Mbunge wa Viti maalum Chadema (Kwimba) Mh Leticia Nyerere
amefanya ziara ya kutembelea Ofisi za Bunge la Marekani mjini Washington DC
Ijumaa 15 Machi 2013. Lengo la ziara hiyo ya Mh Leticia Nyerere ni kutaka kujua
namna Mabunge mawili ya Marekani yanavyofanya kazi. Bunge la Marekani
limegawanyika katika sehemu kuu mbili yaani Bunge la wawakilishi (House of
Representative) na Bunge la Seneti (Senate). Katika ziara hiyo Mh Leticia
Nyerere alipokelewa na Mtaalamu wa kamati ya Bunge la Marekani anayeshughulikia
Mambo ya Nje Tamara Klajn.
Ikumbukwe katika
Mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Spika wa Bunge la Tanzania Mh Anna
Makinda alitoa maoni kwa kushauri katika Tume ya Katiba tuwe na Mfumo wa
Mabunge mawili yaani Bunge la wawakilishi na Bunge la seneti ili kuboresha
mfumo wa Uendeshaji wa Bunge la Tanzania.
No comments:
Post a Comment