Tuesday, January 21, 2014

Chadema kuwajengea uwezo Makatibu na Wenyeviti.

BRYCESON NYEREGETE
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Kata ya Sungaji wilayani Mvomero, kinakusudia kuwajengea uwezo Makatibu na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Kata hiyo, ili wajue kuweka Kumbukumbu za Chama katika hali nzuri.

Chama ngazi ya kata hiyo kimesema, kinakusudia kumuomba aliyekuwa Katibu wa Wilaya ya Mvomero, Dismas Ngeresha, ili awaelekeza Viongozi hao wa Vijiji namna nzuri ya kuandika taarifa na kuihoji Serikali ya Kata kiutendaji.

Akizungumza na mwandishi Mwenyekiti wa Kata ya Sungaji, Musa Kombo, alisema, Kata hiyo Mwaka huu imekuja kivingine ili kuhakikisha kinatunza vizuri Kumbukumbu za Chama, zikiwemo kero zinazotolewa na wananchi.

“Kwa kuanzia, tutamuomba aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema Wilaya ya Mvomero, Ngeresha, ili awanoe na kuwapa Msasa Makatibu na Wenyeviti wetu wa Vijiji, Vitongoji wakiwemo Mabalozi, ili wajue kuandika taarifa zao.

“Tunataka pia, Viongozi hao wapewe ueledi jinsi ya kuihoji Serikali ya Kata, Kuandika na Kutunza taarifa muhimu za Miradi, Kero za Wananchi na Mapato na Matumizi yanayosomwa kila baada ya miezi mitatu”. alisema Kombo.
Alisema, Kata yake imeandaa Kikao na Viongozi wote wa Kata, Vijiji na Vitongoji wa Chama hicho, ili kufikia muafaka wa kuendesha Semina hiyo ya kuwajengea uwezo, ili kuhakikisha Chama katika Kata hiyo kinakwenda na wakati.

Aidha baadhi ya Makatibu na Wenyeviti waliohojiwa, wamempongeza Mwenekiti wa Chama wa Kata hiyo Kombo na Kamati yake ya Utendaji, kwa kufikiri jambo ambalo, litakitoa Chama ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata, hatua moja zaidi.


No comments:

Post a Comment