Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyombo vya ulinzi na usalama badala ya kutumia nguvu nyingi kupambana na chama hicho, mwaka huu kijielekeze kupambana na ufisadi na kutumia vizuri rasilimali za taifa ili kuchangia ukuzaji wa ajira nchini.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Taifa, John Mnyika, alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bavicha) Jimbo la Ubungo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo (Chadema) alisema nchi inakabiliwa na matatizo makubwa ya ukosefu wa ajira hususani kwa wanawake na vijana lakini hata hivyo CCM na Serikali yake wanaelekea kutotambua uzito wa matatizo hayo.
Alisema kumekuwa na propaganda zinazolenga kutisha umma hususani wanawake wasiunge mkono Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), kwa kueleza kuwa Chadema mwaka huu kimetangaza vurugu jambo ambalo siyo la kweli.
“Maana halisi ya falsafa ya Chadema ya ‘nguvu ya umma’ imeelezwa katika katiba ya chama ibara ya 3.A kwamba wananchi ndio msingi na chimbuko la kuundwa kwa dola ya nchi, na kuwa umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na mwisho katika kuamua hatma ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa,” alisema.
Mnyika alisema mwaka 2013 ni wakati muafaka wa kutumia falsafa ya ‘nguvu ya umma’ kuwezesha wananchi kuendeleza maamuzi na mawazo kuhusu rasilimali, uchumi na siasa za nchi.
Aliongeza kuwa maandamano ni moja kati ya mbinu nyingi halali za kidemokrasia za kusimamia uwajibikaji kwa ‘nguvu ya umma’
Alisema CCM imeshindwa kuwezesha maendeleo ya nchi sasa imehamia kwenye siasa chafu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment