Saturday, February 8, 2014

Wajumbe Bunge la Katiba hawa hapa

SERIKALI imetangaza majina 201 ya wajumbe kutoka makundi mbalimbali nchini walioomba kuteuliwa ili kuingia kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Kabla ya kutangaza majina hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Florence Turuka, alisema kazi ya kuwapata wajumbe wa Bunge hilo ilikuwa ngumu kwani walioomba walikuwa 3,754 na waliotoswa 3,553.
Alisema wapo waombaji 118 waliojiteua wenyewe  na kwamba kulikuwa na vimemo vya waliokuwa wakiomba uteuzi kinyume cha sheria.
Alisema uteuzi huo umezingatia ushiriki wa rika na jinsi zote na kwa kuzingatia uwiano wa theluthi moja ya wajumbe kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanganyika kwenye kila kundi.
Kwa mujibu wa Dk. Turuka, wajumbe vijana wenye umri kati ya miaka 22 hadi 35 wapo 35; wenye umri wa kati ya miaka 36 hadi 64 wapo 145 na wenye umri wa miaka 65 na kuendelea wapo 21.
“Hapa kwenye umri yupo mjumbe mwenye miaka 81, tulizingatia hilo kwa sababu uzee dawa… kati ya wote hao wapo wanawake 100 na wanaume 101 ili kuweka uwiano wa jinsia, japo kidogo kwa wanaume imezidi kwa sababu hakuna mtu nusu,” alisema.
Miongoni mwa waliotoswa ni wakili maarufu nchini, Mabere Marando, pamoja na watu maarufu, wenye uzoefu na sifa ya kuingia katika Bunge hilo, lakini ameteua majina 201 kwa mujibu wa katiba kuingia kwenye Bunge hilo.
Walioteuliwa
Wajumbe kutoka taasisi zisizokuwa za kiserikali
Tanzania bara ni Magdalena Rwebangira, Kingunge Ngombale Mwiru, Asha D. Mtwangi, Maria Sarungi Tsehai, Paul Kimiti, Valerie N. Msoka, Fortunate Moses Kabeja, Sixtus Raphael Mapunda, Elizabeth Maro Minde, Happiness Samson Sengi, Evod Herman Mmanda, Godfrey Simbeye na Mary Paul Daffa.
Kutoka Zanzibar ni Idrissa Kitwana Mustafa, Siti Abbas Ali, Abdalla Abass Omar, Salama Aboud Talib, Juma Bakari Alawi, Salma Hamoud Said na Adila Hilali Vuai.
Kutoka taasisi za kidini Tanzania Bara
Tamrina Manzi, Olive Damian Luwena, Shamim Khan, Mchungaji Ernest Kadiva, Sheikh Hamid Masoud Jongo, Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela, Magdalena Songora, Hamisi Ally Togwa, Askofu Amos J. Muhagachi, Easter Msambazi, Mussa Yusuf Kundecha, Respa Adam Miguma na Profesa Costa Ricky Mahalu.
Zanzibar ni Sheikh Thabit Nouman Jongo, Suzana Peter Kunambi, Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu, Fatma Mohammed Hassan, Louis Majaliwa, Yasmin Yusufali E. H Alloo na Thuwein Issa Thuwein.
Kundi la vyama vya siasa
Tanzania Bara;  Hashim Rungwe Spunda, Thomas Magnus Mgoli, Rashid Hashim Mtuta, Shamsa Mwangunga, Yusuf  S. Manyanga, Mchungaji Christopher Mtikila, Bertha Ng’angompata, Suzan Marwa, Dominick Abraham Lyamchai, Mbwana Salum Kibanda, Peter Kuga Mziray, Isaac Manjoba Cheyo, Dk. Emmanuel John Makaidi, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Modesta Kizito Ponera, Profesa Abdallah Safari na Salumu Seleman Ally.
Wengine ni James Kabalo Mapalala, Mary Oswald Mpangala, Mwaka Lameck Mgimwa, Nancy  S. Mrikaria, Nakazael Lukio Tenga, Fahmi Nasoro Dovutwa, Costantine  Benjamini Akitanda, Mary Moses Daudi, Magdalena Likwina, John Dustan Lifa Chipaka na Rashid Mohamed Ligania Rai.
