MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anatimiza ahadi anazozitoa mbele ya wananchi, ikiwemo kuonana na mbunge huyo ili kushughulikia matatizo ya maji yanayolikumba jimbo la Ubungo, ahadi ya barabara ya Kimara Bonyokwa, ujenzi wa kituo cha wanafunzi na nyinginezo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kuhusiana na mgogoro wa ardhi Kwembe Kati, Kisokwa na Mloganzila jijini Dar es Salaam, Mnyika alisema kuwa ni vyema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akajibu juu ya hatua za kumaliza mzozo wa Mloganzila na Kinondoni kuhusu mpaka.
Alisema kuwa ameshangaa baadhi ya ripoti zilizotoka katika vyombo mbalimbali vya habari kueleza kuwa hashughuliki na mgogoro wa ardhi katika maeneo hayo wakati alishafuatilia suala hilo na kukutana na kamati ya kijiji ya mgogoro huo.
Alisema kuwa kama serikali inashindwa kutimiza ahadi ya kulipa sh mil. 9 kama fidia ya ardhi, bora iwatafutie viwanja mbadala wananchi hao.
Mgogoro wa ardhi katika Kata ya Kwembe, Kisokwa na Mloganzila unatokana na kuelezwa kuwa maeneo hayo yana hati ya Tanganyika Packers, hivyo wananchi wa eneo hilo wamevamia wakati hati nyingine ya eneo hilo ni ya kijiji ikionyesha wako kihalali na serikali kuchukua jukumu la kudai kuwa hati ya Tanganyika ndiyo halali.
Mnyika aliwataka wananchi waliolipwa stahiki zao mwaka 2008 kumpelekea vielelezo ili afuatilie fidia yao ya ardhi.
Safi sana Mnyika ila kuna mambo 2 unapaswa kuyajua.1: Kuna siku miaka ya nyuma tukiwa chuoni kikuu,Kikwete alikuwa anaongea na Wanafunzi wa elimu ya juu,wewe pia uliudhulia na bila kufahamu kulikuwa na kundi la watu walitaka wakutoe ndani na kukufanyia fujo moja ya hao watu uko naye na unamuona rafiki,hana upendo nawe,bila kujua mlimpokea toka CCM pale alipohama chama mkiwa Tarime
ReplyDelete2: Achana na hilo kundi linalompinga Zitto kwani Ubungo utaikosa kiulaini kama ukishirikiana na hao jamaa wSiopenda ukweli.