Tuesday, January 14, 2014

Madiwani Chadema waishambulia CCM, 20 Wavua Magamba wavaa Magwanda.

MADIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Mvomero, wakishambulia Chama cha Mapinduzi (CMM) kwa kushindwa kuwatatulia wananchi kero zao na kudai badala yake viongozi wake wamekuwa wakiwafanya watumwa katika nchi yao.

Hayo yalisemwa na Madiwani hao Katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Januari 13, Kijiji cha Kigugu Kata Sungaji, moja ya eneo lililokuwa na Mapigano ya Wakulima na Wafugaji, wilayani Mvomero, ambapo wanachama 20 wa CCM walivua Magamba na kuvaa Magwanda.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema Morogoro na Diwani wa Gairo Mjini, Dunstan Mwendi, alisema, Wananchi wa Kigugu wasidanganyika tena na Ubwabwa, Kanga, Tisheti, Skafu, bali wawachague Viongozi wa Chadema tangu Balozi hadi Mbunge ili wawaondolee kero zilizowatesa miaka Mitano.

“Mlidanganyika kutochagua, Wenyeviti wa Vitongoji, Mitaa, Vijiji, Diwani wa Kata, Jairos Msigwa, na Mbunge Matokeo Wardern, waliogombea kwa tiketi ya Chadema, kwa miaka Mitano cha moto mmekiona, kero zipo pale pale na ardhi mmeporwa”.alisema Mwendi akitaka wasifanye kosa hilo chaguzi za serikali za mitaa.

Diwani wa Kata ya Nyandira, Luanda Zengwe, alisema, wananchi wa Kigugu wasikubali kuishi maisha ya Panzi ya kuliwa na Kunguru kila siku, bali wakatae na wabadilike kwa kukichagua Chadema kwenye chaguzi za Serikali Mitaa, ambacho hata walipowekwa ndani kiwawekea dhamana.

Kwa Upande wake Diwani Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya, aliwaambia wananchi wa Kigugu waige Ujasiri wa wananchi wake (Mtibwa), ambapo wakidhurumiwa haki zao na Mwekezaji wa Kiwanda,anakesha nao Langoni kwa Mwekezaji hadi haki ipatine.

Aidha katika Mkutano huo Matawi Mashina matatu ya Chadema yalifunguliwa, ili kuwawezesha wananchi kwenda kutoa kero katika ofisi hizo ziweze kushughulikiwa, ambao wanachama waliovua magamba na kuvaa Magwanda walisema, waajuta kuchelewa maamuzi hayo,


1 comment:

  1. hongereni madiwani kwa kutambua mchango wa CHADEMA katika kuimarisha utu wa wa watanzania kwa ujumla, tuipende siku zote nchi yetu na tukipende chama chenye mwelekeo chanya,,CHADEMA

    ReplyDelete