Monday, November 4, 2013

Mbowe ahimiza mshikamamo Bunda

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe, amewataka wanachama wa chama hicho Wilaya ya Bunda kuendeleza mshikamano ili kuimarisha chama hicho.
Mbowe alitoa kauli hiyo mjini Bunda jana wakati akitoa salamu za pole kwa familia ya aliyekuwa diwani wa Nyasura, Zamberi Mwisarya (CHADEMA), aliyefariki dunia Oktoba 28 mwaka huu kwa ugonjwa wa kiharusi.
Aliwashukuru wananchi wa kata hiyo na wilaya kwa ujumla kwa mshikamano waliouonyesha tangu kuugua kwa diwani huyo hadi kifo chake na kwamba wanapaswa kuuendeleza katika kipindi chote.
“Ndugu wafiwa, mimi na msafara wangu tumepita kuwapa mkono wa pole. Kuweni na uvumilivu huku mkimtegemea Mwenyezi Mungu na kwa kweli pengo la huyu kiongozi mwenzetu halitazibika,” alisema Mbowe.
Awali, mtoto wa marehemu, Emmanuel Mwisarya alimwambia Mbowe kuwa baba yake aliuugua kwa muda mrefu na alikuwa akitibiwa katika hosptali ya Bugando Mwanza hadi mauti yalipompata.
Baada ya kuhani msiba huo, Mbowe alisema wataelekea mjini Shinyanga ambako watafanya mkutano wa ndani wa Kanda ya Ziwa Mashariki na baadaye ataelekea Dodoma kuendelea na vikao vya Bunge

No comments:

Post a Comment