Kwa kuzindua rasimu ya sera hii ya Mabadiliko ya Tabianchi, CHADEMA kinakuwa chama cha kwanza Tanzania na Afrika nzima kuwa na sera ya namna hii, huku pia kikiwa ni moja ya vyama vichache duniani vyenye sera ya suala hili ,mtambuka.
Baadae itafuata sera ya elimu na uchumi na masuala mengine ya kijamii, kama vile afya, maji, ajira, vijana n.k.
UTANGULIZI
Mabadiliko
ya tabianchi ni jambo bayana linalotokea kwa dhahiri na kuathiri kila sehemu ya
dunia tuishiyo kwa kasi ya ajabu.
Nchi
yetu ya Tanzania ni mhanga mkubwa tayari imeshaathirika sana na mabadiliko ya
tabianchi, kama inavyobainika katika namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukame
uliokithiri na wa mara kwa mara ambao una athari kubwa sana kwenye kilimo,
usafirishaji, nishati, biashara, na sekta ya uchumi-jamii. Hivi sasa zaidi ya asilimia 70 ya majanga
yote ya asili yanayotokea Tanzania yahahusiana na mabadiliko ya tabianchi
vikiwemo ukame na mafuriko.
Wakati
wa matukio hayo, kilimo katika maeneo husika hudorora au kusimama kabisa,
mifugo mingi na wanyama pori hufa kwa kukosa chakula na maji na wakati mwingine
husambazwa na mkondo wa maji yaliyofurika.
Kutokana na ukame wa muda mrefu, Tanzania kwa vipindi tofauti, imekuwa
ikiathirika na ukosefu mkubwa wa nishati, ambao umekuwa na athari kubwa kijamii
na kiuchumi. Aidha, matukio ya mafuriko
ya mara kwa mara yamekuwa na madhara makubwa kwa binadamu, mali na miundominu.
Kilimo
na ufugaji, ambavyo ni shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wengi wa Tanzania,
kwa kiasi kikubwa zinategemea mvua za misimu.
Hii inamaanisha kwamba uchumi wa Tanzania, kwa kiasi kikubwa, unategemea
tabianchi. Kwa hiyo, ingependa kutoa
mwongozo katika jambo hilo. Hivyo,
waraka huu ni mwongozo wa Sera ya CHADEMA ya mabadiliko ya tabianchi.
Waraka
huu wa Sera unafafanua mpango mzima wa CHADEMA wa namna ya kushughulikia
mabadiliko ya tabianchi na masuala mengine husianifu. Inatarajiwa kwamba
viongozi wetu wa kisiasa katika ngazi za kanda, mikoa. Wilaya na kata wataiweka sera hii katika muktadha wa maeneo
yao ili iendane na maeneo husika.
Mwisho,
ninawashukuru Wajumbe wote wa Kamati Kuu kwa kuona umuhimu wa sera hii na kutoa
mawazo ya awali ambayo wataalamu wetu waliyatumia hadi kuwa na mwongozo kamili
wa sera.
Ninamshukuru
Bwana Finias Magesa kwa kuratibu mawazo yote mpaka kuandikwa kwa rasimu ya
awali ya waraka huu. Pia ninaishukuru
Kamati ya Wataalamu ya CHADEMA inayohusika na Sera kwa ajili ya kuuhariri
waraka huu na kuuboresha. Juhudi zao
zinapaswa kuthaminiwa sana kwani wamekifanya CHADEMA kuwa chama tofauti chenye
mawazo mbadala na bila shaka cha kwanza kuwa na sera inayotoa mwongozo wa mambo
yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa
namna ya kipekee kabisa, ninapenda kumshukuru kwa dhati, mshirika wetu muhimu
na wa muda mrefu, Konrad Adeneur Stiftung (KAS), kwa kugharamia uzalishaji wa
waraka huu.
………………………
Freeman
Aikael Mbowe
Mwenyekiti
wa Taifa,
CHADEMA
Hongera sana chadema kwa uzinduzi huo
ReplyDeletenashukuru sana kwa uwezo mkubwa wa wataalamu wa chadema kwa ubunifu huu mi nilikuwa naomba pia muweke sera ya KUPAMBANA NA MAJANGA, disaster preparedness SIJUI KAMA IPO LAKINI NI VITU AMBAVYO VINAENDANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI maana linapotokea janga hapa tanzania inachukua mda mrefu kutatuliwa mfano utaambiwa wataalamu na vifaa vinasubiriwa kutoka africa ya kusini
ReplyDelete