Kutoka Zanzibar;  Ally Omar Juma, Vuai Ali Vuai, Mwanaidi Othman Twahir, Jamila Abeid Saleh, Mwanamrisho Juma Ahmed, Juma Hamis Faki, Tatu Mabrouk Haji, Fat –Hiya Zahran Salum, Hussein Juma, Zeudi Mvano Abdullahi, Juma Ally Khatibu, Haji Ambar Khamis, Khadija Abdallah Ahmed na Rashid Yussuf Mchenga.
Kundi la taasisi za elimu
Kutoka Tanzania Bara ni Dk. Suzan Kolimba, Profesa. Esther Daniel Mwaikambo, Dk. Natujwa Mvungi, Profesa. Romuald Haule, Dk. Domitila A.R. Bashemera, Dk. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa, Profesa Bernadeta Kilian, Teddy Ladislaus Patrick, Dk. Francis Michael, Profesa Remmy J. Assey, Dk. Tulia Ackson, Dk. Ave Maria Emilius Semakafu na Hamza Mustafa Njozi.
Zanzibar;  Makame Omar Makame, Fatma Hamid Saleh, Dk. Aley Soud Nassor, Layla Ali Salum, Dk. Mwinyi Talib Haji, Zeyana Mohamed Haji na Ali Ahmed Uki.
Kundi la watu wenye ulemavu
Tanzania Bara;  Zuhura Musa Lusonge, Frederick Msigala, Amon Anastaz Mpanju, Bure Zahran, Edith Aron Dosha, Vincent Venance Mzena, Shida Salum Mohamed, Dk. Henry Mwizengwa Nyamubi, Elias Msiba Masamaki, Faustina Jonathan Urassa, Doroth Stephano Malelela, John Josephat Ndumbaro na Ernest Njama Kimaya.
Kutoka Zanzibar ni Haidar Hashim Madeweyya, Alli Omar Makame, Adil Mohammed Ali, Mwandawa Khamis Mohammed, Salim Abdalla Salim, Salma Haji Saadat na Mwantatu Mbarak Khamis.
Kundi la vyama vya wafanyakazi
Tanzania Bara: Honorata Chitanda, Dk. Angelika Semike, Ezekiah Tom Oluoch, Adelgunda Michael Mgaya, Dotto M. Biteko, Mary Gaspar Makondo, Halfani Shabani Muhogo, Yusufu Omari Singo, Joyce Mwasha, Amina Mweta, Mbaraka Hussein Igangula, Aina Shadrack Massawe na Lucas Charles Malunde.
Zanzibar ni Khamis Mwinyi Mohamed, Jina Hassan Silima, Makame Launi Makame, Asmahany Juma Ali, Mwatoum Khamis Othman na Rihi Haji Ali.
Kundi la vyama vinavyowakilisha wafugaji
Tanzania Bara; William Tate Olenasha, Makeresia Pawa, Mabagda Gesura Mwataghu, Doreen Maro, Magret Nyaga, Hamis Mnondwa na Ester Milimba Juma.
Zanzibar; Said Abdalla Bakari, Mashavu Yahya na Zubeir Sufiani Mkanga.
Kundi linalowakilisha vyama vya wavuvi
Tanzania Bara; Hawa A. Mchafu, Rebecca Masato, Thomas Juma Minyaro, Timtoza Bagambise, Tedy Malulu, Rebecca Bugingo na Omary S. Husseni.
Kutoka Zanzibar; Waziri Rajab, Issa Ameir Suleiman na Mohamed Abdallah Ahmed.
Kundi linalowakilisha vyama vya wakulima
Tanzania Bara ni Agatha Harun Senyagwa, Veronica Sophu, Shaban Suleman Muyombo, Catherine Gabriel Sisuti, Hamisi Hassani Dambaya, Suzy Samson Laizer, Dk. Maselle Zingura Maziku, Abdallah Mashausi, Hadijah Milawo Kondo, Rehema Madusa, Reuben R. Matango, Happy Suma na Zainab Bakari Dihenga.
Kutoka Zanzibar ni Saleh Mohamed Saleh, Biubwa Yahya Othman, Khamis Mohammed Salum, Khadija Nassor Abdi, Fatma Haji Khamis, Asha Makungu Othman na Asya Filfil Thani.
Kundi la watu wenye malengo yanayofanana
Tanzania Bara ni Dk. Christina Mnzava, Paulo Christian Makonda, Jesca Msambatavangu, Julius Mtatiro, Katherin Saruni, Abdallah Majura Bulembo, Hemedi Abdallah Panzi, Dk. Zainab Amir Gama, Hassan Mohamed Wakasuvi, Paulynus Raymond Mtendah, Almasi Athuman Maige, Pamela Simon Massay, Kajubi Diocres Mukajangwa na Kadari Singo.
Zanzibar ni Yussuf Omar Chunda, Fatma Mussa Juma, Profesa Abdul Sheriff, Amina Abdulkadir Ali, Shaka Hamdu Shaka na Rehema Said Shamte.

No comments:

Post a Comment