamoyo ambako kuna uchaguzi katika Kata ya Magomeni, gari moja inayosadikiwa kuwa ya CCM imekamatwa na vijana wa Ulinzi wa CHADEMA, Red Brigade, ikiwa silaha za jadi yakiwemo mapanga.

- Habari zilizopatikana kutoka Shinyanga zinasema kuwa kuna watu 18 kutoka mjini hapo ambao wamekodiwa na mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM mkoani humo ambaye ni mmoja watu muhimu wa team Lowassa kwenye masuala ya mbio za urais, vijana hao wamepandishwa kwenye moja ya magari ya kampuni maarufu ya mabasi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga. 

- Idadi yao ni 18. Gari walilopandishwa linatoka Kahama kwenda Ulowa. Walitakiwa washuke Ulowa No. 5 ili wapokelewe na watu wa CCM, kisha wapelekwe kwenye kata ya uchaguzi ambayo ni Ubagwe kwa ajili ya kufanya 'kazi' waliyoelekezwa.

- Taarifa kutoka Kata ya Ukumbi, Kilolo zinasema mgombea wa CHADEMA pamoja na makamanda wengine pamoja na gari lao wamekamatwa na kushikiliwa polisi, hivyo CCM wako huru wakiendelea kufanya hujuma kadri wanavyotaka.

- Polisi wametumia mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa CCM, Chadema kwenye vurugu zilizotokea punde kwenye uchaguzi kata ya Sombetini

-----------
Updates kutoka Iringa;

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na vijana wengine 4 wa CHADEMA, wanashikiliwa central police Iringa. Mbunge huyo alikamatwa wakati akitoa maelekezo kwa makamanda.

Updates kutoka Mrijo, Kondoa

Kura zimeanza kuhesabiwa vituoni. Muda si mrefu tutapata matokeo ya kata hiyo...

Updates kutoka Kata ya Ibumu, Kilolo;

Mbunge wa Viti Maalum, Kamanda Chiku Abwao anasema upigaji kura umeshakoma katika vituo vyote na shughuli ya kuhesabu kura imeanza kitambo. Matokeo yanaweza kutoka wakati wowote kuanzia sasa. Kamanda Abwao anasema hali ni nzuri na uwezekano wa mgombea wa CHADEMA, mpiganaji Jully Petro Mpugula kuibuka mshindi ni mkubwa.

Updates kutoka Ukumbi, Kilolo

Vituo vyote vya kupigia kura vimeshafungwa. Shughuli ya kuhesbau kura inaendelea. Kamanda Nyalusi anasema hali iko shwari hadi muda huu. Polisi wamemuachia mgombea wa CHADEMA, mpiganaji Oscar Ndale, lakini wameendelea kuwashikilia makamanda kadhaa, akiwemo Kamanda Mwambigija (Mzee wa Upako) pamoja na gari la M4C.

Matumaini ya ushindi hapa ni makubwa. Baada ya gari kukamatwa. Vijana wa bodaboda wamejitolea kwenda kuziba nafasi hiyo na kujitoa kufanya kazi kuhakikisha mapambano ya kumpata kiongozi wao hayakwami.

MATOKEO:

- CHADEMA Tumeshashinda Kata ya Sombetini kwa 2548 na CCM 2077, Kiboriloni ya Mjini Moshi na Njombe Mjini Mkoani Njombe. Matokeo yote utayapata hapa. Usiwe mbali tafadhali.

Kata ya Kasanga Mkoani Rukwa CHADEMA tunaongoza kwa mbali sana.

Kata ya Kiomoni Mkoani Tanga CHADEMA tumeshindwa.

===========
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimefanikiwa kutetea kata zake zote tatu ambazo leo wananchi wameshiriki kupiga kura kuwachagua madiwani kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki dunia


Kurugenzi ya Habari

1 comment:

  1. hahahaha AIBU... CHADEMA NDIO MWISHO WENU MWAKA HUU

    ReplyDelete