Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya bunge kwa siku ya jana, kwa maana ya order paper, Wizara ya Maliasili na Utalii ilipaswa kuwasilisha hotuba yake ya bajeti (makadirio ya mapato na matumizi) ya mwaka 2013/2014 siku ya jana Jumatatu, Aprili 29, 2013.

Ndiyo maana hata taratibu zote zilifuatwa, ikiwemo uwasilishaji wa hati mezani, ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni kwa wizara hiyo, wote waliwasilisha hotuba zao.

Taratibu za bunge ni kwamba, ukiwasilisha hati (yaweza kuwa hotuba, taarifa, kauli au randama), wakati huo unapaswa kuwa umewasilisha hati husika kitengo cha hansard na uchapaji, kwa ajili ya taratibu za kumbukumbu na uchapaji kwa ajili ya kuwagawia wabunge ndani ya ukumbi.

Kilichotokea jana kila mtu anakijua. Serikali na bunge wakaboronga tena katika bajeti ya Wizara ya Maji, ilikuwa ni baada ya miongozo ya akina Kabwe Zitto, Tundu Lissu na John Mnyika. Serikali ikaanguka tena bungeni. Spika kama ada akaiokota na kuwaambia warudi wakarekebishe kisha warudi session ya jioni. Ratiba ya vikao haikuwa sawa tena.

Hivyo ratiba ya kuwasilisha hotuba za Wizara ya Maliasili na Utalii siku ya jana ikashindikana. Lakini tayari hotuba zikawa ziko uchapaji na hansard.

Hotuba inayosambaa mitandaoni

Kwa hiyo hadi jana asubuhi hotuba hiyo haikuwa siri tena. Hata mtoto wa chekechea angeweza kuipata. Sasa kilichotokea ni CCM kupata soft copy ya hotuba hiyo (ofcourse mnajua wameipata wapi, ofisi za serikali hapa bungeni), kisha wakawapatia vijana wao eti waonekane ni credible kiasi cha kupata information ndani ya CHADEMA na Kambi ya Upinzani Bungeni. Nonsense calculation.

Wanataka kuonesha kuwa Kambi ya Upinzani iko loose na CHADEMA haiko makini, which ofcourse they are also very wrong, hata wao wanajua. Lakini pia wanataka tuanze kutumia muda wetu hapa kukimbizana na watu waliochukua nguo zetu wakati sisi tukioga bafuni, ili watu wasione tofauti ya yule mwehu aliyechukua nguo zetu...hatutawakimbiza. Tusiwakimbize, wote tusije kuonekana wehu...

Kitu kikubwa kinachowatisha CCM, ambacho walitaka wajue msimamo wa CHADEMA kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni ni pamoja na masuala ya ujangili ambako viongozi waandamizi wa chama hicho wamehusishwa na hawana utetezi na suala tete la Loliondo, ambako tunajua wamempanga yule mbunge wao kiongozi msema ovyo aje kuzungumza kwa nia ya CCM kumruka Waziri wa Serikali yao bungeni. Hivyo ndivyo ripoti aliyowaandikia baada ya kutembelea kule inashauri.

Hatua zilizochukuliwa

Hotuba hiyo ya Kambi ya Upinzani Bungeni, imebadilishwa. Hivyo naombeni mtulie, hotuba genuine ni ile tutakayoisambaza kwa wananchi, ikiwemo kwenye vyombo vya habari, social na mainstream, muda si mrefu na hapa jamvini mtapata nakala kama ilivyo ada. Hiyo ndiyo inastahili kujadiliwa.

Kuhonga waandishi

CHADEMA kitakuwa chama cha siasa cha mwisho kujihusisha na kitendo au vitendo vya namna yoyote vinavyohusu rushwa, ufisadi, ubadhirifu au kuminya haki yoyote ile, ikiwemo kuhonga waandishi wa habari.

Ili CHADEMA kifanye uchafu huo, maana yake Idara ya Habari, chini ya Kurugenzi ya Habari na Uenezi, iwe imehusika. Hakuna kitu cha namna hiyo...

Kuna watu ni mabingwa wa kujisema wao walivyo, kwa kuwarushia watu wengine tabia zao. Yaani kwa sababu CCM imefikia mahali inahonga hata kupata wanachama kutoka vyama vingine na kununua baadhi ya wanahabari ili kufanya kazi ya kuchafua CHADEMA bila ushahidi, wanafikiri chama makini kama CHADEMA kinaweza kufanya hivyo hivyo. Guilty consciouness. Ni ugonjwa nao.

Wanaogopa nini

Kama chama chao kimefikia hatua kinaongozwa na watu wenye tuhuma nzito kama hizi, tena wengine wanatangazaa dunia nzima, hadi kutolewa kwenye majarida, waache Watanzania waone, wajue na wajadili. Wasiogope mijadala, tena inayotokana na ushahidi usiopingika!

Kama CCM ni hawako hivyo ambavyo kila mtu mwenye akili timamu anawaona, kwa nini wanaogopa?

Hotuba rasmi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii, itakayosomwa na Kamanda Peter Msigwa, itawekwa hapa mara tu wakati wa kusomwa bungeni utakapofika.

Makene