CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
(CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA KIKAO
CHA KAMATI KUU YA CHAMA KILICHOFANYIKA TAREHE 06-07/07/2013 KATIKA HOTEL YA
BLUE PEARL, DAR ES SALAAM.
Kamati
kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ilikutana katika Kikao cha dharura
kuanzia tarehe 06-07/07/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Dar es salaam kujadili pamoja na mambo
mengine Rasimu ya Katiba mpya na hali ya Siasa nchini.
Kamati
kuu imejadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali kama ifuatavyo:
1:0.
Hali ya Siasa Nchini.
Kamati
kuu imepokea taarifa ya hali ya siasa nchini na kuzingatia mambo yafuatayo:
a)
Shambulio
la Bomu Arusha.
ü Kamati
Kuu imesikitishwa na kulaani kwa nguvu zote tukio la Bomu Arusha
lililosababisha watu wanne kuuwawa na zaidi ya watu 70 wengine kujeruhiwa
vibaya.
ü Kamati
Kuu imeridhika kwamba shambulio hilo lililenga kuwaua viongozi wakuu wa CHADEMA
akiwamo Mwenyekiti wa Taifa Mheshimiwa Freeman A. Mbowe na Mbunge wa Jimbo la
Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mheshimiwa Godbless J. Lema na viongozi
na wanachama wengine wa CHADEMA waliohudhuria Mkutano wa kufunga kampeni za
udiwani katika Jiji la Arusha pamoja na kuvuruga Uchaguzi huo na kuinyima
CHADEMA ushindi mkubwa;
ü Kamati
Kuu imeridhika kwamba ushahidi uliopo wa vielelezo na wa mashuhuda wa shambulio
unaonyesha ushiriki wa moja kwa moja wa Jeshi la Polisi katika shambulio hilo;
ü Kamati
Kuu imefadhaishwa na kauli ya Serikali bungeni iliyolenga kulikosha Jeshi la
Polisi kwa kuhusika kwake na shambulio hilo dhidi ya CHADEMA na wananchi wa Jiji
la Arusha na kuilaumu CHADEMA wakati CHADEMA ndio mhanga wa shambulio hilo;
ü Kamati
Kuu imeshangazwa na kitendo cha Serikali kupuuza maafa yaliyowafika wananchi wa
Arusha kwa kushindwa kushiriki katika mazishi ya wahanga wa mauaji ya Soweto na
kuwashambulia kwa mabomu ya machozi, vipigo na maji ya sumu waombolezaji
waliokusanyika kuwaaga marehemu waliouawa kwenye shambulio;
ü Kamati
Kuu imesikitishwa na Rais Kikwete kuendelea kukaa kimya juu ya shambulio la
Arusha na kushindwa kwake kuunda Tume huru ya Kimahakama kuchunguza kwa uwazi
shambulio hilo. Aidha, Kamati Kuu inaamini kwamba ukimya huu wa Rais Kikwete na
kushindwa kwake hata kuwatembelea wafiwa na wahanga wengine wa shambulio hilo
ni ushahidi mwingine wa kuhusika kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali
katika kupanga na kutekeleza shambulio la Arusha;
ü Kamati
Kuu imefadhaishwa na kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano kuendelea na
vikao vya Bunge kama kawaida; kukataa kutoa mchango wowote kwa wahanga na kushindwa
kupeleka ujumbe wa Bunge kuwatembelea na kuwafariji wahanga na waathirika wa
shambulio kinyume na utaratibu uliozoeleka wa Bunge kutambua na kushiriki
katika majanga na misiba ya aina hii. Kamati Kuu inautaka uongozi wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano uwaeleze Watanzania kama maafa ya shambulio la Arusha
yalikuwa na tofauti yoyote na maafa ya shambulio la bomu la Olasiti, au na
maafa ya mabomu ya Gongo la Mboto, ajali ya MV Skargit au maafa mengine
yaliyosababisha Bunge la Jamhuri kuahirisha shughuli zake, kutoa michango kwa
waathirika pamoja na kupeleka ujumbe wa Bunge kuwafariji wafiwa na wahanga wa
matukio hayo;
Kutokana
na maelezo hayo hapo juu Kamati kuu imeazimia kuwa:
·
Iwapo Rais ataendeleza msimamo wa kutokuunda
tume huru ya kimahakama, Ushahidi uliopo
juu ya tukio la kurushwa Bomu Arusha utawekwa wazi muda utakapofika kwa wananchi wa
Tanzania; vyama na mashirika ya kiraia ya haki za binadamu hapa nchini na ya nje ya nchi; ofisi za kibalozi
za mataifa rafiki na Tanzania pamoja na jumuiya ya kimataifa ili yaishinikize
Serikali kuunda Tume huru ya Kimahakama kuchunguza shambulio hilo na matukio
mengine ya mauaji yenye sura ya kisiasa ambayo yamehusishwa na Jeshi la Polisi na
vyombo vingine vya usalama vya Serikali au vya Chama cha Mapinduzi;
2:0.
