Wiki mbili zilizopita Polisi mkoani Arusha Ilimfungulia kesi baada ya kumshikilia kwa siku 3 Mbunge wa Arusha mjini mh GODBLESS LEMA kwa kile wanachodai polisi kua ni Uchochezi baada ya Mkuu wa mkoa Arusha Magesa Mulongo kuzomewa na wanafunzi wa chuo cha Uhasibu. Hii ilitokea baada ya mkuu wa mkoa kwenda kuwasikiliza wanafunzi waliotaka kuandamana kwa sababu ya mwanafunzi mwenzao mwenyeji wa mkoa wa Iringa kuchomwa kisu na hatimae kufariki. Mkuu wa mkoa alishindwa kuelewana na wafiwa kitendo kilichosababisha Kuzomewa na ndipo alipoamuru polisi kuwatawanya kwa Mabomu ya Machozi.
Mbunge Lema aliekua kwenye tukio ilibidi aondoke na hata kuliacha gari lake na ndipo polisi walilichukua. Lema alikamatwa siku mbili baadae na kunyimwa dhamana kituo cha polisi hadi siku alipopelekwa Mahakamani na kufunguliwa kesi nne. Lakini mahakama ilimfutia kesi tatu na kubakiza moja ya Uchochezi pia ilimpa dhamana.
Baada ya Lema kuachiwa alisindikizwa na Wafuasi wake kwa maandamano makubwa hadi Ofisi za mkoa za chadema,maeneo ya NHC Ngarenaro.
Jumapili wiki ya jana Polisi mkoani Iringa ikamkamata mbunge wa Iringa Mch Peter Msigwa kwa wanachodai kuwa ni Uchochezi. Tofauti ya Lema ni kuwachochea Wanafunzi. Lakini Msigwa ni kuwachochea Wamachinga!
Msigwa alinyimwa zamana polisi na kufikishwa mahakamani jana jumatatu na kufunguliwa kesi ya uchochezi lakini Mahakama ilimuachia kwa dhamana. Kama Lema Mh Msigwa baada ya kuachiwa alisindikizwa kwa Maandamano makubwa na Wafuasi wake.
Ninachojiuliza wabunge wa CDM karibia wote ukiwaondoa wachache wa viti maalum wamekua wakikamatwa mara kwa mara na Polisi na sijui kama kuna ambae hana Kesi zaidi ya moja!!
Tulishuhudia mwaka juzi Kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni mh Mbowe akiletwa kwa Helkopita chini ya ulinzi mkali kutoka Dar kuja Arusha kwa kesi ya kutohudhuria mahakamani.lakini baadae aliachiwa huku kukiwa kumetumika garama kubwa.
Tundu Lissu nae tuliona akikaa Mahabusu kwa zaidi ya siku mbili kwa kosa hilo hilo la Uchochezi kwa kujaribu kuwatetea Wananchi waliouawa na polisi kwa kile kinachodaiwa kutaka kuvamia Mgodi wa Mwekezaji.
Kwa ujumla Wabunge karibia wote wa CDM wana kesi zaidi ya moja na haswa ya uchochezi. Naomba kujua Wabunge wa Ccm huwa sio wachochezi na kama sio kwanini ni Cdm tu? Je ni Wanaonewa, Ni Wakorofi au ni DEMOKRASIA imekua?
Sokoine
No comments:
Post a Comment