Thursday, May 23, 2013

BAJETI YA WIZARA YA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


NDUGU WATANZANIA WENZANGU.
MIMI NI MWANAFUNZI NINAYESOMA KATIKA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI - MWEKA (COLLEGE OF AFRICAN WILDLIFE MANAGEMENT - MWEKA) KILICHOPO MOSHI - KILIMANJARO.
 
KERO YANGU KUBWA NI KUHUSU ADA INAYOTOZWA NA CHUO HIKI HAIKIDHI KABISA HALI YA WATANZANIA WENGI KWANI LICHA YA SERIKALI KUZUIA ULIPAJI WA ADA KWA DOLA KATIKA VYUO NCHINI TANZANIA, BADO CHUO HIKI CHA WANYAMAPORI - MWEKA KINAENDELEA KUTUTOZA ADA KWA DOLA INGAWA LICHA YA KUWA KIPO NCHINI TANZANIA PIA KINAMILIKIWA NA SERIKALI.
 
ADA INAYOTOZWA NA CHUO HIKI NI KUBWA MNO KWANI HUWA TUNALIPA HADI DOLA ZA KIMAREKANI 3520 KIASI AMBAPO WATANZANIA WENGI HUWA INATUUMIZA SANA UKIZINGATIA WENGI TUMELETWA NA TCU PASIPO KUJUA ADA YA CHUO HIKI.
 
NINAMUOMBA WAZIRI KIVULI WA WIZARA YA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PINDI AWASILISHAPO BAJETI YAKE BUNGENI, ALIZUNGUMZIE NA SUALA HILI LA ADA KUWA KUBWA AMBAPO HUSABABISHA WATANZANIA WENGI KUSHINDWA KUMALIZA ELIMU YAO AU KUTOJIUNGA KABISA NA CHUO HIKI LICHA YA KUPATA NAFASI KWANI ADA HII INATUUMIZA SANA.
 
MAELEZO ZAIDI KUHUSU ULIPAJI HUU WA ADA UNAPATIKA KATIKA KITABU CHA TCU (TCU GUIDE BOOK) NA PIA KWENYE ANUANI YA CHUO HUSIKA (http://www.mwekawildlife.org/).
 
TUNAAMINI SUALA HILI LITASHUGHULIKIWA KABLA YA KUANZA MWAKA MPYA WA FEDHA 2013/2014.

No comments:

Post a Comment