Ni kweli aliyosema Mhe. Rais Mstaafu ndugu Ben Mkapa kwamba harakati za maendeleo hazitakiwi kuwa siri.
Nami nashikilia papo hapo.
Ni kwa nini serikali imeshindwa kuweka wazi mikataba ya bomba la gesi na ujenzi wa nyumba za wanajeshi?
Ninashauri ndugu zangu Watanzania wote tudai uwazi wa mkataba wa gesi. Achilia mbali huo wa ujenzi wa nyumba za jeshi. Kwanza tuone huo wa ujenzi wa bomba la gesi.
Sidai watuletee wananchi wote tuuone, bali waukabidhi Bungeni kama walivyoomba Wabunge wapewe hiyo mikataba ipitiwe. Wabunge wameomba tangu mwaka jana wapewe huo mkataba lakini hadi sasa kumekuwa na kigugumizi. Sisi tumeshituka kwa kuona serikali imebana kuweka wazi mikataba. Kwani mikataba ya Tanzania huwekeshwa nje ya nchi kwamba tunapoihitaji atumwe mtu kuifuata Ulaya au Australia?
Haingii akilini kwamba gharama za ujenzi wa bomba ziko juu kuliko kujenga mtambo wa kusafisha gesi hapo hapo Mtwara.
Ni kwa nini Watanzania tumewaachia wananchi wa Kusini kulalamika peke yao bila kuwaunga mkono? Hata nyie wa Uchaggani, Tanga, Uhayani… mtafaidika tu hata kama gesi itabidi isindikwe huko huko iliko.
Ninashauri tena, Watanzania wote wa ndani na nje ya nchi tudai haki.
Tumechoka kuibiwa. Ingekuwepo sheria ya kuwataifisha walivyojilimbikizia huenda na wengine wangeogopa. Baya zaidi, wezi wa kodi zetu hata wakibainika wanaishia kufukuzwa au kusimamishwa kazi na mabilioni yetu wanaondoka nayo kuendeleza jeuri mtaani. Maana wanasema kwamba, “hata wakinifukuza nimeshachota changu nyie mlie tuu,” huo ndio usemi wa mafisadi wa Kitanzania. Huko tunakoelekea itafika wakati wananchi wenyewe wanachukuwa hatua ya kugawana mali za mafisadi; Na siyo mbali…
Chanzo - Wavuti
No comments:
Post a Comment