Chuo kikuu cha Alabama ina wanafunzi 16,000 katika Kitengo cha tiba. Hii ndio moja ya vyuo vikubwa nchini marekani katika maswala ya tiba, ikiwa na vitengo karibia vyote vinavyotibu magonjwa mbali mbali. Chuo hicho pia ufanya utafiti nchi nyingi duniani husasan afrika. Chuo hicho ushirikiana na nchi kama Afrika kusini, Zambia, Malawi, na Aljeria katika mambo ya utafiti na kutayarisha watafiti. Kadhalika imekuwa ikisaidia mataifa kama Saudi Arabia, Uchina na Qatar kutayarisha madaktari bingwa
Ikiwa ni moja ya sera za chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuweka mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya huduma bora za afya kwa watanzania, Dr. Slaa Amekuwa akizunguka nchini marekani ili kujifunza mambo mbali mbali hasa mafanikio ya vyuo kama hivi, na ni jinsi gani anaweza kupata ushirikiano na vyuo hivi ili kutayarisha madaktari wengi wa tiba na mabingwa ili kuiokoa taifa gharama kubwa ya kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi.
Kujibu ombi la Dr. Slaa, rais wa chuo cha tiba, ameahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania chini ya CHADEMA ili kujenga vyuo vya utafiti na tiba nchini Tanzania. Viongozi hao wameweka bayana nia yao ya kuisaidia Tanzania hasa ufisadi na urasimu uliopo utaondolewa. Naye kwa upande wake, Dr. Slaa amemuahidi kwamba, ufisadi utakuwa ni historia katika serikali ya CHADEMA.
Chuo hicho itakuwa tayari kuwatuma madaktari wake bingwa wa kila aina nchini Tanzania kusaidia katika mambo mbali mbali ya tiba itakayoambata na makubaliano na serikali ya CHADEMA ikiwemo kuwafundisha na kuwatayarisha madaktari 4,000 katika kipindi cha miaka (accelerated program) miwili kama walivyofanya nchini Bangladesh ili kupunguza uhaba wa madaktari. Hawa ni madaktari wasaidizi ambao wanaujuza Fulani. Madaktari wengine watahitaji miaka mitatu ili kuwa madaktari bingwa.
Dr. Slaa akiongozwa na Professor ambaye pia ni dean msaidizi
Dr. Slaa pamoja na viongozi wa Chuo cha Tiba
Dr. Slaa na Dean wakiwa kwenye maongezi ya kufanya kazi pamoja
Dr. Slaa akielekezwa kwenye chumba cha Mikutano na rais wa chuo cha tiba
Dr. Slaa akipewa maelekezo na rais wa chuo cha Tiba
No comments:
Post a Comment