Saturday, February 22, 2014

Werema!; Msiende Bunge la Katiba na Vyeo Vyenu!

KUTOKANA na Malumbano, vijembe na mvutano ulioanza karibuni katika Bunge la Katiba na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kutoa elimu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, huku Tundu Lissu, akidai Werema ainapotosha, ni Vema vigogo wasiende na Vyeo vyeo kwenye Bunge hilo.
Ni vema wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakajua kwamba, baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kufanya kazi iliyopo mbele yao, viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Mwanasheria Mkuu, Werema na Mawaziri, wanapaswa kuvua nyadhifa zao na kuwa Wajumbe.
Tabia ya kujisahau na wao kuona Wanatetea Serikali, Wizara, Taasisi na Vyeo, na Nyadhifa walizonavyo, inapaswa kuvuliwa kama Gamba la Nyoka, ili wafanane na Wajumbe walioteuliwa na Rais, Wakulima, Wafungaji, Viongozi wa Dini, Wafanya Biashara, Walemavu na wengineo.
Ikifika mahali wakidhani wanajadili hoja ya Katiba na watu wanaowaongoza, kutokana na Vyeo, Nyadhifa, Mashangingi, Ofisi na Madaraka waliyokalia, hawawezi kupokea mawazo ya walalahoi, waliotunukiwa nafasi hiyo kuwawakilisha wenzao.
Iwapo Vigogo hao watajitandika na kujifunika Mtandio mweusi, na kuziba masikio kwa kutotaka kupumzisha madaraka yao ofisini mwao kwa siku 70 au 90 za kujadili Rasimu hiyo zipite, tutaishia mahakamani au kukosa Katiba iliyotarajiwa na wananchi kwa kipindi kirefu.
Lakini pia, tunawataka wajumbe wengine waliochaguliwa kutoka taasisi mbalimbali wasijikane na kujiona Wadogo au si kitu kutokana na kuwa pamoja na Viongozi wenye Nyadhifa na Vyeo vyao serikalinini na Vyama, kiasi cha kuwaogopa na kutochangia hoja za kuwatetea wananchi.
Hatutaki wajumbe wateuliwa, waoneshe unyonge dhidi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri na lile la Wawakilishi, kwa sababu wananchi wawategemea sana ninyi msio na chembe ya ubinafsi na Mashinikizo ya Vyeo, Nyadhifa, Mashangingi na Ofizi kubwa hadi zikawanyong’onyeza na kuwatisha.
Nawataka wajumbe muelewe mmetumwa na wananchi kuwatendea kazi ya kuichambua, kuboresha na kupitisha Katiba ambayo wananchi wametoa mawazo yao, tofauti na Katiba zilizopita ambazo zilifanywa na mawazo ya watu kwa faida za watawala na si watawaliwa kama hii.
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema”. Inasema Biblia 1Petrol 2;9-10.
Hivyo, wajumbe ninyi ni wateule wa wananchi walalahoi, ninyi ni ukuhani wa kifalme wa waajiri (wananchi), ambalo ni taifa takatifu, linalomiliki Tanzania pamoja na Mungu, mpate kufanya kitu chema ili taifa lisiwe gizani ila liingie katika nuru na haki ya ajabu kwa miaka na karne zijazo kwa vizazi vyetu.
Kama hamkuchaguliwa na mtu, Serikali, Cheo, basi nawasihi kama wapitaji wa nafasi hiyo, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho ya uharibifu wa Katiba yetu iliyotarajiwa baada ya kuitolea maoni ya kwanza na kundi la pli na sasa ninyi., ili tuingie kwenye kura kwa Amani.
Ni rai yetu Mwe na mwenendo mzuri ili, wakitaka kuwasingizia kuwa watenda mabaya, kwa viposho, agenda za siri za upotoshwaji na ushawishi (Spring Doctors), wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya Mafanikio ya Katiba hiyo nzuri. ikijiliwa. 
Msitii kila kiamriwacho na watu wenye Cheo, Nyadhifa, Mashangingi na Ofisi zao ili kuwapotosha, ila kwa ajili ya kile ambacho Mungu amekubali wananchi watendewe; hata ikiwa ni mfalme, mwenye cheo kikubwa; hapo mtawatendea haki wananchi na posho hiyo nzuri.
Wakubwa, wakifanya walichotumwa na wananchi fanyeni, lakini kama ni kulipiza kisasi ili watenda mabaya na kuwasifu watenda mabaya; Kataeni, ila wakitenda mema. kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu.
Biblia katika 1Petro 2:16 inasema, “Kwa kutenda mema mtaziba vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu”
Hivyo wajumbe nataka wathaminini uteuzi wao ili kujlinda Historia yao nzuri mbele za Mungu na Kizazi Kijacho.

0715933308

No comments:

Post a Comment