1. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Kufuatia marekebisho kadhaa ya kanuni
hususan zinazolenga kwa sasa Utaratibu wa Kutunga Sheria kuhusiana na mambo ya
fedha, nasi kama Kambi Rasmi ya Upinzani tutafanya marekebisho katika utaratibu
tutakaotumia katika kutoa maoni yetu kwa Serikali.
Kwa muda mrefu, kufuatia utaratibu wa mfumo
wa bajeti ulivyokuwa huko nyuma, tulitumia muda mwingi kuishauri serikali namna bora ya kuboresha
bajeti na utendaji wake wa kazi. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana, serikali
hii imekuwa siyo sikivu vya kutosha hata kama pale ambapo ushauri unaotolewa
uko wazi kwa masilahi na mustakabali mwema wa Taifa letu.
Aidha, pale ambapo Serikali imechukua maoni
yetu, mara nyingi imekuwa haina ustaarabu wa kutambua, kukiri na kushukuru
mchango wa Kambi ya Upinzani, bali mbele ya macho ya umma imeendelea kutoa kebehi
kujaribu kuuaminisha umma kuwa vyama vya upinzani havina ufumbuzi mbadala kwa
matatizo yanayolikabili Taifa.
Mheshimiwa Spika,
Tatizo kubwa la Serikali inayoongozwa na
CCM ni kukosa weledi wa kutekeleza kikamilifu vipaumbele vyake pamoja na
kuviainisha kupitia Mpango wake wa miaka 5, bajeti na programu mbalimbali. Hali
hii inaweza kutafsiriwa kama uwezo duni wa kusoma alama za nyakati ikiwemo
kubuni na kusimamia inachokiamini. Ni dhahiri vilevile unapolazimika kufanya
jambo usiloliamini au lisilo kipaumbele chako, bali cha kulazimishwa na
mazingira unatekeleza bila kujua undani wake na hatma yake ni kuharibu zaidi.
Mheshimiwa Spika,
Kwa kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mtambuka, Mwaka
huu tutajielekeza kuzungumzia mambo makuu machache ambayo sisi tunaamini ni
vipaumbele muhimu ambavyo Waziri Mkuu na wasaidizi wake wanapashwa kuja na
majibu ya kueleweka kwa Watanzania. Aidha, mengine yatawasilishwa kupitia
hotuba zetu mbalimbali katika Wizara husika.
2.
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA MSTAKABALI WA
TAIFA
Mheshimiwa Spika,
Tarehe 18 Novemba, 2011 Bunge lako tukufu lilipitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya
mwaka 2011. Kufuatana malalamiko mengi kuhusu utaratibu uliowekwa kwa
mujibu wa Sheria hiyo na kufuatia vikao kati ya Mheshimiwa Rais na Kamati
Maalum ya CHADEMA pamoja na wadau wengine, Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho
wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge hili uliofanyika mwezi Februari mwaka 2012.
Marekebisho hayo yalikuwa ni awamu ya kwanza
ya awamu tatu za marekebisho ya Sheria hiyo kwa mujibu wa makubaliano yetu na
Mheshimiwa Rais. Awamu nyingine mbili za marekebisho zilitarajiwa kukamilika
kabla ya mwisho wa mwaka jana, yaani 2012. Hata hivyo, hadi nasoma maoni haya
leo hii, Sheria ya Marekebisho ya Katiba haijafanyiwa marekebisho mengine
yoyote.
Mheshimiwa Spika,
Mara baada ya marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba kupitishwa mwaka jana, Mheshimiwa Rais alifanya uteuzi wa
wajumbe na watendaji wakuu wa Tume na Tume yenyewe ilianza kazi mwezi Mei,
2012. Kwa maana hiyo, hadi kufikia leo Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeshafanya
kazi kwa karibu mwaka mmoja.
Kwa masikitiko makubwa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inapenda kulijulisha Bunge lako tukufu kwamba katika kipindi
hiki mtiririko wa matukio kadhaa ndani na nje ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
imethibitisha kwamba haina weledi, dhamira au nia ya kusimamia mchakato huru
usiofungamana na upande wowote.
Katika mwaka wa kwanza wa mchakato wa
upatikanaji Katiba mpya, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imethibitisha hofu
tuliyokuwa nayo toka mwanzo kwamba lengo la mchakato wa Katiba Mpya uliowekwa
kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ni kuhakikisha kwamba mabadiliko
pekee yakayokuwepo ni yale yenye kulinda matakwa ya CCM na Serikali yake au
yale pekee yatakayokuwa na Baraka za “Status Quo”.
Mheshimiwa Spika,
Kwanza, Tume haikuweka utaratibu wowote madhubuti
wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala yote yanayohusu Katiba Mpya ili
kuwaandaa wananchi kuchangia maoni yao kwa Tume wakiwa na uelewa wa kutosha.
Badala yake, wakati wa mikutano ya Tume ya kupokea maoni ya wananchi, wajumbe
wa Tume walipewa jukumu la kuwaeleza wananchi juu ya Katiba Mpya kwa muda
usiozidi nusu saa!
Kwa kulinganisha, Tume ya Katiba ya Kenya
ilifanya kazi ya kutoa elimu kwa umma kwa nchi nzima kwa muda wa miezi sita
kabla ya kuanza kukusanya maoni ya wananchi wa Kenya juu ya Katiba Mpya. Matokeo
yake ni kwamba mchakato wa Katiba Mpya wa Kenya umeiletea nchi hiyo Katiba Mpya
ya mwaka 2010 ambayo imeanza kudhihirisha ubora wake kwa jinsi ambavyo mambo
yatokanayo na Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo wa hivi karibuni yalivyotatuliwa.
KUENDELEA BONYEZA READ MORE
Mheshimiwa Spika,
Pili, muda uliowekwa na Tume wa kukusanya
maoni ya wananchi ulikuwa mdogo sana ukilinganisha na ukubwa wa nchi yetu na
wingi wa Watanzania. Katika Majimbo karibu yote ya uchaguzi Tanzania Bara, Tume
iliendesha wastani wa mikutano saba kwa kila jimbo kwa lengo la kukusanya maoni
ya wananchi.
Katika mikutano hiyo wananchi walitakiwa
kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya kwa muda wa dakika tano kila mmoja na mikutano yenyewe ilichukua muda wa masaa
matatu ikiwa ni pamoja na muda wa kutambulishana wajumbe wa Tume na mambo
mengine yaliyo nje ya kuchukua maoni ya wananchi.
Mheshimiwa Spika, matokeo yake ni kwamba kwa mujibu wa
maelezo ya Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Sinde Warioba kwa waandishi habari
tarehe 5 Januari mwaka huu, hadi awamu nne za kukusanya maoni ya wananchi
zinakamilika tarehe 19 Desemba, 2012, Tume ilikwisha kufanya mikutano 1,776 kwa
nchi nzima. Aidha, kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti Warioba, hadi kufikia
kipindi hicho wananchi wapatao 64,737 walikwishatoa maoni yao kwa kuzungumza
wakati wananchi 253,486 walitoa maoni kwa njia ya maandishi, na wengine 16,261
walitumia njia ya “posta, tovuti ya Tume, mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi
wa simu za mkononi....” Kwa hiyo, kwa mujibu wa taarifa hizi za Mwenyekiti wa
Tume, kati ya Watanzania takriban milioni 45, ni Watanzania 334,484 ndio
waliotoa maoni juu ya Katiba Mpya hadi kufikia tarehe 4 Januari, 2013. Idadi
hii ni sawa na asilimia 0.7 ya Watanzania
wote! Na hao ndio waliotoa maoni yao kwa muda wa dakika tano kila mmoja,
wakiwamo waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili tukufu.
Mheshimiwa Spika, ni wazi, kwa takwimu hizi za Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na kwa vyovyote vile, Katiba Mpya itakayotokana na maoni
haya haiwezi kuwa Katiba Mpya ya Watanzania wote. Utaratibu wa hovyo namna hii
utazaa Katiba Mpya ya hovyo!!! Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba
utaratibu huu wa hovyo hauwezi kutupatia Katiba Mpya yenye maridhiano ya
kitaifa kwa ajili ya kutatua migogoro mingi ya kisiasa, kijamii na kidini
ambayo inaikabili nchi yetu kwa sasa.
Mheshimiwa Spika,
Tatu, licha ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
kutangaza kuwa Tume itakuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yake, Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kila dalili za Tume kutokuwa huru au
kuutafsiri uhuru vibaya. Kwa mfano, kuna ushahidi kwamba Tume imekuwa na
mawasiliano ya karibu na Serikali na Ofisi ya Rais kwa namna ambayo inaashiria
Tume kutokuwa huru. Ndio maana katika hotuba yake ya kumaliza mwaka uliopita na
kufungua Mwaka Mpya, Rais Jakaya Kikwete alilitangazia taifa ratiba ya kazi za
Tume ambayo Tume yenyewe ilikuwa haijawahi kuitoa hadharani.
Katika hotuba yake hiyo, Rais Kikwete
alitangaza sio tu kumalizika kwa awamu za kukusanya maoni ya wananchi, bali pia
alitangaza ratiba ya Tume kuanza kuchukua maoni ya vyama vya siasa, taasisi
nyingine na ‘makundi maalum’, tarehe ya kutolewa kwa Rasimu ya Kwanza ya Katiba
Mpya, Mikutano ya Mabaraza ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba na hata tarehe
ya kura ya maoni na upitishwaji wa kura ya maoni kuihalalisha Katiba Mpya.
Mheshimiwa Spika, Rais asingeweza kufahamu ratiba hii yote
bila kupatiwa taarifa ama na Tume yenyewe ama na watendaji au watumishi wake au
na wajumbe wa Tume. Mbali na taarifa ya kwisha kwa awamu ya tatu ya zoezi la
kukusanya maoni ya wananchi, taarifa hizi hazikuwa zimetolewa hadharani na Tume
kabla ya hotuba ya Mwaka Mpya ya Rais Kikwete!
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetambua
siku zote kwamba msemaji rasmi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni Mwenyekiti wa
Tume Joseph Warioba. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haijawahi kusikia wala
kuona mahali popote ambapo Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imempa Rais Kikwete
jukumu la kuwa msemaji wa Tume. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inahoji kama
Rais anaweza kupatiwa taarifa za kina namna hiyo kuhusiana na shughuli za Tume,
kuna uhakika gani kwamba yeye au Serikali yake hawatoi kwa Tume maelekezo ya
kichinichini juu ya nini cha kufanya, kwa namna gani na kwa wakati gani.
Mheshimiwa Spika,
Nne, wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba
ikitoa taarifa za kina juu ya shughuli zake kwa Rais Kikwete na Serikali yake,
Tume hiyo hiyo imetangaza wazi wazi kwamba haiwajibiki kwa Bunge kuhusu
utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria. Zaidi ya kumtuma Naibu
Katibu wa Tume, viongozi wa Tume kama vile Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na
wajumbe wa Tume wamekataa kuhudhuria vikao vya Kamati ya Bunge ya Katiba,
Sheria na Utawala ili kuieleza Kamati juu ya utekelezaji wa majukumu yake kwa
mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi.
Katika hili, Tume imeungwa mkono na
Serikali hiyo hiyo inayoelekea kupata taarifa za kina juu ya utekelezaji wa
kazi zake! Hii ni licha ya kupatiwa jumla ya shilingi bilioni 33.944 za walipa
kodi wa Tanzania zilizoidhinishwa na Bunge katika mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya
kutekeleza majukumu yake. Kwa hiyo, wakati Tume inaharibu mchakato wa Katiba
Mpya kama tulivyoonyesha hapa, Bunge – kwa kupitia kwa Kamati yake –
limezuiliwa kuhoji shughuli za Tume kwa hoja kwamba Tume iko huru.
Mheshimiwa Spika, hii inaweza kuwa mara ya kwanza kwa chombo
cha umma kinachotumia mabilioni ya fedha za umma kilichopewa majukumu ya umma
na Sheria iliyotungwa na Bunge hili tukufu kukataa kuwa chini ya usimamizi wa
kikatiba wa Bunge (parliamentary oversight)!
Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
imesikitishwa sana na kushindwa kwa Kamati husika ya Bunge kudai madaraka yake
ya usimamizi yasipuuzwe na Tume na/au Serikali. Udhaifu huu wa Bunge na Kamati
unaweza kuligharimu Taifa endapo mchakato wa Katiba Mpya utachakachuliwa na
kuliingiza Taifa katika machafuko ya kisiasa, kidini au kijamii.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka
Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu juu ya uwajibikaji wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kwa matumizi ya mabilioni ya fedha za umma
iliyoyaidhinishiwa mwaka jana na inayoyaomba mwaka huu wa fedha.
Mheshimiwa Spika,
Tano, Tume imetengeneza utaratibu wa
mabaraza ya kikatiba ambao kwa ushahidi wa mwanzo tu unaonyesha kwamba hayo ni
mabaraza ya CCM na sio mabaraza ya katiba ya Watanzania wote. Hili limefanyika
kwa kupitia Mwongozo Kuhusu Muundo,
Utaratibu wa Kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya (Mamlaka za
Serikali za Mitaa) na Uendeshaji Wake, uliotolewa na Tume mwezi Februari
mwaka huu. Kwa mujibu wa Muundo huu, wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya
watachaguliwa na Kamati za Maendeleo za Kata (maarufu kama ‘WDC’) baada ya kuwa
wamechaguliwa moja kwa moja na wananchi katika vijiji na mitaa. Wajumbe wa WDC
ni Madiwani wa Kata ambao ni Wenyeviti wake, Watendaji wa Kata ambao ni
Makatibu na Wenyeviti wa Vijiji au Mitaa.
Mheshimiwa Spika, kwa kufuatana na chaguzi za vijiji na mitaa
za mwaka 2009, zaidi ya asilimia 90 ya vijiji na mitaa inaongozwa na wenyeviti
ambao ni wanaCCM. Aidha, kutokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, zaidi ya
asilimia 80 ya Kata zote nchini zinaongozwa na madiwani wa CCM. Hawa ndio
waliochagua wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba tangu mwanzoni mwa wiki
iliyopita. Matokeo yake, kwa taarifa ilizo nazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
kutoka sehemu mbali mbali za nchi yetu, kila mahali wagombea ambao hawakuwa
wanaCCM walienguliwa katika ngazi ya uchaguzi wa vijiji au mitaa au
wameenguliwa na WDC baada ya kushinda katika ngazi hizo.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina
ushahidi kwamba viongozi wa kiserikali kama vile Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa
waliwahamasisha wenyeviti wa vijiji, mitaa na madiwani kuhakikisha kwamba
wagombea wote wasiokuwa wa CCM, hasa wa CHADEMA, wanaenguliwa katika chaguzi za
vijiji, mitaa au kata. Mfano mzuri ni wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Jackson Msome
aliyeitisha mkutano wa wenyeviti wote wa mitaa ya Musoma Mjini na kuwapa
maelekezo ya kuhakikisha kwamba watu
wasiokuwa wanachama wa CCM hawapati nafasi katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya
au Manispaa hiyo.
