Sunday, February 17, 2013

MAWAZO YA RAIA FULANI


Kuelekea 2015 hali ya hatari (State of Emergency) inatengenezwa.


Katikati hapa tutashuhudia mengi. Jakaya alishasema kuwa hawezi kuicha Tanzania ikaenda upinzani. Kwa gharama yoyote Tanzania itabakia chini ya ccm. Hizi chokochoko za kidini zimesababishwa na mwenendo wa kisiasa uliopo kwa sasa nchini. Ni hali ambayo inatishia usalama wa chama tawala na hivyo chama kubuni mbinu kadha wa kadha katika kuhakikisha tafrani inatokea na mwisho wa siku nchi haitawaliki kisha watangazae hali ya hatari ambayo itakuwa haina ukomo maalum.

Ndugu wanajamvi, zimejaribiwa mbinu nyingi sana katika kuhakikisha kuwa upinzani unadhoofika na ccm kuendelea kutamalaki lakini inakuwa kinyume chake. Kete pekee ambayo kwa sasa ccm wamebaki nayo ni UDINI. Propaganda za ukabila zimeshindwa. Za kikanda zimeshindwa. Za mauaji ya raia zimeshindwa. Kamwe uhasama wa kisiasa kati ya wafuasi wa ccm na chadema (upinzani) hauwezi kuleta mvurugano na hatimaye vita. 

Sasa tumeshuhudia kete ya udini ikishika kasi na matokeo yake tumeanza kuyaona. Uislam unaonekana kufanywa chombo cha maamuzi na ukristo chombo cha kupinga maamuzi hayo. Tumeshuhudia wakristo wakiwekwa kizuizini kisa wamechinja mfugo. Tumeshuhudia pia mchungaji akichinjwa kisa kutetea mkristo kuchinja mfugo. Tumeshuhudia viongozi wa kiserikali wakitoa matamko rasmi kuwa mwislam ndiye mwenye haki ya kuchinja. Tumeshuhudia mapadre wakipigwa risasi zanzibar hadi kufa. Serikali inafanya nini? Viongozi wa dini wanafanya nini.

Siku mkristo atakapoamua kumshughulikia mwislam ndio utakuwa utimilifu wa ndoto ya ccm kuamini kuendelea kutawala maana itakuwa ni wakati wa vita ya kidini nchini kuelekea uchaguzi mkuu. Jitihada nyingi zimetumika kuamsha hasira ya mkristo dhidi ya mwislam, na bila shaka zinaelekea kutimia.

Hatma ya Tanzania ipo chini ya Taasisi nne; wakristo, waislam, chadema, na ccm. Kati ya hizi nne, mbili (uislam na ccm) zimeonekana kushindwa kutimiza wajibu wao. Ukristo unalegalega kutoa misimamo thabiti kuhusu hali ya kisiasa na kiimani nchini. Chadema ni Taasisi mpya yenye lengo la kushika Dola. Dola ambayo ina majeraha ya kila aina yaliyosababishwa na ccm. 

Hali ya hatari ikitokea hapa kati, hakuna Taasisi yoyote kati ya hizo nne itakwepa lawama. Ukristo ukae na uislam na kuona ni jinsi gani majaraha haya yanatibiwa bila kuweka makovu. Chadema na ccm wamefikia pabaya zaidi hadi kufikia makada wao kutukana hali za viongozi waandamizi. Tusitukane wakunga uzazi ungalipo. Mwenye dhamana ya kuleta uelewano katika siasa ni ccm maana kwa kiasi kikubwa yeye ndiye chanzo cha vurugu zote hizi. Ccm inaleta ubabe kwenye mambo ya msingi sana, na cdm na wananchi hawawezi kuvumilia haya! Lenin aliwahi kusema, we have to make one step back in order to take two steps forward... Huu ni ujumbe wangu kwa ccm. Tuachieni nchi ikiwa salama. Nendeni Gethsemani mkajitafakari mmekosea wapi, inawezekana baada ya miaka kadhaa mbele mkagundua makosa yenu na mkajisahisha na mkapata tena ridhaa ya wananchi. Kwa sasa mnakotupeleka sio!
haya ni mawazo ya RF


chanzo JF

No comments:

Post a Comment