Hali ya Wananchi wa Mtwara.
Kamati kuu imepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa juu ya unyanyasaji, utesaji, ubakaji na uonevu wanaofanyiwa
wananchi wa Mtwara hivi sasa na vyombo
vya dola huku serikali ikikaa kimya juu ya jambo hili bila kukemea. Kamati kuu imejadili kwa kina
namna wananchi wa Mtwara wanavyofanyiwa na vyombo vya dola na kufikia maazimio
yafuatayo;
ü Vyombo
vya dola vitimize wajibu wake wa kulinda amani na mali ya raia na siyo kuwatesa
na kuwapiga wananchi kwa kuwasababishia
vifo kinyume na Haki za Binadamu.
ü Serikali
iwasikilize wananchi wa Mtwara na siyo kutumia ubabe, unyanyasaji, uonevu na
mateso kama mbinu za kuhalalisha kukubalika kwake kwa wananchi.
ü Rais
Kikwete alitangazie taifa “hali ya hatari” kwa mkoa wa Mtwara kama anaona kuwa
Mtwara ni hatari kwa kiasi hicho cha kulitumia JWTZ kuzunguka mitaani na silaha
za kijeshi ili taifa liweze kujua,Aidha kama jeshi la polisi limeshindwa
kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria atangaze kulivunja jeshi hilo mara
moja .
ü Serikali
iunde tume huru ya kuchunguza matukio ya mauaji,ubakaji,utesaji na ukiukwaji wa
haki za binadamu yaliyofanywa na vyombo vya dola na waathirika wote waweze
kufidiwa kwa mujibu wa sheria.
3:0.
Kauli ya Waziri Mkuu.
Kamati
Kuu imejadili kwa kina kauli ya Waziri Mkuu Bungeni kwamba ni sahihi kwa Jeshi
la Polisi nchini kuwapiga Wananchi wote wanaotumia haki zao za Kikatiba kupinga
sera au maamuzi ya Serikali. Kamati Kuu imeazimia kuwa:
ü Kauli
ya Waziri Mkuu imekiuka Katiba na sheria za nchi yetu zinazokataza Jeshi la
Polisi kutumia nguvu dhidi ya raia wasiokuwa na silaha na ambao wanatumia haki
zao za kikatiba kufanya maandamano;
ü Kamati
Kuu inaamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu inatoa Baraka kwa Jeshi la Polisi
kuendeleza vitendo vya ukatili na mauaji dhidi ya wananchi ambayo yamelifanya
Jeshi la Polisi la Tanzania kutangazwa kuwa moja ya majeshi katili ya polisi
katika Afrika Mashariki;
ü Kamati
Kuu inaungana na wananchi, taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa ambayo
yamelaani vikali kauli hiyo ya Waziri Mkuu na inawataka wananchi, taasisi na
mashirika hayo kuendelea kumlaani vikali Waziri Mkuu kwa kauli hiyo;
ü Kamati
Kuu inaamini kwamba Waziri Mkuu amepoteza sifa za kuendelea kuwa Waziri Mkuu na
inaungana na wananchi na taasisi ambazo zimedai Waziri Mkuu awajibike au
awajibishwe kutokana na kauli yake hiyo. Aidha, Kamati Kuu inawaelekeza Wabunge
wote wa CHADEMA washirikiane na Wabunge wengine wote wenye mapenzi mema na nchi
hii na ambao wanaamini katika utawala wa sheria waanzishe mchakato wa kumpigia
kura ya kutokuwa na Imani Waziri Mkuu kupitia Bunge;
ü Kamati
Kuu imewataka Jeshi la Polisi kama sehemu ya jamii ya watanzania kupuuza kauli
ya Waziri Mkuu katika utekelezaji wa kazi zao kwa kuwa kauli hiyo ni ya
uvunjifu wa Katiba na Sheria na inachochea uvunjifu wa amani.
4:0.