Mheshimiwa Spika, licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
kupatiwa maoni ya wadau kwamba utaratibu huo utaharibu mchakato wa Katiba Mpya,
Tume ilikataa kata kata kuubadilisha Muundo wa Mabaraza haya. Ni wazi kwamba
Tume inafahamu inachokifanya.
Ni wazi vile vile kwamba Tume inafahamu
matokeo ya hicho inachokifanya, yaani kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya
ambayo ni ya wanaCCM. Na wala haihitaji shahada ya uzamivu kufahamu kwamba
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yenye kutawaliwa kwa kiasi hicho na wanaCCM
yatatoa maoni ya aina gani juu ya Rasimu ya Katiba Mpya yatakayoijadili.
Itakuwa ni Katiba Mpya kwa jina tu, mambo mengine ya msingi yatabaki vile vile.
Kwa maneno mengine, itakuwa ni Katiba ile ile, ya watu wale wale, wa chama kile
kile.
Mheshimiwa Spika, Uchakachuaji wa mchakato wa Katiba Mpya wa
aina hii ndio ulioiingiza Zimbabwe katika machafuko makubwa ya kisiasa toka
mwaka 1998 na Kenya mwaka 2007/2008. Kwa utaratibu huu wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, inaelekea Serikali ya CCM inaelekea kutotaka kujifunza kutokana na
yaliyowakuta jirani zetu wa Kenya na marafiki zetu wa Zimbabwe.
Mheshimiwa Spika,
Sita, Serikali imekataa ama imeshindwa
kuheshimu makubaliano iliyofikia na wadau mbali mbali ikiwemo CHADEMA, kufanya
marekebisho zaidi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa sababu hiyo, bado
haijulikani wajumbe mia moja na sitini na sita watakaotokana na taasisi mbali
mbali zilizotajwa na Sheria hiyo watateuliwa kwa utaratibu gani na nani
atakayefanya uteuzi huo.
Vile vile, bado hakuna muafaka juu ya
uhalali wa idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar
kushiriki katika mjadala wa Katiba Mpya kwenye masuala yasiyokuwa ya Muungano
ya Tanzania Bara wakati hakuna mjumbe hata mmoja wa Tanzania Bara anayeweza
kushiriki katika mijadala ya kikatiba inayohusu masuala ya Zanzibar yasiyokuwa
Mambo ya Muungano.
Zaidi ya hayo, bado hakuna majibu
yanayotosheleza yanayompa Rais mamlaka ya kuliitisha upya Bunge Maalum la
Katiba na kulielekeza ‘kuboresha’ masharti ya Katiba Mpya mara baada ya Bunge
hilo kuipitisha. Aidha, haijulikani ni uhalali upi wa kisheria na kikatiba
utakaoiruhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia na kuendesha kura ya maoni ya
kuhalalisha Katiba Mpya kwa sababu Katiba na Sheria za Uchaguzi za sasa
hazitambui wala kuweka utaratibu wa kuendesha kura ya maoni.
Mheshimiwa Spika, kushindwa kwa Serikali kuleta Muswada wa
Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kufanya marekebisho katika
maeneo tajwa ni ushahidi wa wazi kwamba Serikali ya CCM haina nia ya dhati na
dhamira safi ya kuhakikisha Tanzania inapata Katiba Mpya inayoistahili.
Aidha, si nia ya CHADEMA kuendelea
kushiriki na kubariki mchakato huu kama ulivyo sasa kwani ishara zote ziko wazi
kuwa Katiba inayokusudiwa ni ile tu itakayokidhi matakwa ya Wana- CCM na
Washirika wake na hivyo kutokutimiza azma ya kuwa na Katiba itakayoponya
majeraha mbalimbali na kurejesha uzalendo, mshikamano na upendo wa dhati
miongoni mwa Watanzania na kisha mfumo wa Utawala utakaokidhi mahitaji ya
wakati.
Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inatangaza rasmi kwamba: CHADEMA itajitoa ushiriki wake katika mchakato wa Katiba Mpya endapo
mambo yafuatayo hayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu, yaani
tarehe 30 Aprili, 2013:
1. Kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa
mabaraza ya wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata, na
badala yake wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya wachaguliwe moja kwa moja
na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na WDC;
2. Serikali ilete mbele ya Bunge hili tukufu Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yatayofanyia maeneo
yafuatayo marekebisho:
(a)
Vifungu
vyote vinavyohusu uwakilishi katika Bunge Maalum la Katiba wa taasisi
zilizoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba;
(b)
Vifungu
vyote vinavyohusu ushirikishi wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka
Zanzibar katika mijadala inayohusu mambo yasiyokuwa ya muungano ya Tanzania
Bara;
(c)
Vifungu
vyote vinavyohusu mamlaka ya Rais kuitisha tena Bunge Maalum la Katiba baada ya
Bunge hilo kuwa limeshapitisha Rasimu ya Katiba Mpya kwa lengo la kufanya
marekebisho katika Rasimu kabla haijapelekwa kwenye kura ya maoni;
(d)
Vifungu
vyote vinavyohusu mamlaka ya kikatiba nay a kisheria yatakayoiwezesha Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kuendesha na kusimamia kura ya maoni;
3.
ANGUKO LA ELIMU TANZANIA: ANGAMIZO LA
KIZAZI NA JANGA LA TAIFA.
Mheshimiwa Spika,
Nianze kuzungumzia umuhimu wa elimu kwa
kumnukuu Rais wa 55 wa Marekani, John F.Kennedy (1917 – 1963);
“Our
progress as a nation can be no swifter than our progress in education. The
human mind is our fundamental resource”
Mheshimiwa Spika,
Siku za karibuni kumekuwepo mjadala mzito
sana kuhusiana na hali ya elimu nchini. Pamekuwepo na malalamiko mengi sana
yakiwemo yaliyomtaka Waziri wa Elimu Mhe. Shukuru Kawambwa na Naibu wake Mhe
Phillip Mulugo wajiuzulu kama ishara ya uwajibikaji wa kisiasa. Ni dhahiri kuwa
elimu yetu kama Taifa imeporomoka kwa kiasi kikubwa cha sasa kuhatarisha
mustakabali wetu kama Taifa.
Mheshimiwa Spika, ni mwaka mmoja tu umepita tangu Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA itoe angalizo kali kwa Serikali juu
ya kasi kubwa ya kuporokoka kwa Elimu ya Tanzania na hivyo kuitaka
Serikali kuchukua hatua madhubuti ili kuliepusha Taifa na balaa hilo. Hata hivyo, Serikali hii ya CCM imeendelea
kupuuza ushauri mzuri inayopewa bure na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na
matokeo yake ni kwamba anguko la mwaka huu ni kubwa kuliko maanguko yote
yaliyowahi kutokea katika Historia ya Tanzania ambapo asilimia 60.6 (240,903) ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha
nne wamepata daraja sifuri na wengine asilimia 26.02 (103,327) daraja la nne.
Jumla ya kufeli huku ni zaidi ya asilimia 86.62 au sawa na
Mheshimiwa Spika, kufuatia kufeli huku kwa kutisha kwa
wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2012, wadau wengi walitaka baadhi ya viongozi
wa sekta ya elimu akiwemo waziri kuwajibika. Ni bahati mbaya sana kuwa Waziri
Mkuu ni mmoja wapo wa viongozi Wakuu aliyestahili kuchukua hatua za
kuwawajibisha wahusika lakini hakufanya hivyo. Badala yake, akakimbilia kuunda
tume ya uchunguzi, ilhali yeye mwenyewe Waziri Mkuu, Waziri wake wa elimu na
serikali yake yote ikijua fika nini kinasababisha kuporomoka kwa elimu yetu.
Yumkini, kama kweli serikali hadi leo haijui sababu ya kuporomoka kwa elimu yetu,
basi haina tena sifa wala weledi wa kusimamia siyo tu elimu, bali maisha ya
kila siku ya Watanzania.
Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa kufeli huku hakuwezi
kuchukuliwa kama bahati mbaya hasa ikiwekwa maanani kuwa mserereko wa watoto
wetu kufeli umeshika kasi chini ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne hasa
kuanzia mwaka 2007.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2007, ufaulu wa vijana wetu wa
kidato cha nne ilikuwa (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na 2010 (50.4%).
Kufuatia mserereko huu wa kufeli, serikali iliunda timu iliyoshirikisha
wataalam kadhaa kubaini chanzo chake na tiba ya muda mfupi, muda wa kati na
muda mrefu. Timu hii iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Bw. Francis M. Liboy wa
TAMISEMI ilikamilisha ripoti yake mwaka
2011 na kutoa mapendekezo kadhaa kwa serikali. Waziri wa Elimu Mhe. Shukuru
Kawambwa anaijua ripoti hii kwani ndiye aliyeandika dibaji yake. (Angalia kiambatanisho A)
Mheshimiwa Spika, mbali na ushauri wetu wa mara kwa mara,
serikali hii imebeza kwa nguvu zote juhudi mbalimbali zinazofanywa na wadau
wengine wenye kuumizwa na kusikitishwa na kuporomoka huku kwa elimu. Watanzania
ni mashahidi namna katika Mkutano wa Kumi wa Bunge, hoja binafsi ya Mheshimiwa
James Mbatia (Mb) kuhusu udhaifu ulioko katika sekta ya elimu ilivyochukuliwa
kimzaha na kutolewa majibu mepesi na Serikali kinyume na kanuni za bunge na
hatimaye kuyazima maazimio ya bunge ya kuinusuru elimu ya Tanzania yaliyokuwa yamependekezwa katika hoja
hiyo. Ni katika mkutano huohuo wa Bunge
ambapo hoja binafsi ya Mheshimiwa Joshua Nassari (Mb) kuhusu Baraza la Mitihani
linavyoathiri elimu ya Tanzania iliondolewa katika orodha ya shughuli za
mkutano wa kumi wa Bunge bila ridhaa ya mtoa hoja kinyume na kanuni ya 58(5).
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali ya CCM chini ya
mwavuli wa wingi wa wabunge wake bungeni, cha
kuzivuruga hoja hizi na hivyo kusababisha maazimio ya bunge juu ya hoja
hizi kutotekelezwa ni udhaifu mkubwa sana kwa chama kinacho tawala cha CCM na
Serikali yake na ni ushahidi uliokamilika kwamba Elimu kwao sio kipaumbele cha
taifa.
Mheshimiwa Spika, Serikali ambayo Elimu sio kipaumbele chake,
haiwafai Watanzania kwa karne hii. Kuendelea kuukumbatia utawala na aina hii ni
kukaribisha maafa yasiyoepukika kwa Taifa. Mbali na kulisababishia Taifa hili
aibu kubwa mbele ya majirani zetu na jamii ya kimataifa kwa vijana walio wengi
wa Kitanzania kuonekana kuwa na elimu ya mashaka na isiyoweza kuhimili
ushindani wa soko la ajira, ubovu wetu wa elimu umedumaza uwezo wetu wa ndani
wa kusimamia rasilimali za Taifa, Aidha
kambi Rasmi ya Upinzani inawapa angalizo wananchi wote wa Tanzania kwamba haya
yote yanatokea kwa kuwa Serikali ya CCM haijaiweka Elimu kuwa kipaumbele cha
taifa na kwamba umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa
utawala kwa kuchagua chama chenye nia ya dhati ya kuleta mabadilko
kitakachounda Serikali inayojali elimu ya watoto wao na bila shaka chama hicho
hakiwezi kuwa CCM tena.
Mheshimiwa Spika, Taifa kupitia hotuba hii linataka kujua
Serikali ina nini cha kusema kuhusiana na utafiti huu iliofanya mwaka 2011,
imetekeleza mangapi kati ya mapendekezo 27 yaliyotolewa. Aidha ni kwa nini
imeunda tume nyingine kwa kutumia fedha za walipa kodi wa nchi hii ingali
ripoti nyingine inayohusu somo hilo hilo ikiwa mkononi.
3.1
UNYANYAPAA WA FIKRA VYUO VIKUU
Mheshimiwa Spika, pamoja na nia njema ya katiba ya nchi yetu kuheshimu haki ya uhuru wa
mawazo kama ilivyowekwa bayana katika Ibara ya 18(a) na Ibara ya 20(1) kwa
kutoa uhuru wa mtu kushirikiana na wengine, kumekuwepo na propaganda mbalimbali
hasa kwenye taasisi za elimu ya juu, zenye kuminya nafasi na uhuru wa vyama vya
upinzani kuendesha shughuli zake kwa usawa, uwazi na kwa haki katika ngazi ya
elimu ya juu kama ambavyo chama tawala kimejiwekea na kujitengenezea mazingira
hayo.
Mheshimiwa Spika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema hivi: "Lakini kutoa uongozi maana yake siyo
kuwanyang'anya watu wenyewe mamlaka yao. Watu lazima wafanye uamuzi wao wenyewe
kuhusu maisha yao ya baadae kwa kufuata njia za demokrasia. Uongozi hauwezi
kuchukua nafasi ya demokrasi; uongozi lazima uwe sehemu ya demokrasi"
Mheshimiwa Spika, tafakuri ya nukuu hii imekuja wakati ambao ushiriki wa wanafunzi wa elimu
ya juu katika siasa unaonekana kulemea upande moja tu wa kukipendelea na kukipa
uwezo chama tawala katika shughuli zake kwenye taasisi hizo. CCM wamefikiri na
kuamua kuanzisha mkoa maalumu kwa sasa wakitambua kuwa vyuo (hasa vyuo vikuu)
haviruhusiwi kuendesha shughuli za siasa vyuoni, kama ilivyo majeshi, makanisa
au misikiti na ili kuthibitisha hilo wameelekeza pia shughuli za mkoa maalumu
ulioanzishwa zifanyike nje ya chuo. Lakini tujiulize na kutafakari zaidi kuhusu
mshindo (impact) wa shughuli za mkoa maalumu wa kisiasa ndani
ya himaya za vyuo vikuu na elimu ya juu nchini.
Mheshimiwa Spika, ni ngumu kuamini
kuwa shughuli za siasa vyuoni, ambazo Tanzania Commission of University Act
imeweka bayana kuwa ni kosa, zitaweza kudhibitiwa ikiwa vyama vingine
vinajiwekea uhalali na mazingira ya kuingiza wanavyuo kwenye siasa, jambo
ambalo udhibiti wake ni mgumu kwa mamlaka husika hasa vyuoni kwa kuwa wanavyuo
hufanya vikao vya siasa kwa siri, na kwa nyakati ambazo uongozi wa vyuo hauna
taarifa.
