Saturday, June 1, 2013

CCM wamrubuni mgombea wa CHADEMA

VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameingia katika kashfa baada ya kuumbuliwa kwa njama za jaribio la kumrubuni mmoja wa wagombea udiwani wa CHADEMA ili ajitoe katika kinyang’anyiro hicho.
Katika hatua nyingine mikakati ya kutaka kumrubuni mgombea udiwani katika kata hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Nafred Lucas Chahe imegundulika.
Taarifa zilizopatikana ndani ya CCM zimeeleza kuwa wameandaliwa watu maalumu kwa ajili ya kuhakikisha mgombea wa CHADEMA Nafred Chahe ananunuliwa kwa gharama yoyote na kwa njia yoyote ili asishiriki katika uchaguzi.
Akithibisha kuwepo kwa mbinu hizo, Chahe alikiri kupigiwa simu mara kadhaa na watu tofauti tofauti kutaka wakutane naye katika kijiji cha Kidabaga na wakati mwingine wakitaka kukutana naye mjini.
“Ni kweli napigiwa simu mara nyingi wakitaka nikutane nao eti kwa madai kuwa waniongezee uwezo wa kupiga kampeni lakini nakataa.
“Hata sehemu wanazotaka nikutane nao si nzuri kwangu, hali inayonipa wasiwasi,” alisema Chahe, na kuzitaja namba (tunazihifadhi kwa sasa) za watu ambao wamekuwa wakimpigia na kuahidi kumsaidia.
Uchunguzi umebaini kuwa wahusika wote ni makada wa CCM na ambao baadhi ni wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea wa CCM.

No comments:

Post a Comment