Wednesday, January 29, 2014

Lisu Awaonya Viongozi wa Dini ‘Mna Mapepo na Majini Ibadani Mwenu


Bryson Nyeregete
MNADHIMU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lisu, amewaonya Viongozi wa Dini, Wachungaji na Mashekhe nchini kuwa, kuna Mapepo na Majini watu yanajipenyeza kwenye  Nyumba za Ibada ili kusambaza Virusi vya Udini.

Akizungumza katika Mkutano wa M4C-Oporesheni ya Pamoja Daima (OPD) uliofanyika jana Dodoma, Lisu alisema, Viongozi wa Dini wakiwaona Viongozi wa Chama Tawala (CCM) wanaojipitisha makanisani na misikiti kuomba kura, dawa yake si kuombewa ila watubishwe Dhambi zao za Ufisadi.

“Wapo Ma-CCM (Waislamu) wanaozunguzunguka misikitini kueneza na kuchochea Virusi vya Udini, Ukabila na Ukanda, na wapo Ma-CCM (Wakristo) wanaojikomba makanisani kueneza hayo hayo; Hao si waumini wa kweli ni majini na mapepo, si ya kuombewa, dawa ni sanduku la kura.

“Biblia Maombolezo. 5: 1-5 inasema,“ Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni;  Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri.Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane.Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa. Watufuatiao wa juu ya shingo zetu; Tumechoka tusipate raha yo yote”.

Lisu alisema, Nchi hii wageni wana thamani kuliko wananchi wake, hivyo ieleweka Chadema si Yesu aliyetundikwa Msalabani akasamehe, Chadema kikiona CCM inawanyanyasa wananchi tena kikitumia wasaliti ndani ya Chadema, kitaishughulikia CCM na wasaliti kwa  pamoja.

Heche aeleza sababu ya kuruka na chopa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa (BAVICHA), John Heche, ametoa siri ya kurusha Chopa tatu (Vikosi vya Anga na Ardhini) kuwa, ni ili kuwahi kuwazindua watanzania wasiuzwe kama nchi ilivyouzwa kwa wageni.

Heche aliieleza Dodoma jinsi watanzania wenzao walivyoteswa na Askari waliojiita Oporesheni Tokomeza Majangili, kumbe ni Tokomeza wananchi.  Kuna Mama aliyechomwa Singe tumboni na kutokea upande wa pili na wengine wakiambiwa wakanyage panga lililochomwa Gesi.

“Kuna watu wanasema tunatumia fedha vibaya kurusha Chopa tatu, nauliza, tumezichukua CCM? ….Hapana…; tumezichukua serikalini? ..Hapanaa….tumetoa maisha yetu, .tumefanya hivyo ili tuwahi kabla hawajawauza kama nchi ilivyouzwa kwa wageni.

“Kama viongozi wa serikali wanakwenda kuomba Vyandaraua na Kondom Ulaya, halafu wanaporudi huko angani wanapishana na wazungu wamebeba dhahabu, Pembe za Ndovu, Twiga na Rasilimali yetu, ninyi mtasalimika?

"Kama CCM itakuwa kichwa ngumu isiboreshe daftari la Kura, tutarusha Chopa 10”angani kila Kata nchini itatua”.alisema Heche na kushangiliwa.

Aliongeza, inasikitisha kuona Askari wetu wanawatokomeza wananchi, badala ya kuwakamata na kuwatokomeza Viongozi wa CCM waliotajwa bungeni kuhusika na kutoroshwa kwa twiga, ambapo pamoja na  urefu wa twiga walimkunja shingo hadi anaingia kwenye Ndege.

Aidha wananchi waliohojiwa baada ya Mkutano huo walisema, kama Askari Polisi wanaotakiwa kulinda raia na mali zao na sasa wamegeuka na kuwa Askari wa kuwinda raia na mali zao; Basi tumefika mahali pabaya

No comments:

Post a Comment