Thursday, May 23, 2013

Wabunge wasiwe watoro majimboni Mwao!


KATIKA hali isiyo ya kawaida nchini, baadhi ya wabunge wameyatelekeza majimbo yao kwa kutorudi kusikiliza kero za wananchi na kutimiza ahadi zao.
 
Imefikia baadhi ya wanasiasa wanadhani majimboni ni sehemu ya kuchota kura na kuwaacha wananchi waendelea kubaki kama walivyo kana kwamba wapo kisiwani kusiko na msaada, huku hawajui ni lini wataokolewa labda pale tu watakapofanya maamuzi magumu ya kuitosa.

Wananchi katika Majimbo mbalimbali nchini wamemekuwa wakilia na tabia ya wabunge wao waliowachagua ili wawawakilishe bungeni, kwa bahati mbaya baadhi yao wamekuwa wasaliti kwa wapiga kura wao, kutokana kuonekana mara chache kwenye majimbo yao.

Hali hiyo imewapelekea wakiwa wabunge hao wakiwa bungeni, hulipuka kusema mambo ambayo hawakuagizwa na wapiga kura, kitendo ambapo muda wao huishia kuwashukuru wake zao, kutukana matusi, sanasana kulala usingizi, bila kusemea kero za majimboni mwao.

Kutokana na wabunge kuasi majimboni kuongee na wapiga kura nini wakazungumze bungeni dhidi ya kero zinazowasibu, utashangaa wanabakia kusikiliza wapinzani wamepinga kitu gani ili waanze kuwashambulia, badala ya kuwatetea wapiga kura wao.

Uchunguzi ambao umefanywa na kubaini mapungufu kadhaa ya wawakiliishi hawa, wabunge karibu wote imebainika wanakwenda mara chache sana majimboni mwao, na wanaweza kwenda na wasifanye mikutano yoyote, jambo linalowaudhi wananchi.

Kuthibitisha malalamiko ya wapiga kura na wananchi wa baadhi ya majimbo, ukichunguza kwenye mahudhurio yao kwenye vikao vya DCC na RCC, wabunge hao ni nadra kuhudhuria kwenye vikao hivyo.

Mara kadhaa ukisoma kwenye mihutasari utaona labda ni mbunge mmoja tu alikuwepo, lakini wengine wote utakuta imeripotiwa ni udhuru tuuu, jambo ambalo linawakasirisha sana wapiga kura na wapenzi wa vyama husika.

Mwananchi mmoja wa Mvomero ambaye ni Kiongozi wa Chama kinachotawala (CCM) aliyeomba asitajwe jina lake kwa kuhofia kukemewa alichodai ni kukolimbwa kwa kudai haki alisema, ”Tumechoshwa na wabunge wanaojifanya wazaliwa wa wilaya na mikoa ya maeneo yetu,  na baadaye wanahamishia makazi na shughuli zao Dar es Salaam.

“Kimsingi tunatafakari kwa umakini Udanganyifu huu na Usanii tunaofanyiwa na baadhi ya wabunge wetu, kuchota kura na kamwe tutaendelea kubaki kama tulivyo kama watu walio kwenye kisiwa na hatujui lini tutaokolewa labda pale watakapofanya maamuzi magumu ya kuitosa CCM mwaka 2015”. 

Wakati wapiga kura wakiwalalamikia wabunge wasiochukua maoni yao na kuwatetea bungeni, Rais Dk. Jakaya Kikwete kwenye kikao chake na wabunge wa CCM Dodoma hivi karibuni, amekea tabia ya wabunge watoro wasiotembelea majimbo yao.

Katika kikao hicho kilichofanyika mjini Dodoma, Imefahamika Rais amekaririwa akisema baadhi ya wabunge wameyatelekeza majimbo yao kwa kutorudi kusikiliza kero za wananchi na kutimiza ahadi zao, kitendo ambacho ni hatari kwa wao kurudi kwenye majimbo yao na CCM.

Hivi karibuni bila ya kuuma uma maneno kwa Mkutano wa hadhara, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amewachongea Wabunge wa Mkoa wa Tabora (CCM) kwa wananchi, akidai ni wasaliti kwa wapiga kura wao, ambapo baadhi ya wananchi walimuunga mkono.

Ni rai yangu Wabunge wa namna iliyoelezwa, wajikague wajitathimini, ili wasiwe watoro majimboni na kuwa Viwete, Bubu, Vipofu na wagumu wa kuwatetea wapiga kura wao, ingawa ni rahisi kudai posho zao, wanahatarisha uwakilishi wao 2015.


0715-933308

No comments:

Post a Comment