Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kesho ataongoza maelfu ya wananchi katika uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki.Uzinduzi huo utafanyika mjini Shinyanga ambayo ni ngome kuu ya Chadema kwa ukanda huo.
Kanda ya Ziwa Mashariki inajumuisha mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu.
Uzinduzi huo utatanguliwa na maandamano makubwa yakifuatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara.
Leo Mbowe aliongoza viongozi zaidi ya mia mbili wanaounda Kanda hiyo kutoka majimbo yote katika kikao cha kupanga mikakati.
Mwenyekiti Mbowe kwa wiki zaidi ya tatu sasa amejichimbia mikoani katika kanda mbalimbali za Chadema akiwajengea uwezo viongozi wa ngazi za chini,akifungua mashina na ofisi za chama,akipokea maelfu ya wanachama wapya vijijini na akihutubia mikutano ya hadhara kutangaza sera za Chadema.
visit here and telllmwe what do you think (made in Tanzania-GO local) http://www.khmbuzz.blogspot.com/
ReplyDelete