Mheshimiwa Spika, kwa uangalifu
mkubwa, ningependa kutoa angalizo kuwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
haitokubali unyanyapaa wa fikra wa aina yoyote utakaoendana na kujenga matabaka
kutokana na utofauti wa mitazamo baina ya jamii ya wasomi kwa kuwa, kutoka
taasisi mbalimbali za elimu ya juu , chimbuko la viongozi mahiri wa nchi hii
pamoja na nchi nyingine mbalimbali duniani limechipukia. Kambi Rasmi ya
Upinzani, itaendelea na juhudi zake za kuhakikisha kuwa taifa kwa kupitia
wanafunzi wa elimu ya juu, wanapata fursa mbalimbali za kuikomboa jamii ya
kitanzania ambayo inadumazwa kwa unyanyapaa wa fikra.
Mheshimiwa Spika, njia pekee ya
kufuta unyanyapaa wa fikra kwa vijana waliopo kwenye elimu ya juu ni kwa
Serikali kurejesha rasmi na kuruhusu uwepo wa siasa katika elimu ya juu na vyuo
vikuu vyote nchini kama shughuli ambazo ni nje ya masomo ili kusaidia kujenga
uwanja wa demokrasia katika serikali za vyuo na vile vile itasaidia katika
kuweka mazingira ambapo wasomi wetu wanaanza kujifunza mbinu na utendaji wa
kisiasa katika mazingira ya elimu ili waweze kujifunza kuishi pamoja, kupingana
kwa hoja na kujua jinsi ya kuvumiliana katika mazingira ya tofauti mbalimbali
za kiitikadi, imani, na mtazamo kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya
CHADEMA ya mwaka 2010. Hapa nikisisitiza maneno ya baba wa Taifa, Mwalimu
Nyerere juu ya kuboresha maisha ya Watanzania:
"Tukiwasaidia watu wa Tanzania kuendelea, ndiyo
tunaiendeleza Tanzania. Maana Tanzania Ni ya Watanzania Na Watanzania Ni wote,
Hakuna mtu mwenye haki ya kusema "Mimi ndiyo watu". Wala hakuna Mtanzania mwenye haki ya kusema "
Najua linalowafaa watanzania na wengine
lazima wafuate".
3.2 BODI YA
MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Mheshimiwa Spika,lengo la kuanzishwa kwa bodi ya mikopo ya
wanafunzi wa elimu wa juu ni katika kusaidiakupunguza maumivu ya wazazi na
walezi wa kitanzania katika kuhakikishsa vijana wetu wanapata elimu ya juu kwa
kusaidiana na taasisi hii ya Serikali (HELSB), kwa kugawa mikopo kwa waombaji
wenye vigezo sahihi na kuwapa mikopo kwa viwango vya madaraja ,balimbali ya
uhitaji.
Mheshimiwa
Spika, Vigezo
ambavyo vimekua vikitumika katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu,
vimekua vikilalamikiwa. Baadhi ya wanufaika wa mikopo hii, wamejikuta wakipewa
asilimia chache huku wakiwa wametoka katika familia za kifukara ambazo hazina
uwezo wa kuendesha maisha yao. Familia nyingi hazina uwezo hata wa kuhimili mlo
mmoja kwa siku, je mzigo wa kuwasomesha watoto na vijana wao ngazi ya elimu ya
juu nani ataubeba? Kutokana na udhaifu huu, vijana wameanza kujigawa katika
matabaka ya 'wao'(matajiri na wenye nazo) na 'sisi'(masikini, wasionacho) na
wamefikia mahali wananukuu maandiko ya dini kuwa "mwenye nacho huongezewa,
asiye nacho hupokonywa hata kile kidogo walicho nacho".
Mheshimiwa
Spika, Malalamiko
juu ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu yameendelea kuwa mengi, huku waombaji
wakilalamikia mlolongo wa taratibu zilizowekwa ili muombaji aweze kufanikisha
usajili wake katika bodi. Malalamiko haya yameendana sambamba na utaratibu
mbovu wa utunzaji wa kumbukumbu za watu katika mfumo mzima wa elimu Tanzania
ambao unajenga urasimu mgumu katika kupata taarifa za mwombaji na hivyo
waombaji kulazimika kujaza taarifa upya kila mwaka mpya wa masomo unapoanza.
Mheshimiwa
Spika, Bodi ya
mikopo iliingia gharama ya kununua mfumo utakaotumika katika kuchambua viwango
vya ukopeshaji kwa wanafunzi , kutoka kwa kampuni ya nchini Afrika Kusini ya
ADBSC kwa gharama za dola za kimarekani shilingi 188,000 na marekebisho ya
mtambo huu yaliigharimu bodi kiasi cha dola za kimarekani 42,000. Mfumo huu
ulitarajiwa kupunguza malalamiko ya waombaji na badala yake malalamiko
yanaongezeka kila kukicha.
Mheshimiwa
Spika, Ongezeko
la malalamiko mbalimbali juu ya ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi waliopo
vyuoni hali ambayo imekua ikisababisha migomo ya mara kwa mara katika taasisi
hizo nalo limekua tatizo lisiloisha. Na tumeshuhudia migomo hiyo ikiambatana na
kusimamishwa ama kufukuzwa kwa wanavyuo, hali ambayo inajenga kizazi chenye
hofu hasa inapokuja katika kutetea haki zao za msingi.
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu
wa kifungu cha 19 (1) cha sheria No. 9 iliyoanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu, ni wajibu wa kila mtu aliyenufaika na mikopo ya elimu ya juu
kurejesha mkopo serikalini kupitia Bodi ya mikopo. Pamoja na changamoto ya
urejeshwaji wa mikopo kwa walionufaika, bodi haijafanya kazi ya kutosha katika
kufuatilia na kujua kuhusu wanufaika wa mikopo hiyo (tracking system).
Mheshimiwa
Spika,ni dhahiri
kuwa bodi ya mikopo haijaweka utaratibu na mfumo sahihi wa kuwafuatilia wadeni
wake, na hivyo kuna asilimia kubwa ya wanufaika wa mikopo hiyo ambao wako
makazini na wana ajira, lakini mpaka leo hawajawahi kukatwa marejesho ya mikopo
wala kufuatiliwa na bodi kwa ajili ya taratibu za kuwaingiza katika mfumo wa
marejesho.
Mheshimiwa
Spika, ni wazi
kuwa kumekuwa na ubabaishaji mkubwa si katika marejesho tu, hata katika utoaji
wa mikopo kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu. Pamoja na ushauri ambao
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ulitoa kwa Serikali katika uwasilishaji wa
hotuba ya mwaka 2012/2013 kuanzisha na kutumia mfumo wa urejeshaji mikopo kwa
kutumia technolojia ya kibenki kupitia mitandao ya simu kama M-PESA,TIGO PESA,
Airtel Money, Z-Pesa, n.k, Serikali na bodi ya mikopo inaonekana kutofuata
ushauri huu na hivyo kuendelea kuwanyima fursa wahitaji wa mikopo.
Mheshimiwa
Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani bungeni inaitaka wizara husika pamoja na bodi ya mikopo kutoa
maelezo juu ya utekelezaji wa mapendekezo haya, kama wamefanya tathmini juu ya
uanzishwaji wa mfumo huu, faida na hasara zake na kama la! hawajafanya
tathmini, wizara husika itoe kauli katika mkutano huu wa bunge, juu ya njia
mbadala na mfumo utakaohakikisha wanufaika wanapata uraisi katika urejeshaji wa
makato ya mikopo yao.
Mheshimiwa
Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani, inaendelea kusisitiza juu ya utekelezaji wa mapendekezo
yake, yaliyopo katika ilani ya CHADEMA ya kuivunja Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Juu kutokana na uendeshaji mbovu, mfumo wake mbovu wa kisheria, na uongozi
ambao umeshindwa kufanya elimu ya juu ipatikane kwa kila kijana na ambayo
kutokana na uongozi usiofaa imeshindwa kukusanya madeni toka kwa wakopaji.
3.2 HATIMA YA WATOTO WANAOSHINDWA KUENDELEA NA
MASOMO YA SEKONDARI BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa
tafiti mbalimbali, watoto na vijana wa Kitanzania walio chini ya umri wa miaka
18 ambao wamefeli darasa la saba na au kidato cha nne, kwa sasa ni wastani wa
watoto 800,000 kwa sasa. Kwa wengi wa watoto hawa ambao wengi hutoka familia
masikini, hawana uwezo wa kujiendeleza na hawana sifa za kuajiriwa ikiwa ni
pamoja na umri mdogo. Kundi hili ni kubwa na linakuwa kwa kasi.
Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha
miaka 51 ya Uhuru, Serikali haijatengeneza sera yoyote au sheria ya kusaidia
kundi hili kubwa ili liweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi
ili waweze kujikimu wao wenyewe na kuchangia katika pato la taifa. Kundi hili
lililo hazina kubwa ya nguvukazi ya Taifa letu siku za usoni limeachwa solemba
huku likipewa majina ya kebehi ya kila aina ikiwemo wazururaji, vibaka,
machinga nk.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali kueleza mbele ya Bunge hili, kwamba inampango gani
wa kupunguza idadi hii ya watoto wanaobaki mitaani bila shughuli rasmi ya
kufanya? Pili kwa wale ambao imeshindikana kabisa kuendelea na masomo, kuna
mpango gani wa kisera wa kuweza kuwasaidia ili waweze kushiriki katika shughuli
rasmi za kiuchumi ili kulinusuru taifa kuondokana na umasikini uliokithiri?
4. DEMOKRASIA, UTAWALA
BORA NA HAKI ZA BINADAMU
4.1.
DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA CHAGUZI
ZA KIDEMOKRASIA NCHINI.
Mheshimiwa Spika, chaguzi huru na za haki ni kipimo muhimu
cha demokrasia ya kweli. Kwa kutambua umuhimu huu katika chaguzi na hatimaye
katika kuongoza nchi, ibara ya 5(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inatoa haki ya kupiga kura kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri
wa miaka kumi na minane.
Mheshimiwa Spika, ili kuweka utaratibu mzuri wa kila raia wa
Tanzania mwenye sifa ya kupiga kura aweze kupiga kura, ibara ya 5(3) (a) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fursa kwa Bunge kutunga sheria
ya Uchaguzi ambayo pamoja na mambo mengine, itaanzisha Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura na kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika daftari hili.
Mheshimiwa Spika, Ni vyema kwamba Daftari la Kudumu la Wapiga
kura lipo, lakini ni bahati mbaya sana pia kwamba utaratibu wa kurekebisha au
kuboresha yaliyomo katika daftari hilo hauendi sawia na haki ya raia kupiga
kura na mahitaji makubwa ya kukuza
demokrasia katika chaguzi hapa nchini.
Mheshimiwa Spika, mara kadhaa nimemuuliza Waziri Mkuu mbele
ya Bunge hili juu ya mkakati wa Serikali kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura. Wakati wote majibu yamekuwa ni mepesi na yasiyokidhi hitaji hili muhimu
la Kikatiba. (Tazama Taarifa Rasmi za Bunge (Hansard) za tarehe 19 Aprili, 2012
na 8 Novemba, 2012).
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu akijibu swali
langu la papo kwa papo juu ya Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,
katika Mkutano wa Tisa wa Bunge, tarehe 8 Novemba, 2012, alisema kwamba mfumo
uliopo wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni mzuri. Jambo hili linaibua
mashaka makubwa juu ya utayari wa Serikali kulinda haki ya mwananchi ya kupiga
kura kama ilivyotolewa na Katiba ya Nchi, kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi
kutokana na wanachi kukosa haki ya kupiga kura kutokana na Daftari hilo
kutofanyiwa marekebisho. Aidha mtazamo huo wa Waziri Mkuu, hautoi fursa ya
kulifanyia maboresho Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa wakati; na kwa maana
hiyo haki ya kupiga kura na demokrasia ya uchaguzi katika Taifa hili vipo
katika hatari ya kupotezwa au kupatikana kwa hisani ya watawala na siyo haki ya
kikatiba.
Mheshimiwa Spika, kwa
kuwa tangu uchaguzi mkuu wa 2010, kumefanyika chaguzi ndogo mbili za Ubunge
katika Majimbo ya Igunga Tabora na Arumeru Mashariki mkoani Arusha. Aidha, kata
kadhaa zimerudia chaguzi nchini kwa sababu mbalimbali. Katika chaguzi hizi,
daftari la Kudumu la Wapigakura halikufanyiwa marekebisho na hivyo kuwanyima
wananchi wengi waliokuwa na sifa ya kuandikishwa na kupiga kura haki ya
kushiriki katika chaguzi hizo.
Mheshimiwa Spika, Ni kilio cha muda
mrefu ndani ya nchi hii kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), haiko huru na
inafanyakazi zake kwa shinikizo la viongozi waliopo madarakani. Kilio hiki
kimethibitishwa na Tume yenyewe pale walipokutana na Tume ya marekebisho ya
Katiba wakati walipotoa maoni yao.
Mheshimiwa Spika, kuna mchakato wa
maandalizi ya siri unaoendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wa kuandaa
utambuzi wa wapiga kura kwa kutumia mfumo wa “biometric” kwa maana ya kumtambua
mpiga kura kwa alama za mwili kama alama za vidole na au mboni ya jicho kama
sehemu ya maandalizi ya Uchagizi Mkuu ujao wa 2015. Kwa mujibu wa taarifa
tulizo nazo, tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshaanza maandalizi mengi ya
msingi bila hata vyama vya siasa kujua
Aidha, mchakato
huu unaofanywa kwa siri kubwa na unaokisiwa kutumia zaidi ya dola za kimarekani
million 200 tayari umeanza kutafutiwa fedha.
Mheshimiwa Spika,
teknologia hii kwa siku za karibuni imetumika katika chaguzi nchini Ghana na
Kenya. Kote huko, ilifeli na chupuchupu ingeyaingiza mataifa hayo katika vurugu
kubwa za uchaguzi. Mataifa haya yalilazimika kurudia mfumo wa upigaji na
uhesabuji kura “manually” hali iliyosababisha hofu kubwa.
Mheshimiwa Spika, Si kwamba Kambi
Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA haiafiki matumizi ya teknologia mpya
kurahisisha na kuboresha mfumo mzima wa uchaguzi katika nchi yetu, bali
inatambua athari kubwa zinazowezekana siku za usoni kama zoezi hili lililo
“sensitive” halitafanywa katika misingi ya uwazi na ushirikishwaji wadau muhimu
kama vyama vya siasa katika hatua zote la tangu awali kabisa. Ni kwa sababu
hizi basi, tunaitaka Serikali kutoa maelezo ya kina kuwa ni sheria gani
iliyotungwa na bunge inayoruhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
kwa mfumo huu na ni bajeti ipi inatumika
kutekeleza mpango huo? Na ni kwa nini mpango huo unafanyiaka kwa siri?
