RAIS Jakaya Kikwete ametakiwa kuwashauri wabunge kuboresha rasimu ya pili ya Katiba inayokwenda kujadiliwa hivi karibuni katika Bunge la Katiba, mjini Dodoma badala ya kuijadili kwa masilahi ya vyama vyao.
Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, alipozungumza na waandishi wa habari katika kongamano la Katiba ambalo lilijumuisha watu kutoka asasi mbalimbali.
“Kuna kazi kubwa ya kuipitia rasimu hiyo na kuirekebisha na tuache mambo ya serikali mbili au tatu, kwani hiyo ni kupotosha maana nzima ya Katiba wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba imefanya kazi katika mazingira magumu,” alisema.
Aidha, alisema anatumaini Watanzania watafika mahali watazungumzia mambo muhimu ya nchi kuliko kuzungumzia mambo ya kutaka vyeo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Tanzania (TAPID), John Malya, alisema Katiba itakayojadiliwa iwe ni ya manufaa kwa Watanzania na yenye kuleta muafaka kwa taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment