KUMEKUWEPO na wimbi la baadhi ya Mahakimu, kutokuwepo mahakamani kuhukumu kesi walizopangiwa kwa mfululizo, hivyo kushindwa kuhukumu kesi na kukwamisha mwendelezo wake na watuhumiwa kurudi bila kesi zao kusikilizwa.
Hivi sasa wapo watu ambao wanateseka na kukaa gerezani kwa muda mrefu kwa sababu tu, watendaji na Hakinu hawapo, ambapo kukosekana kwao hakuoneshi mashiko zaidi ya kuwa na sababu nyepesi, na linalokwamisha kesi husika zisiendelee mahakamani.
Mahakama zimekuwa kama zinawaadhibu watu wasio na hatia! ambapo ningeitaka Mahakama na serikali kukomesha tatizo hilo na kuacha kuwaadhibu watu bila sababu! Ikibidi Hakimu asipokuwepo, awekwe Mbadala kazi iende.
Ningependa, ikitokea Hakimu hayupo, ni vizuri Uongozi wa Mahakama uweke Mbadal wake, kuliko kuacha watu wasubiri hadi wiki nyingine tena huku Watuhumiwa wakiendelea kukaa mahabusu bila sababu.
Sioni sababu za msingi zinazosababisha kesi zisizohitaji uchunguzi ambazo uchunguzi wake umekamilika kutotolewa uamuzi haraka, hasa wakati mwingine mtu kakanyaga Nyanya au hakuvaa Kofia Gumu (Helmet), apewe Faini aende.
Ni rai yangu, Serikali na Wiziri ya Katiba na Sheria na Ofisi hiyo, iweke muda maalum ambapo kesi za Jinai kwa mfano, Kesi za Madai, Biashara na kadharika, ziwe na muda ambao Ukifika, lazima kesi hizo ziwe zimekwisha.
Tukifanya hivyo tutawafanya mahakimu na wanaowasaidia Polisi na Magereza, kuwajibika na kuisaidia Mahakama, kutimiza malengo yao (Tentative Time), hivyo tunaweza kupima ufanisi wa vyombo hivyo na kuvizawadia.
Ukifanye uchunguzi Magereza nyingi; Utakuta Mahabusu wengi katika Magereza, hawafikishwi Mahakamani kwa sababu ya Mahakimu na Watendaji wa Mahakama kutokuwepo kwa sababu ya Udhuru mbalimbali, na Mahakama haiweki mbadala wake.
Kwa kuendekeza kuwaweka watuhumiwa kwa muda mrefu, hasa kwa wale ambao Kesi zao ni za kudhulumiana au kuiba Njiwa, anakaa gerezani kwa Gharama ya Bajeti ya Mahakama ya Wilaya au Mkoa, ni Matumizi mabaya ya fedha.
Nafahamu kesi zikishafunguliwa mahakamani sheria na kununi za uendeshaji zinataka kesi isikilizwe na itolewa uamuzi mapema ila kama kuna sababu ya msingi inayosababisha kuchelewesha uamuzi. Lakini si kesi ya kuiba Bata ikae miaka mitatu.
Tufike mahali Serikali, Bumge na Mahakama kama vyombo muhimu (Mihimili Mitatu), watendaji wa Magereza na Polisi, waelewe Thamani ya Kodi (Value for Money) ili tuwe na tahadhari ya Gharama hizo (Cost Conscious).
Haingilii akilini kuwaweka wamachinga 100 gerezani, wakala Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Robo mwaka, kwa kosa la kutembeza Mitumba, kosa la kuvuka na nguo kulipokuwa na msafara wa Mgeni toka nje. Huyu ni Mtanzania atembeze nguo wapi?
Wakati mwingine, kumekuwa na wingi wa kesi zinazofunguliwa unaokinzana na idadi ndogo ya watumishi waliopo kwa sababu kesi zingine ni ndogo zisizo na madhara kwa Taifa, mfano unamuweka ndani mzazi ambaye hajalipa michango ya Shule ya Msingi! Aibu.
Mashahidi kusababisha kesi kuahirishwa mara kadhaa, mahabusu kutofikishwa mahakamani, dharura kwa watendajii mahakamani, Hakimu, Mwendesha mashtaka, Wakili wa utetezi, mshtakiwa na wazee wa baraza, haya yamo ni ya uwezo wetu.
BRYCESON NYEREGETE
No comments:
Post a Comment