TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMATI Kuu ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana katika kikao cha dharura kwa
siku mbili mfululizo, kuanzia tarehe 6-7 Julai, 2013, jijini Dar es Salaam.
Katika muda huo wa
siku mbili, kikao hicho kitajadili masuala mbalimbali, ambapo agenda zitakuwa;
Rasimu ya Katiba Mpya, taarifa ya hali ya siasa nchini, taarifa juu ya mfumo wa
uendeshaji wa chama kwa kanda (uzinduzi) na taarifa juu ya uchaguzi mdogo wa madiwani
katika kata 26, uliofanyika Juni 16, 2013.
Kupitia agenda za
kikao hicho, Kamati Kuu ya CHADEMA, itajadili, kuazimia na kutoa msimamo wa
chama juu ya masuala ya kitaifa na mengine yanayohusu maeneo mbalimbali, ikiwa
ni sehemu ya kufanikisha moja ya malengo ya chama ambayo ni pamoja na kutoa
uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganaizesheni thabiti kwa ajili
ya maendeleo endelevu ya jamii nzima ya Watanzania.
Imetolewa leo, Julai
5, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa
Habari CHADEMA
Msisahau kujadili kwa kina juu ya masuala ya usalama wa viongozi wetu na wa mikusanyiko ya wanachama.
ReplyDeleteMbuni mbinu nyingi za kukabiliana na vitendo vya kigaidi kama ilivyotokea hapa Arusha.