Mkutano wa CHADEMA jimboni kisarawe umemalizika kwa mafanikio makubwa sana kuwaamsha wana Kisarawe sasa wamesema uonevu basi wako tayari kwa mabadiliko kwa kipindi cha miaka 52 wameishi katika umasikini wa kutisha sana sasa wamesema wanakiacha CCM na kila kitu chake leo tumepokea wanachama wapya 100 huku kina mama wengi wakionekana kuvutiwa naharakati zetu.
Mapambano ya leo yaliongozwa na makamu mwenyekiti wa chadema taifa kuwapa somo wana kisarawe kuhusu chadema,historia ya CHADEMA viongozi wake wa kwanza,pia alifuta propaganda zote za udini,ukanda na kuonyesha viongozi wachadema na maeneo waliyotoka kuondoa zana ya udini inayoenezwa na CCM.
Kwa taarifa mkuu wa wilaya ya Kisarawe ni mama Lyimo yule wa Igunga alifanya kila jinsi kuzuia mkutano wa leo lakini tulipata kibali na kuweza kuufanya huu mkutano tawi lililozinduliwa leo ndo lipo kwenye mgogoro kati ya mkurugenzi wa wilaya aliyetuandikia barua tulivunje eti lipo barabarani wakati la CCM limejenga ndani ya kituo cha kisarawe.
Kisarawe leo watu wameamka na kuonyeshwa kuwa uoga wao ndo utakao wamaliza wamepewa somo na makamo mwenyekiti jinsi ya wabunge wa CHADEMA wanavyopiga kazi kama kina Mnyika,Lissu,Mdee,Mbowe,Lema,Z itto na kiongozi wa chama Dr. Slaa.
Pia wamepewa somo kuhusu wanasheria makini wa CHADEMA kwenye kusimamia na kutetea haki kwamba CHADEMA sio chama cha fujo chini ya makamanda kina Lissu,Marando,prof. Safari walivyoweza kuibwaga CCM Igunga,Arusha na sehemu nyingine.
Wamepewa somo kuhusu hela za barabara ya shule zinavyoliwa barabara mbovu elimu yao bado ni duni watu wanaweka pesa zao mkunoni.
Pia wakapewa elimu kuhusu mfuko wa jimbo ambao mpaka sasa mh. mbunge Jaffo hajatolea mafafanuzi yake hizo pesa zimetumikaje hata kufanya mkutano mmoja.
Lakini mwisho tukawapa somo la umuhimu wa kujiandikisha na kuwa na kadi ya kupiga kura kumuondoa serikali dhalimu ya CCM kuanzia serikali za mitaa mwakani sema hapa hakuna kadi ya kupiga kura inayotumika lakini wameweka nia kweli mwakani tushinde chaguzi za serikali za mitaa.Pia waliambiwa kuhusu ufisadi wa CCM na viongozi wake.
Lakini tumetoa onyo yoyote atakaye shusha bendera ya chama kwenye tawi letu tutamstaki kwahiyo mkuu wa wilaya madiwani wa CCM wawe makini tutawafunga wakivunja sheria na mkurugenzi wa wilaya kama kiti kimemshinda aache aje kupiga siasa
No comments:
Post a Comment