Mheshimiwa Spika, kwa
kuwa Serikali haioneshi dhamira ya dhati ya kusukuma mchakato wa kuleta
marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi ili kuondoa ukomo wa kuboresha Daftari la
Kudumu la Wapigakura (wa mara mbili kwa
kipindi cha miaka mitano) na badala yake daftari hilo liwe huru wakati wote
kuandikisha wapigakura wapya wanaotimiza masharti ya kupigakura na
kuingiza marekebisho ya taarifa za wapigakura wengine, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa kusikiliza na kuzingatia
sauti na utashi wa watu na uzingativu wa kutosha wa dalili za nyakati na
mazingira ya nchi pamoja na kuheshimu maono na falsafa za waasisi wa taifa
letu, inakusudia
kuleta Hoja Binafsi kuhusu marekebisho
ya sheria zote za uchaguzi nchini ili kuinusuru haki ya kikatiba ya raia wa
Tanzania kushiriki kikamilifu katika chaguzi tena zilizo huru na za haki.
4.2 MFUMO WA KUKABIDHIANA MADARAKA KATIKA OFISI ZA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI.
Mheshimiwa Spika,
Pamoja na Taifa kuwa katika mchakato wa
kuandika upya Katiba ya nchi yetu, hakuna “guarantee” kuwa katika hiyo itakuwa
tayari kwa ukamilifu wake kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. Hivyo basi ni bora
hatua zote za urekebishaji wa viashiria vya mvurugano kuendelea kushughulikiwa
sambamba na mchakato wa Katiba Mpya.
Mheshimiwa Spika, Ni jambo la kiungwana kwa viongozi wanaoondoka
madarakani kukabidhi madaraka na ofisi kwa wale watakaoingia madarakani na
katika ofisi hizo.
Mheshimiwa Spika, pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kutoa muda wa siku saba,
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 42(1) kuwa “Rais Mteule
atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba
amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya
kupita siku saba”. Lakini utaratibu huo haujatungiwa sheria na ni
utaratibu ambao ulikuwepo tangu enzi za chama kimoja na kwa misingi hiyo
haukidhi mahitaji ya kipindi hiki cha vyama vingi endapo itatokea kwamba
mgombea urais kutoka chama cha upinzani atashinda uchaguzi na kuapishwa kushika
madaraka ya Urais.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa nchi mbalimbali duniani
zimeanzisha sheria ya kipindi maalumu cha mpito cha kukabidhiana madaraka ya
Urais baada ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge,
Na kwa kuwa sheria kama hii huelekeza mtu
atakayesimamia rasilimali za nchi ili kudhibiti ubadhirifu mkubwa ambao
hufanyika katika kipindi hiki cha mpito;
Na kwa kuwa nchi yetu imeridhia kipindi cha
uongozi wa u-rais wenye ukomo wa miaka kumi;
Na kwa kuwa mfumo wetu wa Siasa ya vyama
vingi sasa umekomaa na hivyo kutoa nafasi ya uwezekano wa chama cha upinzani
kutwaa madaraka ya Dola;
Hivyo basi ni jambo la busara sana kutunga
sheria ya Kipindi cha mpito chenye kutoa muda wa kutosha na utaratibu
utakaotumika kuruhusu kukabidhiana madaraka ya urais na serikali (Presidential
Transition Act) kutoka utawala mmoja kwenda mwingine ili kuepusha migongano au
hofu ya kutojua kitakachotokea.
Mheshimiwa Spika, ni azma ya Kambi Rasmi ya Upinzani, CHADEMA
kuleta hoja binafsi Bungeni ili Bunge liazimie kutungwa kwa sheria hii
muhimu sana kwa Taifa letu siku za usoni.
4.3
UCHOCHEZI WA KISIASA: UDINI, UKABILA NA
“UGAIDI”
Mheshimiwa Spika, nchi yetu kwa miaka mingi imesifika sana
duniani kutokana na tunu yake ya “Amani na Utulivu.” Hata hivyo, tunu hii ya
amani na utulivu iko mashakani baada ya kuibuka kwa matukio kadhaa ya uvunjifu
wa amani yenye sura ya udini.
Mheshimiwa Spika, matukio hayo ni pamoja na mgogoro kati ya
waislamu na wakristo huko Geita, Tunduma na kwingineko juu ya uhalali wa
kuchinja ambapo watu kadhaa walijeruhiwa na wengine kuuwawa. Matukio mengine ni
kushambuliwa kwa viongozi wa dini akiwemo Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh
Fadhil Soraga ambaye alimwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana, Padre Ambrose
Mkenda ambaye alinusurika kifo baada ya
kupigwa risasa na kuvunjwa taya na Padre Evaristi Mushi ambaye aliuwawa
kwa kupigwa risasi tarehe 17Februari, 2013.
Mheshimiwa Spika, matukio haya ya kihalifu yenye sura ya
kidini yalijumuisha pia kuchomwa moto nyumba za ibada hususan makanisa huko
Zanzibar na Dar es Salaam na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali. Aidha
matukio haya yalizua hofu kubwa miongoni mwa wananchi kwa kuwa hawakuwa na
uhakika wa usalama wao.
Mheshimiwa Spika, mengi yamesemwa, mengi yameandikwa, mengi
yamehubiriwa kwenye nyumba za ibada na vyombo vya habari. Lakini jambo moja
ambalo halijasemwa wazi na ambalo tumekuwa na kigugumizi kulisemea, ni hili: Kwamba kwa kiasi kikubwa mgogoro huu wa
kidini nchini, hasa mgogoro wa uchinjaji
wa kitoweo, umechochewa na baadhi ya wanasiasa wa kutoka chama tawala.
Mheshimiwa Spika, Madhehebu ya dini yamekuwapo kwa muda
mrefu nchini na katika kipindi chote hicho, hakujawahi kutokea mgogoro wa
uchinjaji wa nyama kwa minajili ya kitoweo. Pamoja na kwamba Kambi Rasmi ya
upinzani Bungeni, haina nia ya kutoa hukumu juu ya matukio haya, lakini ni vema
Watanzania wakaelewa kwamba kwa vyovyote iwavyo, serikali ya CCM haiwezi
kukwepa lawama katika kulikuza tatizo hili;
na kwamba imeshindwa kujua wajibu wake wa msingi wa kuilinda nchi na
raia wake na kuhakikisha jamii yote inaishi kwa upendo na kuvumiliana. Uhalifu
wowote unaotokea dhidi ya nchi na raia ni dalili ya wazi kabisa ya udhaifu wa
Serikali iliyoko madarakani katika kutimiza wajibu wake. Utawala unaotumia dini
kuwagawa wananchi wake na kutafuta ushindi
Mheshimiwa Spika, uchochezi na propaganda za kidini na
kikabila vilichagizwa kasi na CCM mara baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi vya
siasa kama mojawapo ya turufu yake ya kukabiliana na vyama vya upinzani.
Uchochezi huu ulishika kasi katika uchaguzi wa mwaka 2005 na mwaka 2010.
Vikundi kadhaa vya kidini vilifadhiliwa kuhubiri chuki dhidi ya dini nyingine
waziwazi na kwa muda mrefu katika maeneo kadhaa ya nchi. Mihadhara, mahubiri na
hata matamko ya hatari na uchochezi yalitolewa waziwazi hata kupitia vyombo
kadhaa vya habari vya kidini na mitandao ya kijamii. Malalamiko mengi
yalitolewa lakini Serikali ilifumbia macho tatizi hili kwani ilionekana kuwa
mpasuko na hofu iliyo matokeo ya propaganda hizo ulikinufaisha zaidi chama
tawala na baadhi ya viongozi wake.
Mheshimiwa Spika, chuki na hofu hii iliyopaliliwa kisiasa
sasa ndiyo inayoitesa nchi yetu na hakika linastahili kuwa somo kwa wanasiasa
wote walioasisi uhalifu huu dhidi ya mstakabali mwema wa Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, kama vile hili halitoshi, sasa
tunashuhudia kuibuka kwa uchochezi mpya wa kisiasa tena wenye ubia kati ya
chama Tawala na vyombo vya dola na kinachoitwa “Ugaidi”.
Mheshimiwa Spika, vitendo viongozi wa dini kujeruhiwa na
kuuwawa kwa kupigwa risasi, kuchoma moto nyumba za ibada huko Zanzibar na Dar
es Salaam ni Ugaidi kwa mujibu wa tafsiri ya Sheria ya Ugaidi ya Tanzania.
Kambi Rasmi ya Upinzani inashangazwa sana kuona kwamba Serikali haikuyachukulia
matukio haya ya wazi ya kigaidi kama ni ugaidi ila imekuwa hodari sana kuchukua
suala la mtu aliyebambikiwa kesi ya ugaidi kwa ushahidi wa kughushi kuwa yeye
ndiye gaidi. Pili, Kwa mujibu wa Sheria ya ugaidi mtu yeyote anayefanya
mawasiliano na gaidi au magaidi, yeye pia anahamasisha ugaidi na hivyo naye
anastahili kuunganishwa katika tuhuma hizo za mashtaka ya ugaidi.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
inasikitika sana kuona wale wote waliokuwa wakiwasiliana na hao wanaoitwa
magaidi ambao pia ni viongozi wa CCM na washirika wao hawajachukuliwa hatua yoyote. Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inaulaani mkakati huu wenye nia ovu ya kufifisha demokrasia
hapa nchini. Aidha Kambi ya Upinzani inaamini kwamba, kamwe mpango huu haramu hautafanikiwa na naomba kuchukua nafasi hii
kuonya kuwa vyama vya siasa vifanye siasa zake kwa ushindani wa sera na isiwe
kwa mikakati ya kiharamia ya kudhuru, kubambikiza na kisha kutengeneza ushahidi
kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama. Hili nalo likiachiwa likakomaa
litaliingiza Taifa letu katika hatari nyingine ya machafuko.
4.4
UHURU
WA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba uhuru wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) ni kichocheo muhimu sana katika kujenga na
kukuza demokrasia katika Taifa lolote linaloamini katika haki. Hali kadhalika,
uhuru wa kujieleza na kupata habari ni miongoni mwa haki za msingi za raia. Ibara
ya 18 ya Katiba yetu inaweka msisitizo kwamba, kila raia wa Tanzania anao uhuru wa maoni na kueleza fikra zake,
uhuru wa kutafuta na kupokea habari na haki ya kufanya mawasiliano bila
kuingiliwa katika mawasiliano yake.
Mheshimiwa Spika, matukio yaliyotokea mwaka jana peke yake
katika tasnia ya habari ni kinyume cha katiba ya nchi lakini pia yanapingana na
dhana ya Utawala Bora na kaulimbiu ya Serikali ya Uwazi na Uwajibikaji
(Transparency and Accountability).
Mheshimiwa Spika, gazeti la MwanaHALISI limefungiwa kwa muda
usiojulikana na serikali. Muda usiojulikana maana yake, ni hadi mtawala
atakapotaka na au hadi waliolifungia gazeti watakapojisikia kutaka
kulifungulia.
Mheshimiwa Spika, kwa taarifa zilizopo, gazeti hili
limefungiwa bila wamiliki wa kampuni inayochapisha gazeti hilo kupewa haki ya
kusikilizwa. Mbali na kitendo hiki kuwataabisha wafanyakazi kadhaa walioajiriwa
na kampuni inayochapisha gazeti hili, kitendo hiki kimewanyima mamilioni ya
Watanzania haki yao ya kupata habari kwa mujibu wa katiba. Kutokana na hali
hiyo, ninaisihi serikali itafakari upya uamuzi wake wa kulifungia gazeti hili
ili kuondoa kiza na malalamiko kuwa gazeti la MwanaHALISI limefungiwa kwa
sababu ya kulinda uhalifu dhidi ya waliomteka na kumtesa Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Madaktari nchini, Dr. Steven Ulimboka.
Mheshimiwa Spika, katika kadhia hiyo hiyo ya kuminywa kwa
vyombo vya habari na uhuru wa habari, mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa
kwa kupigwa kitu kilichohisiwa kuwa bomu na polisi. Utata mkubwa umezunguka
tukio hili na polisi walewale ambao kwa mtazamo wa jumla ni watuhumiwa,
wameachiwa mamlaka ya kuchunguza na kushtaki kuhusiana na kifo hiki.
Mheshimiwa Spika, kifo hiki kimelitia doa kubwa Taifa letu
na zaidi kutokana na kitendo cha Serikali kuonekana kulinda wahalifu. Sina
hakika kama watu walioshiriki katika kumpiga na kumuua Mwangosi wamekamatwa,
ila nina hakika kuwa kifo chake kimepunguza wigo wa upatikanaji habari.
Ili serikali iweze kujinasua katika lawama, shutuma na tuhuma kwamba
ilihusika katika kupanga njama za mauaji ya Mwangosi, ni vema itumie kupitia
Rais, mamlaka yake ya kisheria kuunda tume huru ya kimahakama itakayochunguza
kifo hiki na vingine kadhaa vyenye utata.
Mheshimiwa Spika, kilio hiki cha kuundwa kwa Judicial
Commission of Enquiry kimekuwa cha muda mrefu na kila mwaka nazungumzia jambo
hili katika hotuba zangu bila hatua zozote kuchukuliwa. Mara kadhaa,
nimezungumza na wewe ndani na nje ya Bunge. Rais Jakaya Kikwete naye
nimemwandikia na hata kuzungumza naye kuhusiana na haki hii ya msingi ya raia.
Pamoja na wote kuahidi kuchukua hatua, hadi sasa hakuna hatua iliyochokuliwa
hali inayoashiria serikali kujua ukweli na pengine kuhusika na hivyo kulindana
katika mauaji.
Mheshimiwa Spika, napenda kwa niaba ya Kambi Rasmi ya
Upinzani kutoa pole kwa Ndg. Absalom Kibanda, Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri
ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania kwa maumivu na mateso
makali aliyoyapata kutoka kwa watu wasiotaka kusikia uhuru wa kujieleza. Na
kama ilivyo kwa matukio mengine kadhaa ya kuongezeka kwa utesaji wa aina hii,
tunaitaka serikali itoe tamko rasmi la ni nani waasisi na watekelezaji wa
mkakati huu wa kuzima uhuru wa wanahabari na vyombo vyao.
4.5 UWAJIBIKAJI WA KISIASA (POLITICAL
ACCOUNTABILITY)
Mheshimiwa Spika, uwajibikaji wa
kisiasa ni moja kati ya misingi ya utawala bora katika uendeshaji wa shughuli
za Serikali. Serikali inayofuata misingi ya utawala bora huwa inawajibika kwa
mema na mabaya yanayotokea chini ya utawala wake. Ni vyema ikaeleweka kuwa
hitaji la kumtaka kiongozi wa kisiasa kuchukua hatua za uwajibikaji wa kisiasa,
pale jambo linalosababishwa na uzembe wa ama yeye binafsi, walio chini ya
mamlaka yake na hata mfumo anaousimamia, siyo jambo la chuki binafsi; bali ni
kielelezo cha uongozi unaojali, unaojutia madhila yaliyosababishwa na ulio
tayari kujirekebisha ili yaliyotokea yasijirudie tene siku za usoni.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya
Tanzania siku zote hujikweza kama Serikali inayofuata misingi ya utawala bora.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba kila mara viongozi wake wanakwepa
kuwajibika kwa mambo mengi ya aibu yanayotokea chini ya utawala wake.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni imekuwa ikipiga kelele ikiwataka mawaziri wa Serikali hii
kuwajibika kwa kujiuzulu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kusimamia vyema
kazi za Serikali lakini hakuna chochote kinachofanyika jambo ambalo
limesababisha maovu kuendelea kufanyika na hivyo kuathiri ustawi wa Taifa.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani ilimtaka waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
kujiuzulu kwa kushindwa kuzuia mauaji holela ya raia wasio na hatia
yaliyofanywa na polisi maeneo kadhaa hapa nchini lakini hakufanya hivyo.
Tulimtaka Waziri wa Elimu na Naibu wake kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia mfumo
wa Elimu hapa nchini jambo ambalo limepelekea kiwango cha wanafunzi wanaopata
alama sifuri katika mitihani kuongezeka
kila mwaka na hivyo kuweka hatarini mustakabali wa maisha ya wanafunzi hao na Taifa kwa jumla lakini bado
wameng’ang’ania madaraka. Tuliitaka Serikali kuwawajibisha Makamanda wa Polisi
wa Mikoa ya Morogoro na Iringa kwa kusimamia mauaji ya raia wasio na hatia
lakini mpaka leo wanafurahia maisha kana kwamba hakuna kilichotokea.
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu ndiye Kiongozi Mkuu wa
shughuli zote za Serikali. Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo daraja kati ya Serikali
Kuu na wananchi. Ni dhahiri kuwa Waziri
Mkuu ndiye mtunza nidhamu na uwajibikaji mkuu katika Taifa hili. Ni nafasi ya
uongozi inayostahili kuwa tayari kupokea lawama katika kufanya maamuzi magumu.
Ni nafasi inayohitaji uwezo wa kufanya maamuzi hayo mazito na kwa wakati kwa
maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, kwa idadi ya makosa ya kizembe yanayotokea
katika nchi hii, na jinsi viongozi kadhaa wa serikali hii wasivyowajibika tena
kwa kubeza na kukejeli malalamiko ya mara kwa mara ya wananchi; kitendo cha Waziri Mkuu kukaa kimya wakati mwingi bila
kutumia rungu lake la madaraka kulitetea au kuliokoa Taifa ni kigezo tosha cha
kutafakari kama upole nauungwana wa Waziri Mkuu leo ni tija au fedheha kwa
Taifa?
Mheshimiwa Spika, napenda nimkumbushe Waziri Mkuu kwamba,
Ofisi yake inategemewa sana kwa mustakabali wa maisha ya Watanzania. Kwa
misingi hiyo, Waziri Mkuu hana budi kuwa mstari wa mbele katika kujibu kero na
matatizo ya wananchi kwa haraka kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa Spika, bado taifa liko katika msiba mzito
uliosababishwa na kuporomoka kwa ghorofa katikati ya Jiji la Dar Es Salaam.
Ofisi ya Waziri Mkuu imekalia kwa muda mrefu bila kuchukua hatua stahiki ripoti
kadhaa zilizotahadharisha kuhusu ujenzi holela wa maghorofa katika nchi yetu.
Mbali na waliopelekwa mahakamani, hakuna waliochukua hatua ya kuwajibika
kisiasa / kiutendaji. Hili ni janga kuu na ishara ya watendaji na viongozi
wengi wa Serikali kutokutambua kuwa nafasi zao za kazi ni dhamana waliyonayo
kwa niaba ya Umma.
Mheshimiwa Spika, si nia yangu
kutangaza mgogoro na Serikali kwa tabia hii ya kutowajibika, lakini napenda
kuiasa Serikali kwamba kwa tabia hii inajitangazia mgogoro yenyewe na
wananchi. Hili si jambo zuri kwani
uvumilivu wa wananchi utakapofikia ukomo, Serikali isishangae kuona nguvu ya
umma ikitumika kuwawajibisha viongozi wanaong’ang’ania madaraka huku wakiwa
hawana sifa na weledi wa kufanya kazi za umma. Aidha, naomba kuwataka wananchi
wasiendelee kutegemea “muujiza wa uwajibikaji” hivyo watafakari wenyewe uwezo
walio nao kuchukua hatua muda muafaka ukifika.
5.0 DENI LA TAIFA
Mheshimiwa Spika,
Mwaka 2012 takwimu zinaonyesha kuwa
deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 15.2. Ndani ya mwaka mmoja wa fedha
kutoka shilingi bilioni 18,258.62 Desemba 2011 na kuwa shilingi bilioni
21,028.61 Desemba 2012 . Kati ya hizo deni la nje lilikuwa ni asilimia 75.97 na
sababu inayotolewa kuwa ndiyo chanzo cha
kuongezeka kwa deni hili kwa kasi namna hiyo ni pamoja na mikopo mipya
kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu hususani ya Barabara na Umeme na
malimbikizo ya riba .
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Waziri Mkuu ambaye ndiye Kiongozi
Mkuu wa Serikali alieleze Bunge hili ni utaratibu gani uliotumika nje
ya Bunge kuchambua na kuithinisha matumizi hayo kwani bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa ajili ya
miradi ya barabara ilikuwa ni shilingi trilioni 1, na bajeti nzima ya nishati
ilikuwa shilingi bilioni 502 ( bajeti
2012/2013) ilhali mkopo huu ulio katika deni la Taifa ni zaidi ya shilling
trilioni 3? Ni miradi gani mikubwa hivyo ya barabara na umeme ambayo
iligharimiwa na fedha hizo kama kweli zilikopwa kwa ajili ya kuhudumia miradi
hiyo.
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Taarifa ya tume ya mipango iliyowasilishwa kwenye
kamati ya Bunge zima na Waziri Stephen Wassira inaonyesha kuwa barabara
zilizojengwa kwa kipindi hicho ni kilomita 170.6 ikilinganishwa na lengo na
bajeti iliyopitishwa na Bunge ya kujenga kilomita 414 kwa mwaka 2012/2013 kwa
barabara kuu kwa kiwango cha lami, hii ikiwa ni sawa na asilimia 41.2 tu ya
lengo lililokuwa limepangwa .
Aidha ukarabati uliofanyika kwa barabara
kuu ulikuwa kilomita 64.57, ikilinganishwa na lengo la kukarabati kilomita 135
kwa mwaka 2012/2013 na kwa upande wa ujenzi na ukarabati wa barabara
zinazounganisha Mikoa na Wilaya ni ujenzi wa kilomita 8.2 tu ndio umekamilika
ukilinganisha na lengo la kujenga kilomita 31.9 kwa mwaka kwa kiwango cha lami.
Kwa upande wa ukarabati ni kilomita 99.45 tu zilikarabatiwa ikilinganishwa na
lengo la kilomita 573.6 zilizokuwa zimepangwa kufanyiwa ukarabati ( chanzo:
taarifa ya ofisi ya rais tume ya mipango).
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Aidha kwa upande wa miradi ya umeme ambayo
ilitekelezwa ni pamoja na maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi ambayo
yamekamilika ikiwa ni pamoja na kulipa fidia wanakijiji wapatao 3,092 na kwa
upande wa mradi wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira kwa ajili ya kuzalisha MW 200
ni stahiki za wafanyakazi kulipwa pamoja na sehemu tu ya madeni ya CRDB, NSSF
na PSPF ndio viliweza kulipwa.
Ni wazi kuwa taarifa hizi mbili yaani ya Waziri wa fedha na ile ya Tume ya mipango inaonyesha wazi kuwa kuna tatizo kubwa kuhusiana na suala la deni la Taifa, kwani upande mmoja unasema fedha hizo zilikopwa kwa ajili ya miradi ya umeme na barabara wakati upande wa tume ya mipango unaonyesha wazi kuwa hakuna miradi kama hiyo iliyoweza kutekelezwa kwa kipindi hicho.
Mheshimiwa Spika,
Ni wazi kuwa taarifa hizi mbili yaani ya Waziri wa fedha na ile ya Tume ya mipango inaonyesha wazi kuwa kuna tatizo kubwa kuhusiana na suala la deni la Taifa, kwani upande mmoja unasema fedha hizo zilikopwa kwa ajili ya miradi ya umeme na barabara wakati upande wa tume ya mipango unaonyesha wazi kuwa hakuna miradi kama hiyo iliyoweza kutekelezwa kwa kipindi hicho.
Mheshimiwa Spika,
Taarifa ya serikali inaonyesha kuwa hakuna
kitengo / idara ya madeni na sasa ndiyo serikali ipo kwenye mchakato wa
kuanzisha idara ya madeni ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa na jukumu la
kujenga uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu na kuhakikisha usimamizi madhubuti
wa deni la Taifa. (Chanzo: Taarifa ya Waziri wa fedha juu ya mwongozo,
matazamio na upeo wa bajeti ya serikali kwa Bunge 2013/2014, tarehe 25 machi
2013)
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Mhe Waziri
Mkuu alieleze Bunge kwa kuwa haikuwepo idara kwa ajili ya uchambuzi juu ya
mikopo hii, nani alikuwa anahusika na kusimamia ukopaji huu na hasa kuhusiana
na riba kwani katika taarifa hiyo takwimu zinaonyesha kuwa fedha iliyolipwa kwa
ajili ya deni la nje kama riba tu ilikuwa kiasi cha shilingi bilioni 66.1
wakati deni halisi tulilipa kiasi cha shilingi bilioni 35.5 na hivyo tulilipa jumla ya shilingi bilioni 101.56 kwa
deni hilo.
Aidha kwa upande wa deni la ndani tulilipa
kiasi cha shilingi bilioni 1,044.85 na kati ya fedha hizo tulilipia riba ya kiasi
cha shilingi bilioni 210.7 tu.
Je, riba halisi kwa ajili ya mikopo hiyo tuliyochukua ilikuwa ni kiasi gani kwa mwaka? Na je madeni mapya riba yake iko kiasi gani kwa mwaka? Na ni kitengo gani kilihalalisha uchukuaji huu wa mikopo hiyo. Ni vyema sasa taarifa rasmi ya madeni ya Taifa yawe yanawekwa hadharani kwani kuna hisia ya kuwepo ufisadi wa kutisha kupitia akaunti ya madeni ya nje kama ilivyokuwa EPA.
Je, riba halisi kwa ajili ya mikopo hiyo tuliyochukua ilikuwa ni kiasi gani kwa mwaka? Na je madeni mapya riba yake iko kiasi gani kwa mwaka? Na ni kitengo gani kilihalalisha uchukuaji huu wa mikopo hiyo. Ni vyema sasa taarifa rasmi ya madeni ya Taifa yawe yanawekwa hadharani kwani kuna hisia ya kuwepo ufisadi wa kutisha kupitia akaunti ya madeni ya nje kama ilivyokuwa EPA.
6.0 GESI ASILIA
Mheshimiwa Spika;
Waziri Mkuu akiwa ndiye msimamizi na
mdhibiti wa shughuli za kila siku za Serikali ndani na nje ya Bunge, anapaswa
kutoa maelezo kuhusu hali inayoendelea hivi sasa katika sekta ndogo (sub
sector) muhimu kwa nchi yetu ya gesi asili kuhusu mazungumzo yanayoendelea na
makampuni mbalimbali ya kimataifa na mikataba inayozidi kusainiwa huku kukiwa
na ombwe la kisera na udhaifu wa kiuongozi katika sekta hizo nyeti hali ambayo
itakuwa na athari za muda mrefu sana kwa taifa.
Mheshimiwa Spika;
Mpaka sasa kwa mfano nchi haina sera ya
gesi asili huku sera ya nishati ikiwa imepitwa na wakati, lakini mazungumzo
yanaendelea na mikataba inazidi kusainiwa bila kuwa na mfumo thabiti wa
kuhakikisha kwamba rasilimali za nchi zinanufaisha wananchi wa maeneo husika
kwa ridhaa yao.
Aidha, kumekuwepo na ufisadi kama ambavyo
ulielezwa pia katika taarifa iliyowasilishwa bungeni Novemba 2011 ambayo msingi
wake ulikuwa pia madai ya Kambi ya Upinzani ya
Julai 2011; hata hivyo mpaka sasa sehemu kubwa ya maazimio ya Bunge toka
wakati huo mpaka sasa hayajatekelezwa kwa ukamilifu.
Wakati ufisadi huo ukiwa haujashughulikiwa,
yameibuka madai mengine ya kasoro katika mkopo wa ujenzi wa Bomba la gesi, huku
kukiwa pia na tuhuma za usiri katika mkataba huo ikiwemo kuhusu dhamana na
masharti mengine yaliyoko kwenye mikataba ya ujenzi wa bomba husika.
Mheshimiwa Spika:
Kutokana na hali hiyo mwezi Februari 2013
katika maswali ya papo k wa papo bungeni, niliuliza swali kwa Waziri Mkuu iwapo mikataba hiyo sasa inaweza
kutolewa kwa bunge na kwa wabunge na kuahidi kwamba wabunge wanaweza kupata
nakala hiyo kwa kufuata masharti ya Sheria naomba ninukuu kauli yake “ serikali
imekwisha kubali kwamba, Bunge hili linayo fursa ya kupata mkataba wowote,
kubwa ni kufuata utaratibu kupitia ofisi ya spika”
Kambi Rasmi ya Upinzani kupitia kwa Waziri
Kivuli wa Nishati na Madini alitumia sheria ya kinga, haki na madaraka ya Bunge
kuomba kuona nakala ya mkataba wa ujenzi wa bomba husika ili kutekeleza wajibu
wa kibunge wa kuishauri na kuisimamia Serikali lakini toka wakati huo mpaka
sasa mikataba hiyo imeendeelea kufanywa kuwa ni siri hata kwa wabunge.
Hata baada ya mazungumzo kati ya Rais wa
Tanzania na Rais wa China masuala hayo yameendelea kufanywa kuwa siri; hivyo
Kambi Rasmi ya Upinzani kupitia Bunge hili inaitaka Serikali kuweka wazi
masharti ya mikopo na dhamana zinazohusika kwa kuzingatia kwamba mwelekeo
unaonyesha kuwa miradi ya chuma na makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga
imetumika kama sehemu ya mpango wenye kuacha maswali mengi kuhusu unyonyaji wa
rasilimali za taifa katika sekta hizo muhimu.
