Saturday, February 8, 2014

Diwani Chadema kuongoza Maandamano!

Na Bryceson Mathias, Nyandira Mvomero. 

WAFANYA Biashara wa soko la Nyandira, wanaandaa maandamano wakidai yatakoyoongozwa na Diwani wa Kata, Ruanda Zengwe (CHADEMA), yenye nia ya kumtoa ofisini Mhandisi wa Wilaya, William Lameck, akatengeneza barabara, inayowagharimu Mil.9.6/- kwa mwaka.

Kero ya barabara hiyo, pia inaungwa mkono na wananchi wa Kata ya Nyandira, ambao kimsingi wamedai watakuwa tayari kumuunga mkono Diwani na wafanya biashara hao, ili kushinikiza Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na Viongozi, kutengeneza barabara hiyo yenye adha kwao.

Alipohojiwa na Gazeti hili jana kuthibitisha kama malalamiko ya wafanya biashara hao ni ya kweli. na kama yupo tayari kuwaunga mkono kuongoza maandamano hayo, Diwani Zengwe alisema kwamba, 

“Madai ya Wafanya biashara hao ni ya kweli, kila mwezi wanakatwa Ushuru, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ikiwa inachukua Sh. Laki 8/- kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni Mil.9.6/-; hivyo inasikitisha kwa nini barabara hiyo haitengenezwi, kiasi cha kuhatarisha maisha yao.

“Mara maandalizi hayo yatakapoiva, kama Diwani ninayejua uhalisia wa madai ya wafanya biashara hao, jinsi wanavyoporwa fedha zao, halafu hawatengenezewi miundo mbinu yao. ‘Nitakuwa tayari na nitaongoza maandamano hayo’,kama yatakavyokusudiwa”.alisema Zengwe.

Pia Zengwe alisema, anafahamu lipo fungu lililotengwa kwa ajili ya ukarabati wa miundo mbinu ya barabara hiyo, lakini sielewi fedha hizo zimeingia kwenye Tumbo na Mfuko wa nani! Kiasi cha kuacha wajawazito na wagonjwa wakiwemo watoto wadogo, maisha yao yawe hatarini.

Aidha kwa upande wake Mhandisi wa Wilaya ya Mvomero Lamecck alipoulizwa alikiri kwamba, “Ipo asilimia 10% ya fedha za ukarabati wa barabara hiyo, hivyo ni vizuri umuulize Diwani wa Nyandira, Zengwe, anafahamu suala hili”, jambo ambalo limepingwa ikihofiwa fedha hizo zinatafunwa.

No comments:

Post a Comment