Monday, May 27, 2013

Lema: Makuyuni chagueni CHADEMA

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbles Lema, amewataka wakazi wa kata ya Makuyuni kumchagua Japheti Sironga kuwa diwani wao ili kuleta ukombozi wa wananchi jamii ya kimasai.
Lem alitoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi huo mdogo.
“Safari hii hata sisi tulipata mshtuko kwa kupata mgombea msomi mwenye master (shahada ya Uzamili) ambaye ameamua kwa dhati kurejea nyumbani kuomba ridhaa ya kuwakomboa ndugu zake. Sasa ni wajibu wenu wananchi kumchagua, ili dhamira yake kwenu itimie,'' alisema Lema.
Aliwahakikishia wananchi wa Makuyuni siku moja baada ya kumchagua Sironga kuwa diwani atakwenda naye mjini Dodoma kumkutanisha na mawaziri, ili awasilishe kero zao ambazo zimekua sugu.
Naye mgombea huyo, Japheti Sironga, akiwahutubia wananchi na kuomba kura aliwaahidi kuwa kazi yake kubwa ya kwanza wakimchagua ni kuhakikisha rasilimali ardhi iliyopo Makuyuni inawanufaisha wananchi wote.
“Mkinichagua nitakikisha ardhi yote ambayo hivi sasa inamilikiwa kinyemela na vigogo wa Monduli ikiwemo Ranchi ya Manyara inakuwa ya manufaa kwa wananchi wote,”alisema.
Kuhusu kero ya maji, alisema atahakikisha anafuatilia miradi yote ambayo ilikabidhiwa kwa wawekezaji ambao hawafahamiki walipo ili kujua fedha za miradi hiyo zimeliwa na nani na kuwafikisha katika vyombo
husika.
Alisema Rais Jakaya Kikwete alipokwenda Makuyuni alipewa shukurani na mbunge wa Monduli, Edward Lowasa kuhusiana na mradi wa sh bilioni mbili uliopelekwa katika kata hiyo, lakini mpaka sasa mradi huo haujulikani ulipo, hivyo itakua jukumu lake kufuatilia mradi huo kuona unafanya kazi.

No comments:

Post a Comment