Sunday, May 26, 2013

Wakuu wa Wilaya hawa; Wanatuhumiwa Kusababisha Migogoro,Fujo na Vurugu.

SHERIA ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 na Ibara ya 82 ya Katiba, inazuia viongozi wa Umma kutumia ofisi za Serikali, Kubagua, Kufanya Biashara, na kukumbatia itikadi za Vyama vyao kwa Manufaa binafsi dhidi ya Wananchi na Taifa.

 

Watendaji Kata, Madiwani, Wabunge, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa, wamekuwa wakitumia vitisho na dola kuzuia maamuzi halali ya Wananchi kuwang’oa viongozi wanaoshindwa kusoma mapato na matumizi au uzembe wa ubadhirifu wa mali za umma.

 

Mbali na kuvunja Sheria, Viongozi hao wanaendeleza Uvunjifu wa Amani, Migogoro, Fujo, na Vurugu sehemu mbalimbali za nchi, hasa pale wanapobaini haki yao inamong’onyolewa kwa hila ya kumnufaisha mtu, kikundi au Chama fulani cha siasa na kuwatosa walio wengi.

 

Kwa uchache, uchunguzi uliofanywa hivi karibuni mkoani Morogoro, wananchi kwa upande wao, wamewatuhumu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hassan Masala, kwa madai anafanya maamuzi kwa kukisaidia Chama chake Tawala (CCM), badala ya kuisaidia jamii.
Madai hayo pia yamemuunganisha Mkurugenzi wa Halmashauri yake, Azimina Mbilinyi, kuwa naye anafanya maamuzi kwa kukibeba chama tawala, kiasi cha kuwakumbatia baadhi ya viongozi kadhaa, ambao uovu wao umefikishwa kwake na hajachukua hatua.
Wanakijiji wa Mkamba-Kidatu, pia wanamlalamikia Mblinyi wakidai anaikumbatia Serikali ya Kijiji, ambayo iliuza Kiwanja cha ujenzi wa Kliniki kwa mfanya biashara moja kwa Mil. Saba, wakidai anamkasirikia maana vielelezo vya uovu huo anavyo.
“Ni aibu kwa Serikali ya Kijiji hiki, kutudanganya kuwa wamekopa Sh. Laki 550,000/- kwa Mfanyabiashara mmoja ili zisaidie Maendeleo ya Kijiji na kulazimishwa wananchi tuchangie kulipa deni hilo, wakatiho kumbe Uongozi unatakiwa urejeshe fedha za Kiwanja hicho”.alisema Methew Likwina mkutanoni.

 

Masala, analalamikiwa na wanakijiji wa Sagamaganga wilayani Kilombero kuwa, hivi karibuni waliung’oa uongozi wa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Mohamed Mkupika (CCM), kwa tuhuma mbalimbali, lakini ulikumbatiwa usiondolewe haraka.

 

Wanadai, hatua hiyo iliridhiwa na uchaguzi kusimamiwa na Masala wakipiga kura, lakini kuachia ngazi kulifuatiwa na Mizengwe ambayo walidai ilikuwa na sura ya kisiasa kuwang’ang’aniza wabaki, pamoja na maovu ya wazi.

 

Mkuu wa wilaya Mwingine anayelalamikiwa na wananchi kuwa ni chanzo cha Migogoro, Fujo na Vurugu, ni Elias Tarimo wa Kilosa, ambaye pamoja na Mkurugenzi wake Lameck Masembejo, wanadaiwa kuwa vyanzo vya vurugu za Uongozi wa Kijiji cha Ruaha, Kilosa.

 

Wananchi Ruaha wanadai, kama Masembejo alipewa onyo na Serikali akiwa Mkurugenzi  Korogwe, na kuhamishiwa Kilosa, atakuwaje muadilifu wa kuwapa haki, hasa za uchaguzi zaidi ya kunyenyekea na kuwafanyia kazi waliotunza makosa yake na kuyahamishia Kilosa?

 

Wananchi Ruaha wameingia katika vurugu na Serikali ya CCM mkoani Morogoro zilizojeruhi na kuharibu mali, kuziba barabara na kuchoma matairi, wakipinga kuwachagulia kiongozi wasiyemtaka, kufuatia tuzo ya Uenyekiti wa Kijiji hicho uliotolewa na Tume ya Uchaguzi bila kupiga kura halali.

 

Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero, Sarah Linuma, kabla hajakataliwa na Baraza la Madiwani  kufanya naye kazi naye kwa tuhuma za ufujaji  wa Mil. Mia 800/-, amelalamikiwa na wananchi, aliwakumbatia viongozi wabovu waliokataliwa wabaki, akijua wanavunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 na Ibara ya 82 ya Katiba.
nyeregete@yahoo.co.uk  0715933308

No comments:

Post a Comment