Saturday, February 22, 2014

LIVE UPDATES: Uzinduzi wa kampeni za CHADEMA jimbo la Kalenga


Kama mnavyojua kuwa leo CHADEMA kinazindua kampeni zake kwenye Jimbo la Kalenga, uzinduzi utao ongozwa na katibu mkuu wa chama na nguli wa siasa za Tanzania Bwana Dr Wilbroad Slaa utakata utepe kusafisha njia ya kwenda kuchaguliwa Bi Grace Mvanda anayeeperusha bendera ya CHADEMA kwenye uchaguzi unao tarajiwa kufanyika tarehe 16 Machi 2014.
Updates kutoka eneo la tukio zitakujua hapa hapa.


- msasafara wa CHADEMA ulianza kwa kwenda kuzuru kaburi la Chief Mkwawa kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara ambapo viongozi na wanachama ambao walikuwa hawajawahi kufika hapo walipata baraka za wana ukoo wa chiefu huyo aliyeandika historia mujarabu ya eneo hilo.

- Msafara huo ulipata fursa ya kuongea na familia na wana ukoo wa Chief Mkwawa na kupata baraka za ukoo wa chief huyo kwa kupata maelezo kutoka kwa mwana ukoo Bwana Augustino Mkini. Baada ya kuzuru kaburi msafara wa CHADEMA na mbunge mtarajiwa Bi Grace Tendega uliondoka kuelekea kwenda kwenye mkutano wa hadhara huku mvua kubwa ikiwa inanyesha.

- Mvua ni kubwa sana lakini watu wanavumilia mvua hiyo bila kujali huku wakionyesha mapenzi yao kwa chama chao na mbunge wao mtarijiwa anaye kwenda kuziondoa kero za wanakalenga zilizodumu kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru.

- Sasa msafara ndio umefika eneo la mkutano katika uwanja wa mpira wa Kalenga, mvua ni kubwa lakini watu wanaendelea kuvumilia na kuiona kama baraka kuelekea kuapishwa mbunge wao mtarajiwa Bi Grace Mvanda tumaini la wana Kalenga baada ya aliyekuwa waziri mzigo kufariki na sasa mzigo mtoto unataka kurithi mikoba.

- Mkutano unaanza kufunguliwa kwa maombi, amenza kupanda sheikh wa wilaya ya Kalenga na kuomba dua ya kufungua mkutano na kufuatiwa na kiongozi wa madhebu ya kikristo. Kama kawaida CHADEMA huanza, wako na Mungu na watamaliza na Mungu. Wao huanza na mabomu na kumaliza kwa kuwategemea tume na Polisi ili washinde uchaguzi.

- Viongozi wa dini wamemaliza kufungua mkutano kwa dua na maombi yatakayo simamia kampeni ziende vizuri kwa amani na usalama huku ikitegemewa kuwa maombi hayo yataenda kuwaongoza wanakelenga kufanya maamuzi sahihi kwa kumchagua mwana mama Mvanda tendega GRACE mbunge mtarajiwa wa jimbo la Kalenga.

2 comments:

  1. naomba wananchi wa kalenga waenzi ujasiri wa mkwawa, kwa kumkataa mgombea kibaraka asiyejua hata asili yake, kwani hakuna asiyejua kwamba ndugu mgimwa amebebwa na CCM kama kifuta machozi tokana na baba yake kufariki huku akishutumiwa kuwa ni mzigo kwa serikali,

    ReplyDelete
  2. ukiwapima wagombea wa CCM na CHADEMA mgombea wa chadema anauzika zaidi kuliko wa CCM, MUHIMU chadema kuwa makini na rafu zozote ambazo zinaweza kuchezwa na CCM, na kiukweli kunahitajika wabunge wengine wa CHADEMA ili kuwatetea wananchi wa iringa kwani msigwa na abwao wamebeba mzigo mzito,

    ReplyDelete