Mheshimiwa Spika:
Udhaifu huo unapaswa kurekebishwa kwa
kuongeza jitihada za kutekeleza ahadi za kuhakikisha kwamba matumizi ya gesi katika viwanda vya mbolea,
viwanda vya bidhaa za kemikali zinazotokana na mafuta (petrochemicals), saruji
na uzalishaji wa umeme katika mikoa ya Mtwara, Iringa, Ruvuma, Dar es Salaam na
maeneo mengine yanayohusika.
Pamoja na Serikali kuingia makubiliano ya
awali (MOU) na Kampuni ya kutoka nchini Marekani ya Symbion kuhusu uzalishaji
wa umeme mkoani Mtwara, ieleze pia hatua ilizochukua katika kurekebisha kasoro
zilizopo kwenye miradi ya Mchuchuma na Liganga na Mnazi Bay kwa kuzingatia
ahadi ilizotoa mwaka 2004.
Mheshimiwa Spika;
Kambi Rasmi ya Upinzani pamoja na kutaka
maelezo zaidi na vielelezo vya ziada kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa bomba la
gesi na matumizi ya gesi; inatoa mwito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Watanzania kwa ujumla kufungua mjadala mpana zaidi wa kitaifa
kuhusu gesi kwa kujikita katika suala la ubovu wa sera ya gesi na mchakato
unaoendelea hivi sasa kuhusu rasimu ya sera hiyo na uozo wa mikataba kwenye
utafutaji, uvunaji na usafirishaji wa gesi.
Serikali badala ya kuendelea kukimbilia
kusaini mikataba mipya kuhusu utafutaji wa gesi asili na mafuta ishughulikie
kwanza ubovu wa mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi kuweka hadharani ripoti
ya uchunguzi kuhusu mikataba 26 ambayo ilikamilika tangu mwaka 2012 na kueleza
hatua ambazo zimechukuliwa toka wakati huo.
Hatua hii ni muhimu kwa kuwa toka kusomwa
kwa orodha ya mafisadi (list of shame ) tarehe 15 Septemba 2007 mpaka sasa
yamekuwa yakitolewa madai mbalimbali kuhusu baadhi ya viongozi na watendaji
kutuhumiwa kufanya ufisadi kupitia mikataba ya utafutaji na uvunaji wa gesi
asili, utafutaji wa mafuta na uchimbaji wa madini na kufichwa kwa fedha katika
akaunti za nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika:
Ziara ya Rais wa China ambayo ilihusisha
usiri katika kusainiwa kwa mikataba 17 ya Sekta mbalimbali imedhihirisha kwa
vitendo kwamba Serikali inayoongozwa na CCM isivyo na dhamira ya kutekeleza
maazimio ya Bunge kuhusu usimamizi wa kibunge kwenye michakato ya mikataba.
Wabunge na wananchi wakumbuke kwamba mwaka
2008 kufuatia kashfa ya Richmond, Bunge lilipitisha azimio kwamba kamati za
kisekta za Bunge zihusishwe kwa niaba ya wananchi kwenye maandalizi ya mipango
na mikataba kuanzia hatua za awali ili kuishauri na kuisimamia Serikali; azimio
ambalo halitekelezwi na hivyo kuibua migogoro kati ya wananchi na wawekezaji na
maeneo mengine kufanya nchi kuingia mikataba mibovu.
Mathalani, wakati Tanzania imekopa mkopo
mkubwa kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa Bomba la gesi; miaka michache
iliyopita kutokana na udhaifu wa mipango na mikataba ulifanyika ujenzi wa Bomba
lingine kutoka Songosongo chini ya kampuni ya Songas kwa mkopo. Hata hivyo,
katika mradi huo kulijengwa bomba lenye kipenyo kidogo na matokeo yake ni
kwamba miaka michache baadaye taifa linaingia gharama kubwa ya mkopo mwingine
kutokana na upungufu wa miundombinu ya gesi asili huku kukiwa na mzigo wa
madeni makubwa ya mikopo ya awali. Serikali inapaswa kutoa maelezo kuhusu hatua
ilizochukua kurekebisha hali hiyo toka wakati huo na kuhakikisha uwajibikaji wa
viongozi na watendaji waliohusika ambapo wengine mpaka sasa bado wako katika
ofisi za umma.
7.0 BUNGE KAMA
MUHIMILI WA KUISIMAMIA NA KUISHAURI SERIKALI
Mheshimiwa
Spika, mamlaka ya Bunge
yameainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara za 62 hadi 64. Ibara
hizi zote zinaeleza majukumu ya Bunge juu ya kusimamia utendaji mzima wa
Serikali katika mchakato wa kuwapatia huduma za msingi wananchi.
Mheshimiwa
Spika, jukumu hili kwa hali
ilivyo sasa linashindwa kutekelezeka kutokana na ukweli kwamba Bunge linakosa
taarifa au uelewa wa kutosha kuhusu sekta mbalimbali za kiutendaji. Kwa hali ya
kawaida ni vigumu kumshauri au kumsimamia mtu bila ya kuwa na uelewa wa ziada
kumzidi yule unaye mshauri au kumsimamia.
Mheshimiwa
Spika, ili kukidhi matakwa
ya Ibara ya 64 ni lazima Kurugenzi husika ndani ya Bunge kuwezeshwa kuwa na
watendaji wanaoweza kuwasaidia waheshimiwa wabunge kutimiza matakwa ya Ibara
hiyo.
Mheshimiwa
Spika, sambamba na hilo,
Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka kuelewa toka kwa Mhe Waziri Mkuu, Miswada
binafsi ya waheshimiwa wabunge Zitto Kabwe uliohusu mabadiliko ya sheria ya
maadili ya viongozi na John Mnyika uliohusu uanzishwaji wa baraza la vijana la
Taifa ambayo tayari imekwishawasilishwa Ofisini kwa Katibu wa Bunge ni lini
italetwa rasmi Bungeni kwa utaratibu wa kuzifanya ziwe sheria za nchi?
Mheshimiwa
Spika, Katika hotuba yangu
ya mwaka jana nilieleza kuhusu Watendaji wa Serikali kushindwa kutimiza
masharti ya kifungu cha 10 cha sheria ya Haki na Madaraka ya Bunge mwaka 1988
na marejeo yake ya mwaka 2002. Hali ya kutokuheshimu sheria hii bado
inaendelea, Waheshimiwa wabunge wameomba kupatiwa nyaraka mbalimbali toka
Serikalini kupitia kwa Katibu wa Bunge, lakini kwa bahati mbaya hadi sasa
nyaraka hizo bado hazijatolewa.
Mheshimiwa
Spika, katika hali kama
hii, je Bunge linaweza kukidhi matakwa ya Ibara za 63? Utaishauri vipi na
kuisimamia Serikali ukiwa huna taarifa za kutosha? Je, ni mara ngapi
waheshimiwa Mawaziri wametoa majibu ya kudanganya na kupelekea waheshimiwa
wabunge kukiambia kiti kuwa Waziri hajajibu swali lake? Mapungufu haya yote
yanasababishwa na kutokuwepo kwa taarifa sahihi na za ziada kuwawezesha
waheshimiwa wabunge kufanyakazi ili kukidhi matakwa ya Kikatiba.
Mheshimiwa Spika, Katika moja ya taarifa za asasi za kiraia zinazofuatilia mwenendo wa
Bunge, pamoja na mambo mengine zimeonesha kuwa Bunge letu ni dhaifu na kuwa
halitekelezi majukumu yake. Taarifa za Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na The Citizens’ Parliament Watch (CPW)
za Februari 13, 2013 zimeonesha kuwa
“…kumeendelea kuwa na mivutano yenye upendeleo wa vyama
katika kujadili na kuchangia hoja na kuonekana Mh Spika, Naibu Spika na
Wenyeviti wa vikao kutumia vibaya kanuni za Bunge kuwadhibiti Wabunge kulingana
na vyama vyao. Ukiukwaji wa Kanuni za Bunge, matumizi mabaya ya muda na kukosa
tija kumeendelea kuliathiri Bunge letu. Aidha baadhi
ya Wabunge wamekuwa na matumizi ya lugha zisizostahili Bungeni na hata
kushambuliana katika ubinafsi wao. Wakati wabunge wengine wakitumia muda wao nje ya Bunge
kukutana na wananchi na kueleza ufanisi wao ndani ya Bunge, wengine wametumia
nafasi hizo kupingana na wananchi na kulidhalilisha Bunge mbele ya jamii”.
Mheshimiwa
Spika, Asasi hizi
zinatukumbusha mambo muhimu sana kwa jamii yetu. Tuna kila wajibu wa kuwatendea
haki watu wetu na kutafakari taarifa zinazotupima utendaji wetu na kuchukua
hatua kurekebisha udhaifu huu.
8.0 MAMBO MUHIMU YA
KUKUMBUSHA
Mheshimiwa Spika, mara kadhaa,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA imekuwa ikiitaka
Serikali kutekeleza mambo ya msingi katika usitawi na maenedeleo ya Taifa hili
lakini kwa masikitiko makubwa ni kwamba Serikali hii ya CCM inayojiita sikivu
imeendelea kuziba masikio yake juu ya mahitaji muhimu kwa Taifa.
Kwa mfano, Kambi
Rasmi ya Upinzani ilitoa pendekezo zuri la kuwapatia wazee wote pensheni
(Universal Pension) sambamba na kuwa na mpango maalum wa kuwawezesha wazee wetu
hawa kuishi maisha ya amani katika siku zao za uzeeni.
Licha ya Kambi ya
Upinzani kuonesha njia ya kupata fedha za kuwalipa wazee hawa, lakini mpaka leo
Serikali imekuwa na kigugumizi cha kutekeleza nia hii njema. Jambo hili
linapelekea Kambi ya Upinani iamini kwamba Kauli aliyoitoa Waziri Mkuu, tarehe
01 Oktoba, 2009 wakati akiwahutubia wazee kwamba: “Wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika kukuza uchumi wa nchi yetu
na kuleta mabadiliko ya kiuchumi” ilikuwa ni kuwakejeli na kuwahadaa
wazee waliovuja jasho kuijenga nchi hii hadi hapa ilipo. Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali ieleze ukweli
ili wazee hawa wajue kama Serikali imeamua kuwatupa wajitafutie utaratibu
mwingine wa maisha.
Mheshimiwa
Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikipiga kelele sana juu ya matumizi mabaya ya
fedha za umma unaofanywa na Serikali kwa kisingizio cha uendeshaji wa shughuli
za Serikali. Limekuwa ni jambo la
kawaida kwamba katika bajeti ya Waziri Mkuu, na wizara nyingine, fedha za
matumizi ya kawaida ni takribani asilimia 80 wakati fedha za maendeleo ni ni
takriban asilimia 20 tu. Jambo la kushangaza hapa ni kwamba hata hii asilimia
20 ya fedha za maendeleo, zaidi ya nusu zinatoka kwa wahisani. Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali iueleze umma wa watanzania: Kipi ni kipaumbele;
kutumia fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa matumizi ya ofisi, au kuwaletea
wananchi maendeleo?
Aidha ni vyema Serikali ikaeleza Taifa ni njia gani
inatumia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwani kila siku tunaona kukua kwa
kutisha kwa matumizi ya kawaida ya Serikali. Ni dhahiri hakuna uchungu na fedha
za walipa koda kwa Serikali hii ya CCM.
Mheshimiwa
Spika, Jambo
jingine ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ingependa kuikumbusha Serikali ni kuhusu
Sherehe za Kitaifa. Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukihoji matumizi
yasiyofanyiwa ukaguzi ya sherehe za kitaifa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka
Serikali kuweka bayana matumizi ya fedha katika Sherehe za kitaifa kuwa kuwa
fedha inayotumika ni fedha ya wananchi.
Mheshimiwa
Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaikumbusha tena Serikali kusema ukweli kuhusu
dhamira ya kuhamia Dodoma. Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri tena Serikali kufuta
mpango huu kwani ni upotezaji wa fedha za wananchi na fedha zinazopotezwa
zielekezwe kwenye mipango mingine ya maendeleo na Dodoma iendelee kuwa mji wa Kibunge na Elimu
kama ambavyo Kambi Rasmi ya Upinzani imekuwa ikishauri kila wakati.
9.0 MAPITIO YA
UTEKELEZAJI WA BAJETI 2012/2013 NA UCHAMBUZI WA BAJETI YA 2013/2014
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, Ofisi ya
Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake iliidhinishiwa kiasi cha shilingi
bilioni 35.2 ikiwa ni matumizi ya kawaida.
Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 3.4 ilikuwa ni mishahara ya
watumishi, shilingi bilioni 10.6 ikiwa ni ruzuku kwa taasisi, na shilingi
bilioni 21.1 matumizi mengineyo. Hadi kufikia Februari 2013, shilingi bilioni
20.7 sawa na asilimia 59 zilikuwa zimepokelewa kutoka hazina.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Miradi ya Maendeleo, Ofisi
ya Waziri Mkuu ilitengewa shilingi bilioni 91.7 lakini hadi kufikia Februari,
2013 ni kiasi cha shilingi bilioni 10.7 sawa na asilimia 11.7zilizokuwa zimetumika katika miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Spika, kwa mchanganuo huo ni kwamba fedha za
matumizi ya kawaida zinatumika zaidi kuliko fedha za maendeleo. Aidha, karibu asilimia 90 ya bajeti ya
maendeleo, Ofisi ya Waziri Mkuu haikutekelezwa hadi kufikia Februari 2013.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Waziri
Mkuu atoe majibu kuwa inawezekanaje hadi kufikia “quota” ya 3 ya mzunguko wa
bajeti, asilimia 90 ya bajeti ya maendeleo haijatekelezwa?
Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka huu 2013/2014 Ofisi ya Waziri
Mkuu inaomba kuidhinishiwa shilingi bilioni 35.08 kwa matumizi ya kawaida na
shilingi bilioni 43.87 kwa bajeti ya maendeleo. Wakati matumizi ya kawaida
yamepungua kwa asilimia 0.34 ukilinganisha na mwaka 2012/2013, bajeti ya
maendeleo imepungua kwa asilimia 52.2 ukilinganisha na mwaka 2012/2013.
Mheshimiwa Spika, licha ya bajeti ya maendeleo kupungua kwa
zaidi ya nusu ukilinganisha na mwaka jana bado imeendelea kuwa tegemezi kwa
wahisani. Katika shilingi bilioni 43.87
za maendeleo, shilingi bilioni 37.87 sawa na asilimia 86.3 ni fedha za
nje na shilingi bilioni 6 sawa na asilimia 13.7 ni fedha za ndani.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haiamini kama
tunaweza kupata maendeleo ya kweli kwa kutegemea fedha za wahisani katika
bajeti za maendeleo.
