Wednesday, May 1, 2013

Chadema walalamikia utaratibu wa Katiba

Katibu Chama cha Demokrasia na maendeleo(Chadema), Wilaya ya
Rombo, Venance Semali amelalamikia utaratibu uliotumika katika kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba wilayani hapa.
Semali alisema kuwa katika Kata ya Kisale-Msaranga utaratibu ulikiukwa ambapo waombaji hawakupewa nafasi ya kujieleza jambo ambalo ni haki yao ya msingi.
Pia alisema malalamiko mengine ni kwamba wajumbe waalikwa walitolewa nje ya kikao jambo ambalo lilitia shaka kwamba uchaguzi ulipangwa na haukufanyika kwa njia ya kura za siri, na hivyo kufanya uchaguzi huo kutokuwa wa ukweli na uwazi.
Aidha alisema kuwa katika kata karibu zote za wilaya ya Rombo uchaguzi huo hakufanyika kwa kuzingatia misingi ya Kidemokrasia bali ulikua ni wa kisiasa.
Wajumbe hao waliwasilisha malalamiko yao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kwa njia ya maandishi na Mkurugenzi huyo katika barua yenye kumb namba HWR/C.50/38 akamwagiza Ofisa Mtendaji wa kata hiyo uchaguzi urudiwe, ili kuondoa manung’uniko.(Mwandishi Wetu)e Gervas)

No comments:

Post a Comment