Uchaguzi wa Madiwani.
Kamati
Kuu imepokea taarifa kuhusu ushiriki wa CHADEMA katika Uchaguzi wa Madiwani uliofanyika tarehe 16/06/2013 katika kata 22.
ü Kamati
Kuu imeipongeza Sekretarieti na uongozi wa Kanda mbalimbali za CHADEMA kwa
maandalizi mazuri katika Uchagzuzi huo uliosababisha CHADEMA kuwapokonya CCM
ushindi katika kata 4 ilizokuwa imeshinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Kamati
Kuu imewapongeza wananchi kwa kuipatia
CHADEMA kura asilimia (47.7%) dhidi
ya CCM (49%) na (3.3%) za CUF.
ü Kamati
kuu imesikitishwa na vitendo vya fujo walivyofanyiwa viongozi, wagombea pamoja
na Wanachama mbalimbali katika sehemu
mbalimbali palipo fanyika Uchaguzi. Kamati Kuu imesikitshwa na kulaani
vitendo hivyo vikiwemo vya watu kukatwa
mapanga , kuchomwa visu na kubakwa kwa akina Mama na vijana wahuni
walioandaliwa na Chama cha Mapinduzi
ü Kamati
Kuu imelaani vitendo hivyo vya kinyama vilivyofanywa mbele ya jeshi la polisi na
Wakuu wa Wilaya.
ü Ili
kukabiliana na vitendo vya fujo
vinavyofanywa na vijana wa CCM
dhidi ya wagombea, Wanachama na viongozi wa CHADEMA, Kamati Kuu imeagiza
kwamba kitengo cha ulinzi cha Chama “Red
Brigade” kiimarishwe zaidi kwa kuhakikisha kuwa vijana wote wa Red Brigade Nchi
nzima wanapewa mafunzo maalum ya UKAKAMAVU yatakayoandaliwa katika Makambi
maalum katika mikoa yote.
ü Kamati
Kuu imejadili maandalizi ya Uchaguzi wa madiwani katika kata nne (4) katika
Jiji la Arusha. Kamati Kuu imepokea kwa
masikitiko taarifa juu mipango inayofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana
na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo
na viongozi wengine wa CCM mkoani Arusha katika kuhujumu zoezi la Uchaguzi kwa
kuwatisha wapiga kura kwa kutumia polisi na vijana wa Green Guard siku ya
uchaguzi.
ü Kamati
Kuu inamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kuchukua hatua stahiki kuzuia
harakati za polisi na CCM za kuvuruga Uchaguzi
na kutaka kujipatia ushindi kwa njia za hila. Aidha Kamati kuu imelitaka jeshi
la polisi kuheshimu maadili ya uchaguzi yaliyosainiwa na Serikali, Tume ya
uchaguzi na vyama vya siasa.
ü Kamati
Kuu imesikitishwa na Tume ya Uchaguzi kushindwa kuwazuia CCM kuendelea na
kampeni za Uchaguzi huku wakiwa wamezuia kampeni hizo kwa vyama vingine.
ü Kamati
Kuu imeendelea kuwapa pole wananchi wa Arusha kwa matukio mabaya wanaofanyiwa
na serikali ya CCM mkoani humo, na imewapongeza kwa kusimama kidete katika
kulinda haki na ukweli.
ü Kamati
Kuu imewaomba wananchi wa Arusha wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura
tarehe 14 Julai 2013, na imewataka wabunge wote washiriki katika kusimamia
zoezi la upigaji kura na uhesabuji kura siku ya Uchaguzi na wananchi wajitokeze
kwa wingi kulinda kura bila hofu.
5:0.
Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kamati
Kuu imejadili kwa kina sana maudhui yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba;
·
Kamati Kuu imetambua kazi kubwa iliyofanywa
na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kukusanya na kuchambua maoni ya wananchi
na kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya;
·
Hata hivyo, Kamati Kuu imetambua na kuainisha
mapendekezo mengine ya msingi ambayo yanastahili kuboreshwa zaidi katika Rasimu
hiyo;
·
Msimamo na maazimio ya Kamati Kuu juu ya
Rasimu ya Katiba Mpya yameainishwa na kuchapishwa katika kijitabu maalumu ambacho
kitazinduliwa katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika siku, tarehe na mahali
patakapo tangazwa hapo baadaye.
Imetolewa
na:
……………………….
Freeman
A. Mbowe, (MP)
Mwenyekiti
Taifa
No comments:
Post a Comment