DIWANI wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juliana Petro, ameunga mkono uamuzi uliofanywa na kikao cha Kamati Kuu na kuridhika wa kuwavua Nyadhifa walioandaa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013,” ndani ya Chama akisema, licha ya Umma watakaoathirika xaidi na Migogoro hiyo ni akina Mama na Watoto wadogo.
Petro alisema hayo jana akisema amepokea kwa huzuni kubwa kusikia taarifa za uasi ndani ya Chadema, wakati kimefika mahali pa kuingia Ikulu kwa asili mia 90%, halafu kuna watu wenye nafasi ya kuwaingiza madarakani waonawarudisha nyuma hatua asilimia 80%.
Akizungumzia uasi huo Diwani Petro alisema, Hivi nini maana ya ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013 ndani ya Chadema? Na kwa nini Mkakati huo ifanyike kwa kificho au siri badala ya Uwazi? Nakiomba Chama kichukue hatua kwa naochoma bendera za Chadema hadharani.
Petro alihoji, “Hivi watu wenye nyadhifa muhimu kama za wanaodaiwa kuwa na Mikakati ya Mabadiliko 2013 ambao kwa mtiririko wa kiuongozi wana nafasi kubwa za kuwa na vyeo vikubwa Chadema ikiwa madarakani, hawatosheki wanataka nini?”.
“Hapo ndipo ninaposhawishika kuwa kulikuwa na nia ya Uasi na si kutaka nafasi za nyadhifa kwa sababu Heshima na nafasi walizonazo tayari zilikuwa zinawapelekea kushika maeneo nyeti huko Chama kinakoelekea kwa namna yoyote ile”.alisema Petro kwa masikitiko!
Alikwenda mbali akisema, hapendezwi na M1 M2 M3 kufika walipo, bali anawataka waelewe Mtafaruku na madhara ya kisiasa yanayoendelea nchini ikiwa ni pamoja na kuchomwa Bendera za Chama ni kama yanaasisiwa na wao, kwa hiyo yanapoteza utu wao kwa Umma.
Aidha alidai, Uasi huo hauna tofauti na Majangili wa Meno ya Tembo kwa sababu kama Ndovu anavyouawa na kung’olewa Meno, ndivyo Waasi wanavyoweza kukiua Chama na kuking’oa Misingi ya kuwakomboa wananchi, jambo linalopoteza Wito wa wahusika kwa Umma.
Diwani Viti Maalum wapi? mwandishi afafanue.....
ReplyDelete