Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Phillemon Ndesamburo, amemtaka Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuacha kuyakalia mapendekezo ya serikali ya ufufuaji wa reli ya Moshi hadi Mombasa, nchini Kenya.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya soko la Manyema mjini hapa juzi, Ndesamburo alidai ukimya huo wa Tanzania umeipa nguvu Kenya kujenga reli na uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Taveta.
Alisema ikiwa Kenya imezindua ujenzi wa reli ya Voi-Taveta, sekta ya utalii na uchumi unaotegemea mipaka ya Holili na Tarakea iko shakani.
“Wakenya wanataka kutumeza kwa kutumia ule uwanja wa ndege wa kimataifa unaojengwa pale Taveta ambako ni jirani kabisa na Holili Wilaya ya Rombo na tayari wamezindua ujenzi wa reli ya kisasa itakayotumia treni ya umeme kutoka Voi kuja Taveta... nyingine ni ile ya Nairobi-Mombasa, Nairobi-Malaba/Kisumu na
Malaba/Kisumu hadi Kampala.
Mwakyembe amekaa na makabrasha Wizarani bila ya kutafakari wenzetu wamelenga kuua ukanda huu kiuchumi na hata utalii wetu,” alisema.
Wakati huo huo, Wakili maarufu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Elikunda Kipoko (41), amejiunga na chama hicho huku akiwatolea uvivu wasomi wanaotumika kuua demokrasia ndani ya vyama vyao.
“Mimi sijawahi kujiunga na chama chochote cha siasa hadi nilipoamua kuingia Chadema lakini sikubaliani na mambo ambayo wanafanya watu tunaowaona wamelelewa na kukua ndani ya taasisi kama hii.

Wasomi wengi wa leo wanatumika kuua demokrasia ama kuvivuruga vyama vyao; dhana ambayo haikubaliki,” alisema.
No comments:
Post a Comment