Tuesday, February 4, 2014

Makombora ya Mbowe yamtetetemesha DC-Mvomero.

MAKOMBORA ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, yamemtetemesha Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka, na kumfanya ageukie matapishi ya kauli yake, ambapo amekifungua Kiwanda cha Sukari Mtibwa alichokifunga kianze uzalishaji.
Siku moja kabla ya Mafuriko ya CHADEMA ya M4C-Pamoja Daima yaliyofanyika Kata ya Mtibwa, Makombora aliyotoa Mbowe Siku ya Mkutano kuhusu Mtaka kufunga Kiwanda hicho wakati wananchi wanakidai haki zao, yamemtetemesha na kulazimika kukifungua kianze kazi.
Jumamosi, Februari 01, 2014, gari la Matangazo lilipita katika Mjii mdogo wa madizini likiwataka wafanyakazi na wakulima wadogo wa Miwa wafike ofisi ya Kata ya Mtibwa saa Nne asubuhi ili wapewe na DC Mtaka majibu ya ahadi ya Mwekezaji dhidi ya madai yao zaidi ya Bil. 1.9/-.
Akiamuru kiwanda kufunguliwa na wafanyakazi kwenda kazini Jumatatu, Februari 3, Mtaka alisema, “Ijapo fedha iliyoingizwa kwenye moja ya vyama vya Wakulima inaonesha kuwa chache (Mil. 60/-), nashauri waanze kulipwa wakulima wadogo wenye mil. 1/- na kushuka”.
Kauli hiyo ilisababisha makelele ya wananchi kumdai amruhusu Diwani wa Kata hiyo, Luka Mwakambaya (CHADEMA), (ambaye hakuarifiwa wito wa hadhara hiyo) aongee, ingawa alifika kwa kusikia matangazo, lakini Mtaka hakumpa fursana ndipo wananchi wakanza kumzomea.
Diwani Mwakambaya alipohojiwa alimlaumu Mtaka akisema, “Mimi ni kama Rais wa Kata, sikupaswa kunyimwa kuongea na wananchi wangu, na kwa kwa kunyima fursa ya kuongea, ndiyo imemfanya DC azomewe na wananchi, jambo ambalo lisingemkuta.
“Nimeona wakiondoka kwenye Kikao na kwenda kupongezana na Mwekezaji, Madiwani wa Chama cha Mapinduzi na Viongozi wao, maana ya kwamba, lile Changa la Macho walilokusudia kuwapiga wakulima na wafanyakazi walipoona OPD ya Chadema, limefanikiwa”.alisema Mwakambaya.
Aidha baada ya kikao hicho, Wakulima wadogo wa Miwa na wafanyakazi ambao waliomba majina yao yasitajwe walisema, “Walijuwa wanapigwa Changa la Macho na CCM kutokana na kuihofu Chadema iliyokuwa na M4C-OPD, lakini hasira zetu tutazimalizia serikali za Mitaa na 2015.
Awali Mtaka alikifunga Kiwanda cha Sukari Mtibwa kwa madai, kimeshindwa kuwalipa wafanyakazi na wakulima malipo yao ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero inayomdai Mwekezaji wa Mtibwa zaidi ya Mil.4.4/-, ambapo Mbowe alisema suluhu si kufunga kiwanda ila ni kuwalipa wadai.

No comments:

Post a Comment