Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Nyanda za Juu Kusini , kimejisifu kuwa kimezoa wanawake zaidi ya 600,000 ambao wana kuwa wanachama wapya.
Akiongea na gazeti hili Kaimu Ofisa Habari wa Chadema Nyanda za Juu Kusini Aidan Salehe alisema wanawake wengi wamejiunga na chama hicho na sasa idadi yao imefikia 660,000 .
“Tunawataka wanawake wajiunge kwa wingi kwenye chama hiki kwani ndicho chama mkombozi kwa watu wote,”alisema
Alisema Chadema ni kimbilio lao kwa sababu CCM imemeshindwa kuwakwamua wanawake kwenye umaskini mbali na kuwatumia kama mtaji wa kisiasa nyakati za uchaguzi.
Alidai kuendelea kuikumbatia CCM ni sawa na msemo usemao kichwa cha kuku hakistahimili kilemba na hivyo wanaotaka maendeleo yawanufaishe wote na sio watu binafsi kunufaika kwa maslahi yao .
Katika hatua nyingine Salehe aliwapongeza wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kwa kuvisusia vikao vya marekebisho ya mswada wa rasimu ya katiba mpya.
“Nawapongeza wabunge wa vyama pinzani vya siasa CUFna NCCR Mageuzi kwa kuungana kwa pamoja kwa ajili ya
kuipinga na kususia mijadala hiyo ya muswada wa sheria ya katiba tunawapongeza kwa ushirikiano waliouonyesha bila kujali hoja zimetoka katika chama gani”alisema
Nyanda za juu kusini inataka katiba mpya na inayowatetea wananchi na sio maslahi ya watu binafsi.
No comments:
Post a Comment