Wednesday, January 29, 2014

CCM Mvomero yaihofu Chadema na OPD, yawapiga Changa la macho Wananchi.

Bryson Nyeregete
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mvomero Morogoro, jana kimeonesha kutetemeshwa na M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Oporesheni Pamoja Daima (OPD), ambapo serikali na viongozi wa CCM wilayani, wamelazimika kuwapiga Changa la Macho wakulima na wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari Mtibwa.

Katika kuweweseka huko, Viongozi wa Serikali na CCM wilayani, imewalazimika kusimamisha kwa muda uzalishaji wa Sukari Mtibwa, hadi kitakapowalipa wafanyakazi, wastaafu na wakulima wadogo wa miwa, jambo ambalo imedaiwa ni kiini macho, M4C-OPD ikipita, dhuluma zitaendelea.

Tangu kubinafsishwa kwa kiwanda hicho kwa mwekezaji huyo kwa bei poa, wameshafika Mawziri 20 wakiwemo mawaziri wakuu watatu hadi sasa na Rais Jakaya Kikwete, lakini hakuna aliyetatua ucheleweshwaji wa malipo na dhuluma kwa wakulima na wafanyakazi, huku kesi Lukuki zikiwa mahakamani.

“Ni mbinu za Nguruwe kujiosha matope awe mbele ya watu na baadaye kuyarejea. Wakulima na wafanyakazi tumebaini tumepigwa Changa la Macho, ili kupumbazwa wakati Chadema watakapomwaga sera zao, CCM na viongozi wa Serikali waonekane wameshughulikia kero zetu.

“Mwekezaji wa Mtibwa amekuwa kama Sikio la Kufa halisikii Dawa kutokana na kiwanda kumilikiwa na Mabosi wa CCM na Serikali, ambapo kila mmoja ana mizizi yake hapo, hivyo hakuna wa kumfunga paka Kengele, maana kesi ya Nyani hawezi kuhukumu Tumbili”alisema mkulima mmoja.

Katika Kikao cha Wakulima na Wafanyakazi, kilichofanywa jana, Mkuu wa Wilaya, Antony Mtaka, kabla ya kufunga uzalishaji kwa muda, Meneja wa Kiwanda hicho Yahya, aliwahadaa wakulima kuwa malipo yao zaidi ya Sh. Bil. 1/- na malipo ya wafanyakazi Mil 200/- yatalipwa Februari, 2014.

Aidha mmoja wa Viongozi wa Chadema atakayetua na Chopa kiwandani hapo na kutaka jina lake lisitajwe alisema, Chadema M4C-OPD, tayari inazo taarifa za kiinterejensia kuhusu change la macho kwa wakulima na wafanyakazi wa mtibwa, na kudai waichague chadema imalize Uhuni na Usanii wa CCM na viongozi wake, na ikibidi kuwafikisha wahusika mahakamani.

“Walikolalia CCM sisi Chadema tumeamkia huko. Tuna taarifa, wafanyakazi wastaafu zaidi ya 110 wamekufa bila kupata mafao yao, na waliopata malipo yao yamechakachuliwa hayafiki hata Mil. 2/-; Ingawa mfanyakazi amefanya kazi zaidi ya miaka 30, fedha ya makato yao yote anayo mwekezaji kwenye Akaunti yake”.alisema.

No comments:

Post a Comment