Sunday, June 2, 2013

Kwa Uroho huu CCM inajiaibisha

MWANDISHI Gustav Chahe, Iringa. Hivi karibuni alituhabarisha, Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo kimeumbuliwa kwa kutaka kumrubuni mgombea Udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ajitoe, ambapo uroho huo wa madaraka, ipo siku moja watairubuni hata maiti isiyosema.
Katika hatua nyingine, imetuhumika pia kumenaswa mpango wa kutaka kumrubuni Mgombea, Nafred Lukas, wa CHADEMA, ili naye aweze kujitoa katika kinyang’anyiro cha Udiwani katika Kata yake, na iwapo Viongozi wa CCM wilayani na mkoani humo, wanajihangaisha na Tabia hiyo, Inajiaibisha.
Mbali ya Uroho wa Madaraka unaotafutwa kwa nguvu ndani ya Chama Tawala ndani ya Kata na Wilaya mkoanai humo, imedaiwa kwamba wameandaliwa watuMaalum kwa lengo la kuhakikisha Mgombea wa Chadema , Chahe, ananunuliwa kwa Gharama yoyote ili asishiriki Uchaguzi huo.
Tuhuma za namna hiyo, zingewez kupuuzwa kama Mgombea Chahe, asingethibitisha kwa kukiri kupigiwa simu mara kadhaa na watu tofauti tofauti kutaka wakutane naye katika Kijiji cha Kidabaga, na wakati mwingine wakitaka wakutane naye mjini Iringa, maeneo ambayo alidai ni hatari kwake.
Nanukuu maneno ya Mgombea Chahe kwa Mwandishi, “Ni kweli napigiwa simu mara nyingi wakitaka nikutane nao eti kwa madai kuwa waniongezee uwezo wa kupiga kampeni lakini nakataa.
“Hata sehemu wanazotaka nikutane nao si nzuri kwangu, hali inayonipa wasiwasi,” alisema Chahe, na kuzitaja namba (zinahifadhi kwa sasa) za watu ambao wamekuwa wakimpigia na kuahidi kumsaidia.
Imedaiwa kwamba, katika uchunguzi uliofanywa awali, imebainika kwamba, wahusika wote wanaoendesha mpango huo na simu hizo, ni makada wa CCM na ambao baadhi ni wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenzake wa CMM.
Kimsingi nilitaka nionye kwamba, siku za hivi karibuni, tumeshuhudia watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino), wamekuwa wakiuawa na kukatwa viungo vyao, kwa udanganyifu kwamba, wakivitumia kwenye Biashara zao, zinawawezesha kufanikiwa, Jambo ambalo ni ndoto za alinacha.
Lakini pia, tumeshuhudia, Wazee na Vikongwe wenye Macho mekundu, wakiuawa ovyo nap engine kuchomewa nyumba moto na kufa kifo kibaya na agharabu miili yao isionekane kwa sababu ya Imani potofu kwamba wazee na vikongwe hao ni wachawi.
Ni rai yangu kwa Serikali sasa si Vyama kwamba, kama haitakomessha mtindo huu wa Viongozi wa Vyama vinavyoshindana na hasa Chama Tawala ambcho kimetuhumiwa katika hili. Mahali tunapoelekea sasa ni pabaya sana. Kutaibuka tabaka la mauaji ili mtui au mshindani mmoja wapo afe mwenzake ashinde.
Ninachokiona mbeleni, linatengenezwa kundi la kutafuta ushindi katika chaguzi mbalimbali zinazoendelea, na zile zinazokuja, ambapo zitakuwa na ajenda ya kupata ushindi na kuutupilia mbali Utu na Uzalendo wan chi hii, na hivyo kuzamisha kabisa matumaini ya kwamba nchi hii ni Kisiwa cha Amani.
Kumbe ndiyo maana tunashangaa watu wanatekwa na kwenda kutupwa mabwepande, ina maana ni watu fulani wana tama na uroho wa madaraka, hivyo wanatumia njia fupi (Shortcut) ili kupoteza uhai wa wenzao au kuwapa ulemavu wa viungo kwa lengo la wao kujipatia Vyeo na Uongozi ili waitwa  Wakubwa.
Hivi kweli hadi leo Nyakati za Digitali, bado wako watu wanaoaminishwa wapoteze haki zao kwa kupikiwa Ubwa na Nyama ya Kuku ya siku moja, halafu waumie miaka mitano?

BRYCESON NYEREGETE

No comments:

Post a Comment