BARAZA la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) limewataka wanawake nchini kuungana na kufanya kazi kwa kushirikiana bila kujali itikadi za vyama, dini, rangi wala kabila.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa BAWACHA, Hellen Kayanza, alisema endapo wanawake nchini wakiungana wataweza kujikwamua kiuchumi, kielimu na hata kisiasa.
Alisema Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliopo hauko kwa ajili ya kumkwamua mwanamke kutoka katika hali ngumu ya kiuchumi bali uko kwa maslahi ya chama tawala (CCM) na watu wachache.
Alishauri UWT ivunjwe kwani haifanyi kazi ipasavyo na kiundwe chama kipya cha wanawake ambacho hakifungamani na chama chochote, ili kiweze kumsaidia mwanamke wa Tanzania kujikwamua kiuchumi.
“Ni wakati muafaka kuiga mifano kutoka kwa nchi za nje. Mfano wanawake wa Bern wako juu kiuchumi, kisiasa na kielimu kwa sababu ya umoja wao waliouunda,” alisema Hellen.
No comments:
Post a Comment