Mheshimiwa Spika, katika miradi ya meaendeleo imetengwa shilingi bilioni moja kwa ajili ya
uendelezaji wa kuzikia viongozi wa Kitaifa. Kambi ya Upinzani inataka kujua kama
ni ombi la viongozi wa kitaifa kuandaliwa eneo maalumu la kuzikwa au ni utashi
wa Serikali kufikiri kwamba viongozi wa kitaifa wanahitaji eneo maalumu la
kuzikwa!
Kwa uzoefu ni kwamba waasisi wa Taifa hili
walizikwa kwenye makazi yao. Kwa nini viongozi wa kitaifa walio hai sasa
wasifuate mfano huo? Hivi kweli kuna mantiki yoyote ya kutumia shilingi bilioni
moja ya kuandaa sehemu ya kuzikia watu ambao hawajafariki wakati kuna watu
wenye njaa, wagonjwa, wamama wajawazito wanaojifungulia sakafuni ambao wanahitaji
huduma ya matibabu na dawa ili wapone?
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya maendeleo, Kitengo cha
Maafa kimetengewa shilingi bilioni 1.8 kwa
ajili ya kujenga uwezo wa kukabiliana na maafa. Mheshimiwa Spika, Watanzania
wameshuhudia maafa makubwa katika nchi yetu hasa ya kuzama kwa Meli kwa mfano
Meli ya MV Bukoba, Meli ya MV Skagit na Meli ya MV Spice Islanders huko
Zanzibar na pia wameshuhudia kuporomoka kwa maghorofa na mengine kuungua moto.
Katika ajali na maafa haya Watanzania wengi walipoteza maisha yao na daima
waokoaji wa ndani wamekuwa na uwezo mdogo sana wa kuokoa watu na hivyo
kutegemea zaidi waokoaji na vifaa toka nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini kuwa
fedha hizi ni ndogo na hivyo ni vyema Serikali ieleze uwezo huo unaokusudiwa
kujengwa ni upi!
Mheshimiwa Spika, katika kupunguza gharama za uendesha wa shughuli za Serikali, Kambi ya Upinzani imekuwa ikipinga
matumizi mabaya ya fedha za umma na hasa posho za vikao (sitting allowances)
kwa kuwa vikao ni sehemu ya majukumu yao ambayo wanalipwa mshahara. Kambi Rasmi
ya Upinzani inazidi kusisitiza kuwa posho za vikao zifutwe kwani zinaongeza
gharama za uendeshaji wa Serikali ambazo si za lazima.
Jedwali lifuatalo linaonesha tofauti ya posho za
vikao katika kasma 210314 kwenye Fungu 37 kwa idara zilizo Ofisi ya Waziri Mkuu kati ya
mwaka wa bajeti 2012/2013 na 2013/2014.
Chanzo: Randama Ofisi ya Waziri Mkuu, Fungu 37
KASMA
|
IDARA
|
POSHO YA VIKAO-
2012/2013
|
2013/2014
|
210314
|
Utawala
|
95,000,000
|
92,000,000
|
Fedha na Uhasibu
|
20,250,000
|
8,850,000
|
|
Sera na Mipango
|
31,500,000
|
19,950,000
|
|
Ukaguzi wa Ndani
|
17,400,000
|
17,400,000
|
|
Habari, Elimu na Mawasiliano
|
3,000,000
|
3,000,000
|
|
Ugavi
|
20,000,000
|
42,000,000
|
|
Sheria
|
1,500,000
|
1,200,000
|
|
Menejimenti ya Mifumo ya Habari
|
800,000
|
600,000
|
|
Uratibu wa Maafa
|
39,000,000
|
39,000,000
|
|
Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa
|
47,000,000
|
47,000,000
|
|
Bunge na Siasa
|
15,000,000
|
16,000,000
|
|
Maendeleo ya Sekta Binafsi
|
24,000,000
|
43,500,000
|
|
Uratibu wa Shughuli za Serikali
|
100,500,000
|
61,500,000
|
|
Mpiga Chapa wa Serikali
|
55,100,000
|
53,000,000
|
|
470,050,000
|
445,000,000
|
||
Tofauti kati ya matumizi ya mwaka wa fedha 2012/13 na 2013/14 ni
shilingi 25,050,000/-
Mheshimiwa Spika,
Baada ya maelezo haya naomba
kuwasilisha.
......................................................................
FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB)
KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI MKUU, OFISI YA WAZIRI MKUU
11.04.2013
KIAMBATANISHO
A
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA
WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA YA UTAFITI
KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA
UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO
CHA 4 MWAKA 2010
Dar Es Salaam
Juni, 2011
Rasimu 2
i
SHUKRANI
Utafiti
huu umehusisha wataalamu mbalimbali katika hatua za kubuni, kutayarisha,
kukusanya,
kuchambua takwimu na kuandika ripoti. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi
kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
kwa
pamoja zinawashukuru wataalamu wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine
katika
hatua mbalimbali za utafiti huu. Pia tunawashukuru wadau wote wa elimu
waliohusika
katika kutoa taarifa za utafiti. Aidha shukrani za pekee ziiendee Wizara ya
Fedha
kwa kufanikisha mchakato mzima wa utafiti.
Shukrani
pia zimwendee Bwana Jumanne Abdallah Sagini, Naibu Katibu Mkuu -
TAMISEMI
kwa kuwa msimamizi mkuu wa kazi hii. Aidha, shukrani za dhati ziwaendee
wajumbe
wa kikundi kazi kilichohusika katika utafiti huu kuanzia hatua za awali hadi
mwisho.
Wajumbe hao ni:
JINA
TAASISI WADHIFA
1.
Francis M. Liboy OWM-TAMISEMI - Mwenyekiti
2.
Lawrence John Sanga WEMU - Katibu
3.
Fred Davidson Sichizya WEMU - Mjumbe
4.
Abdallah Shaban Ngodu WEMU - Mjumbe
5.
Hadija Mchatta Maggid WEMU - Mjumbe
6.
Paulina Jackson Mkoma WEMU - Mjumbe
7.
Elia Kalonzo Kibga WEMU - Mjumbe
8.
Paulina Mbena Nkwama OWM-TAMISEMI - Mjumbe
9.
Makoye J.N. Wangeleja TET - Mjumbe
10.Edward
Simon Haule NECTA - Mjumbe
Aidha
shukrani zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa TET kwa kugharamia vikao vya kikundi
kazi
kupitia huduma ya ukumbi na chakula wakati kikiwa Dar-es-salaam.
Prof.
Hamisi O. Dihenga
Katibu
Mkuu
Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Rasimu 2
ii
DIBAJI
Ripoti
hii ya utafiti inahusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa
Kidato
cha
4 mwaka 2010. Utafiti huu umefanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri
Mkuu-
Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya
Ufundi (WEMU) ikihusisha Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani la
Tanzania.
Utafiti
huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa
Taifa
wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri kwa
wadau
wa elimu Serikali iliamua kufanya utafiti ili kuweza kubaini chanzo na ukubwa
wa
tatizo.
Utafiti huu unatoa mapendekezo kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu na ubora wa
elimu
ya sekondari.
Ripoti
hii inaonesha kwamba yapo masuala ya kimfumo, mfano mapungufu katika
usimamizi
na uendeshaji wa elimu nchini ambayo yanaweza kutatuliwa na serikali moja
kwa
moja. Aidha, yapo masuala yanayohusu kujenga uwezo kwa wasimamizi na
watekelezaji
wa mitaala, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora na vya kutosha vya
kufundishia
na kujifunzia na uboreshaji wa majengo na miundombinu ambayo
yanahitaji
nguvu ya pamoja kati ya serikali na wabia wake.
Matokeo
ya utafiti huu ni muhimu kwa serikali, washirika wa maendeleo na wadau
mbalimbali
wa elimu kwani inaonesha chanzo na ukubwa wa matatizo na changamoto
zinazojitokeza
na inatoa mapendekezo ya namna ya kuyatatua na kukabiliana na
changamoto
za kielimu. Hivyo sote kwa pamoja yatupasa tujipange na kuelekeza nguvu
zetu
kupitia mipango yetu ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili tuweze
kuyamaliza
matatizo haya na kuinua ubora wa elimu nchini.
Ninawaomba
wadau wa elimu nchini kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ili kuweza
kupiga
hatua katika utekelezaji wa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Serikali inayo
nia
ya dhati ya kutekeleza mapendekezo haya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa
elimu
ya
sekondari nchini.
Mh.
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB)
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Rasimu 2
iii
YALIYOMO
SHUKRANI............................................................................................................................................
i
DIBAJI...................................................................................................................................................
ii
VIFUPISHO...........................................................................................................................................
v
MUHTASARI
PEMBUZI.....................................................................................................................
vi
SURA
YA KWANZA:
UTANGULIZI................................................................................................
15
1.1.
Usuli ......................................................................................................................................
15
1.2.
Hoja ya Kufanya Utafiti .......................................................................................................
18
1.3.
Malengo ya Utafiti................................................................................................................
19
1.4.
Maswali ya Utafiti.................................................................................................................
19
1.5.
Muundo wa Ripoti................................................................................................................
20
SURA
YA PILI: MAPITIO YA
MAANDIKO....................................................................................
21
2.1
Sera na Mipango ya Elimu..................................................................................................
21
2.2
Mipango na Mikakati ya Elimu ...........................................................................................
22
2.3
Uongozi katika Elimu ...........................................................................................................
23
2.4
Usimamizi na Uendeshaji....................................................................................................
24
2.5
Ugharamiaji wa Elimu .........................................................................................................
25
2.6
Ufuatiliaji na Tathimini ya Elimu........................................................................................
27
SURA
YA TATU: MWONGOZO WA
UTAFITI...............................................................................
55
3.1.
Utangulizi ..............................................................................................................................
55
3.2.
Mbinu ya Utafiti ....................................................................................................................
55
3.3.
Eneo la Utafiti .......................................................................................................................
56
3.4.
Uchaguzi wa Sampuli ..........................................................................................................
56
3.5.
Zana za Utafiti ......................................................................................................................
57
3.6.
Utaratibu Uliotumika Kufanya Utafiti ................................................................................
58
3.6.1.
Kukusanya Taarifa Kutoka Ngazi ya Taifa ................................................................
58
3.6.2.
Kukusanya Taarifa Kutoka katika Kanda, Mkoa na Halmashauri ..........................
58
3.6.3.
Kukusanya Taarifa Kutoka Shuleni na katika Jamii.................................................
59
3.7.
Uchambuzi wa Data.............................................................................................................
59
3.8.
Maadili ya Kufanya Utafiti...................................................................................................
59
SURA
YA NNE: MATOKEO YA UTAFITI NA UCHAMBUZI WA
DATA................................... 61
4.1.
Utangulizi ..............................................................................................................................
61
4.2.
Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ..................................................................................
63
4.2.1.
Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Ngazi Mbalimbali.................................
63
4.2.2.
Mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii......................................................................
68
4.2.3.
Mwamko Duni wa Jamii Katika Elimu........................................................................
69
4.2.4.
Siasa Kuingilia Masuala ya Kitaalam ya Kielimu.......................................................
69
4.2.5.
Ufinyu wa Bajeti ya Elimu ...........................................................................................
70
4.2.6.
Maoni Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu .................................................
71
4.2.7.
Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka
2010
75
4.3.
Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala .............................................................................
76
4.3.1.
Utayarishaji wa Mitaala................................................................................................
76
Rasimu 2
iv
4.3.2.
Uwepo wa Mihtasari Shuleni na Vyuoni....................................................................
77
4.3.3.
Utekelezaji wa Mtaala ..................................................................................................
78
4.3.4.
Mafunzo Kabilishi kwa Ajili ya Mtaala Ulioboreshwa ...............................................
79
4.3.5.
Maoni Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala ........................................................................
79
4.4.
Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa...........................................................................
80
4.4.1.
Utungaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 .......................................................
80
4.4.2.
Usambazaji na Usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4..........................
82
4.4.3.
Usahihishaji wa Mtihani ya Taifa wa Kidato cha 4 ..................................................
83
4.4.4.
Mchango wa Alama za Mazoezi Endelezi (Continuous Assessment-CA)
Katika
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4................................................................................
85
4.4.5.
Upangaji wa Madaraja Unaofanywa na NECTA .......................................................
86
4.4.6.
Matumizi ya Miongozo na Nyaraka Mitihani .............................................................
88
4.4.7.
Athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2............................................................
88
4.4.8.
Maoni Kuhusu Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa .........................................
90
4.5.
Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ...................................................
93
4.6.
Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu...............................................................
97
4.6.1.
Mfumo wa Utayarishaji wa
Walimu...............................................................................
97
4.6.2.
Ajira na Upangaji wa Walimu .....................................................................................
98
4.6.3.
Uwepo wa Walimu katika Shule
..................................................................................
100
4.6.4.
Maoni ya Kuimarisha Ubora na Uwepo wa Walimu ..............................................
106
4.7.
Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia ........................................................
108
SURA
YA TANO: HITIMISHO NA
MAPENDEKEZO..................................................................
115
5.1.
Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................................................
115
5.2.
Utekelezaji wa mitaala ......................................................................................................
118
5.3.
Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa.........................................................................
119
5.4.
Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu .................................................
121
5.5.
Mfumo wa utayarishaji wa walimu..................................................................................
121
5.6.
Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia..........................................................................
124
REJEA
...............................................................................................................................................
126
VIAMBATISHO
...............................................................................................................................
130
Kiambatisho
Na. 3.1: Maeneo Yaliyohusika katika Utafiti ......................................................
130
Kiambatisho
3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa...........................................
132
Kiambatisho
4.1 – Takwimu za ukaguzi wa shule ( 2007–2010) katika Halmashauri
zilizofanyiwa
utafiti.......................................................................................................................
133
Rasimu 2
v
VIFUPISHO
BEST
Basic Education Statistics in Tanzania
CA
Continuous Assessment (Mazoezi Endelezi)
CG
Capitation Grant
CDTI
Community Development Training Institute
CWT
Chama cha Walimu Tanzania
EFA
Education for All
EMAC
Educational Materials Approval Committee
ETP
Education and Training Policy
FDC
Folk Development College
FTC
Full Technician Certificate
GBS
General Budget Support
GDP
Gross Domestic Product
GER
Gross Enrolment Rate
MKUKUTA
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania
MMES
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
MEMK-WSM
Mkakati wa Elimu ya Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Shule za
Msingi
MMEM
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
MMEMWA
Mkakati wa Menejimenti na Maendeleo ya Walimu
MoEVT
Ministry of Education and Vocational Training
MWAKEM
Mafunzo ya Walimu Kazini Elimu ya Msingi
MTEF
Medium Term Expenditure Framework
MDGs
Milemium Development Goals (Malengo ya Maendeleo ya Milenia)
MUCE
Mkwawa University College of Education
NCDF
National Curriculum Development Framework
NECTA
National Examinations Council of Tanzania
OC
Other Charges
OUT
Open University of Tanzania
OWM-TAMISEMI
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
PETS
Public Expenditure Tracking System
SEDP
Secondary Education Development Programme
TAMONGSCO
Tanzania Association of Managers of Non Government Schools and
Colleges
TEHAMA
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
TET
Taasisi ya Elimu Tanzania
TEN/MET
Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania
TES
Tanzania Elimu Supplies
TIE
Tanzania Institute of Education
TSD
Teachers Service Department (Idara ya Huduma kwa Walimu)
UKIMWI
Ukosefu wa Kinga Mwilini
URT
United Republic of Tanzania
TRC
Teachers Resource Centre
UPE
Universal Primary Education (Elimu ya Msingi kwa Wote)
WEMU
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Rasimu 2
vi
MUHTASARI
PEMBUZI
Utoaji
wa elimu nchini Tanzania unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo (ETP) ya
mwaka
1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya
Taifa
2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya
Maendeleo
ya Milenia (MDGs).
Katika
kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu
ilianzishwa.
Aidha, Programu za Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na
Sekondari
(MMES) zilianzishwa kutekeleza program ya sekta. Mafanikio ya MMEM
yameongeza
mahitaji ya upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango wa
Maendeleo
ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu la
kuongeza
uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-
2014)
imeweka kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari.
Kiwango
cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila
mwaka
kwa mfululizo wa miaka minne 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na
2010
(50.4%). Kutokana na hali hiyo, Serikali iliamua kufanya utafiti ili kubaini
sababu
za
kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na
tatizo
hilo.
Utafiti
huu ulifanyika katika mikoa 11, ikiwa ni mmoja kwa kila Kanda ya Elimu. Aidha,
jumla
ya Halmashauri 22 zilihusishwa, mbili kutoka kila mkoa ikiwa moja iliyofanya
vizuri
na nyingine iliyofanya vibaya katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Kwa kila
Halmashauri
jumla ya shule sita zikiwemo nne za serikali na mbili zisizo za serikali
zilihusika
katika utafiti huu. Jumla ya shule 132 ambapo 88 ni za Serikali na 44 ni
shule
zisizo za Serikali zilihusishwa. Pia, ofisi za elimu na ukaguzi wa shule,
Taasisi ya
Elimu
Tanzania (TET), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), pamoja na baadhi ya
asasi
za serikali na zisizo za serikali zilihusishwa. Jumla ya wajibuji 3,894
walilengwa
katika
utafiti ambapo washiriki 3,037 sawa na asilimia 80.0% walifikiwa.
Taarifa
na takwimu za utafiti zilikusanywa kwa kutumia Madodoso, Majadiliano ya
Pamoja,
Hojaji, maandiko na makala mbalimbali. Uchambuzi wa takwimu umefanyika
kwa
kuwasilisha hoja za wajibuji katika namba (asilimia), majedwali na chati ili
kuleta
Rasimu 2
vii
taarifa
zenye mantiki kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti kuhusu
kushuka
kwa kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 2010
yamewasilishwa
kama ifuatavyo:-
a)
Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
Utafiti
umedhihirisha kuwa matatizo yanayohusu usimamizi na uendeshaji
yameathiri
ufanisi katika utoaji wa elimu bora nchini. Baadhi ya viongozi wa
elimu
huteuliwa bila kuzingatia utaalamu, taaluma, uwajibikaji, uwezo na
uadilifu.
Aidha, maamuzi ya kitaalamu kuhusu uendeshaji wa elimu hufanyika
kisiasa
bila kuzingatia utaalamu na tafiti. Vile vile ufinyu wa bajeti ya Wizara ya
Elimu
na TAMISEMI (Elimu) unafanya usimamizi na uendeshaji wa elimu
kutokuwa
fanisi.
Utekelezaji
wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada na ziada umekuwa na
changamoto
ambazo zimeathiri uchapishaji, usambazaji na upatikanaji wa vitabu
vyenye
ithibati katika shule na vyuo. Aidha, kuna uelewa mdogo kwa wanafunzi
na
walimu katika matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia na kujifunzia
katika
shule za sekondari na vyuo vya ualimu.
Utafiti
umebaini kuwa, mmomonyoko wa maadili kama vile matumizi ya lugha
mbaya;
matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),
kutozingatia
mafundisho ya dini, matumizi ya dawa za kulevya na kujiingiza
katika
masuala ya mapenzi ni masuala yaliyobainishwa kuchangia kumeathiri
maendeleo
ya taaluma shuleni.
b)
Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala
Utafiti
umeonesha kuwepo kwa changamoto za utayarishaji na utekelezaji wa
mtaala
kwa miaka mitano iliyopita. Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005
umetekelezwa
bila kufanyiwa majaribio (piloting). Aidha, utafiti umebaini kuwa
kwa
miaka mitatu iliyopita (2008 hadi 2010), jumla ya walimu 588 (1.5%)
walipata
mafunzo kabilishi. Taarifa hii inaonesha kuwa walimu wengi hawana
maarifa
na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari uliboreshwa.
Rasimu 2
viii
Ni
muhimu watekelezaji mitaala kupatiwa mafunzo kabilishi ili kuimarisha
utendaji
kazi wao na kuwawezesha kupata fursa ya mabadiliko ya mtaala, dhana
na
nadharia za ufundishaji na ujifunzaji.
Pia,
utafiti umebaini upungufu wa mihtasari ya mtaala ulioboreshwa katika shule
za
sekondari. Katika shule zilizofanyiwa utafiti, takwimu zinaonesha kuwa kuna
upungufu
wa mihtasari kwa wastani wa asilimia 45.4 ambapo masomo ya
Mathematics
na Geography yameongoza kwa kuwa na upungufu wa zaidi ya
asilimia
50. Vilevile, kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka
TET
kwenda shuleni.
c)
Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu
Utafiti
huu ulilenga Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya
utoaji
wa elimu, utekelezaji wa mtaala na ukaguzi wa shule.
Utafiti
ulibaini kuwa asilimia 49 ya wakuu wa shule hawafuatilii kikamilifu utoaji
wa
taaluma shuleni, hali hii inapunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.
Hivyo
inapaswa wakuu wa shule wasimamie kikamilifu majukumu yao kama
ilivyoainishwa
katika Mwongozo wa Usimamizi wa Shule.
Aidha,
ilibainika kuwa hakuna ufuatiliaji wala tathmini iliyofanyika tangu mtaala
wa
elimu ya sekondari ulioboreshwa uanze kutumika mwaka 2005 na kwamba
mitaala
hiyo haikufanyiwa majaribio kabla ya utekelezaji wake. Kutofanya
tathmini
kwa wakati kuhusu utekelezaji wa mtaala hakutoi fursa kwa serikali na
wadau
wa elimu kubaini matatizo na changamoto za utoaji elimu na kuyapatia
ufumbuzi
kwa wakati na hivyo kupunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji
Pia
utafiti umebaini kuwa, katika shule 132 zilizotembelewa, shule 18 (13.53%)
zilikaguliwa
mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010. Hali kadhalika
shule
6 (51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na shule 46 (34.59%)
hazikukaguliwa
kabisa. Aidha, taarifa za ukaguzi wa shule hazifanyiwi kazi
ipasavyo.
Kutokaguliwa kwa shule hizo za sekondari kumepunguza ufanisi wa
usimamizi
na utoaji wa elimu bora.
Rasimu 2
ix
d)
Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu
Ufaulu
wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa huchangiwa na sababu mbalimbali.
Uwepo
wa walimu wenye sifa stahiki shuleni ni moja ya sababu muhimu.
Utafiti
umebaini kuwa, sifa za udahili kwa walimu tarajali wa stashahada ni za
ufaulu
wa kiwango cha chini (1Principal na 1Subsdiary) katika masomo ya
kufundishia
na baadhi yao hawana wito wa kazi ya ualimu. Aidha utafiti umebaini
kuwa
kuna changamoto katika matayarisho ya walimu tarajali unaosababishwa
na
upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Aidha,
matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu
kimasomo
hususani katika masomo ya sayansi na Mathematics unaosababishwa
pia
na upangaji usiozingatia mahitaji hususan katika sehemu zenye mazingira
magumu.
Katika shule zilizofanyiwa utafiti imebainika kuwa somo la
Mathematics,
lina mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo
kuna
upungufu wa walimu 264 sawa na asilimia 60.6. Tatizo la upungufu wa
walimu
ni changamoto katika utoaji wa elimu.
e)
Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
Matokeo
mbalimbali yahusuyo mfumo wa mitihani yamebainishwa ikiwa ni
pamoja
na muundo wa maswali yatolewayo shuleni kutokidhi viwango
vinavyotumika
na NECTA.
Aidha,
Miundo ya mitihani ya Taifa haiwafikii baadhi ya walimu na wanafunzi na
hivyo
kutoielewa. Hii inaonesha jinsi ambavyo baadhi ya walimu na wanafunzi
hawapati
fursa ya kuiona na kuitumia miundo ya mitihani na miongozo katika
shule
za sekondari. Uwepo wa Nyaraka na miongozo mbalimbali ya mitihani
katika
shule ni muhimu katika kumwandaa mtahiniwa hivyo, wadau wote
wanapaswa
kupata na kutumia machapisho hayo.
Utafiti
umebaini kuwa, uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule haufanywi
kwa
makini. Aidha, utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts’
walizosahihisha
badala ya posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji
Rasimu 2
x
kwa
siku ni baadhi ya masuala yanaweza kuchangia kupungua kwa umakini wa
usahihishaji.
Aidha
utafiti umebaini kuwa, mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45%
majaribio
na mazoezi na 5% projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au
mchakato
wake katika matokeo ya mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu.
Hata
hivyo NECTA wanatumia vigezo vingine vya ulinganifu sanifu ambavyo
mchakato
wake wa kuvitumia haueleweki kwa wadau. Aidha utafiti umebaini
kuwa,
gredi zinazotumika shuleni kwa uzoefu wa miaka mingi ni A (81-100), B
(61-80),
C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa
alama
za gredi zinazotumika kwa Mtihani wa Taifa wa K4 huamuliwa na Kamati
ya
Kutunuku ambapo gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si chini ya alama
70.
Hali hii ya kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu baina ya shule
na
NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama za gredi. Vilevile, kuna
mapungufu
ya kuadhibu watahiniwa kwa kuteremshwa daraja la I au la II kuwa
la
III kutokana na kufeli baadhi ya masomo ya msingi na ya mchepuo.
f)
Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
Utafiti
umebaini kuwa katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti, kuna upungufu mkubwa
wa
miundombinu, samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni ikijumuisha
maabara
ya Chemistry (79.6%), Biology (66%) na Physics (65.2%) nyumba za
walimu
(72%), na maktaba (80.6%). Aidha, baadhi ya shule zimepata usajili bila
kutimiza
vigezo na nyingine kujengwa mbali na makazi ya jamii husika. Vilevile
utafiti
umebaini upungufu wa vifaa vya kufundishia ikiwa ni pamoja na vitabu vya
kiada
na ziada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa kwa baadhi ya masomo
kwa
wastani wa 75.5% katika shule zilizofanyiwa utafiti.
Matokeo
ya utafiti pia yamebaini kutokuwepo kwa chakula cha mchana kwa
wanafunzi
katika shule za kutwa, na hivyo kuathiri mahudhurio na umakini wa
wanafunzi
katika ujifunzaji.
Hali
hii ya upungufu wa miundombinu, upatikanaji wa vitabu vinavyoendana na
mihtasari
iliyoboreshwa na kutokuwepo kwa chakula cha mchana ni changamoto
ambazo
zinaathiri utekelezaji wa mitaala shuleni.
Rasimu 2
xi
Mapendekezo
Kutokana
na taarifa za utafiti kuna mapungufu na changamoto mbalimbali zilizoathiri
kiwango
cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 mwaka 2010. Mapendekezo
muhimu
yametolewa ambayo yanaweza kutekelezwa kwa muda mfupi, kati na mrefu.
1.
Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,
uadilifu
na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na
zisikaimishwe
kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;
2.
Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,
tathmini
na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya
utoaji
wa elimu;
3.
Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili
kutatua
changamoto
zilizopo;
4.
Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)
kianzishwe
kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji
na
haki za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa
inakidhi
malengo yaliyokusudiwa; Utaratibu wa motisha kwa walimu
unaoendana
na uzito wa kazi, wadhifa na ugumu wa mazingira anapofanyia kazi
uandaliwe
na utekelezwe ipasavyo;
5.
Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya
mitihani
ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate sifa za kujiendeleza
kitaaluma
na kitaalamu;
6.
Vyuo vya ufundi stadi kama vile VETA vipanuliwe ili kuwawezesha wahitimu wa
kidato
cha 4 wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na
stadi
za kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri;
7.
Walimu wenye sifa wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji katika shule
zote.
Pia, Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule
ziandaliwe;
Rasimu 2
xii
8.
Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa
ufundishaji
na ujifunzaji yaimarishwe.
9.
Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo
vinavyotakiwa;
10.Walimu
wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia
pia
alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kama
ilivyoelekezwa
katika mwongozo wa mazoezi endelezi;
11.Utungaji
na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala
inayotekelezwa
12.Adhabu
katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III
baada
ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila
mtahiniwa
apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake;
13.Hadhi
ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja
wanafunzi.
Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada
(Remedial)
14.Mfumo
rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika
kwa
wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki
kwa
watahiniwa;
15.Wasahihishaji
wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu kwa sababu ni
haki
ya mwajiriwa wa serikali;
16.Mafunzo
kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa
kwa walimu na wakaguzi wote. Aidha Mafunzo maalumu kuhusu
dhana
ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na kutekelezwa kwa maafisa
mitaala
na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo;
17.Mihtasari
ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft
copy)
ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo
ya Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi;
Rasimu 2
xiii
18.Jukumu
la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili
kubaini
dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki;
19.Taratibu
za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya
utafiti,
tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake.
20.Fedha
za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia
shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo. Vilevile, Hosteli/mabweni na
nyumba
za walimu zijengwe kwenye shule za sekondari zilizo mbali na makazi
ya
watu, na wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha
mchana;
21.Sifa
za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada
zipandishwe
kuwa Principal mbili za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha
mwalimu
kuwa mahiri kitaaluma;
22.Vifaa
vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa
miundombinu
ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na
ongezo
la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa. Wakufunzi na wahadhiri
wapewe
mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi (Competence Based
Curriculum);
23.Maabara
ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na
kuimarishwa
katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali
watatumia
kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na
kuandika.
Pia Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa
walimu
wa masomo yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za
sekondari;
24.Utaratibu
maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post
Graduate
Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili
kukabiliana
na tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi;
25.Ukaguzi
wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa
kupatiwa
nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia;
Rasimu 2
xiv
26.Ufuatialiaji
wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada
pamoja
na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe;
27.Sheria
ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo
na
ithibati katika shule nchini.
No comments:
Post a Comment