MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh amependekeza Katiba Mpya itoe mamlaka kamili kwa ofisi yake ili iwe taasisi inayojitegemea ili itekeleze kazi zake kikamilifu.
CAG alisema hayo jana alipokuwa kitoa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kutoa mfano wa nchi zinazotumia mfumo wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu kuwa na mamlaka ya kuendesha mambo yake kwa uhuru ni Uganda na Afrika ya Kusini.
“Waajiriwa wa ofisi za umma wanachukuliwa kama waajiriwa wa Serikali. Sisi tumependekeza taasisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali iwe huru kama ilivyo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na isiwe na mwingiliano mwingine,’’ alipendekeza Utouh.
Kuhusu Mamlaka yake kuwa na uwezo wa kufungua kesi mahakamani pindi wanapobaini ubadhirifu au wizi katika ofisi za umma, CAG alisema kuwa mamlaka hayo wasipewe ila yaendelee kuwa mikononi mwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Alisema kuwa kinachotakiwa ni Katiba kujenga mazingira kwa vyombo hivyo kushirikiana ili utendaji wa kazi zao uwe na ufanisi hali ambayo itajenga uwajibikaji miongoni mwa taasisi hizo.
Alisema kuwa kinachotakiwa ni Katiba kujenga mazingira kwa vyombo hivyo kushirikiana ili utendaji wa kazi zao uwe na ufanisi hali ambayo itajenga uwajibikaji miongoni mwa taasisi hizo.
‘’Pia tungependa Katiba ijayo iwe na sheria ya kuzibana taasisi za watu binafsi zinazopata misamaha ya kodi kwa kuwa misamaha hiyo inainyima Serikali mapato na hata katika ripoti zetu huwa tunalizungumzia. Ingefaa sasa Katiba iweke mkazo zaidi,’’ alisema CAG.
Naye mwanasiasa mkongwe nchini na aliyewahi kuwa waziri katika Serikali ya awamu ya kwanza, Sir George Kahama jana alitoa maoni yake mbele ya Tume hiyo lakini hakuwa tayari kuzungumzia maoni hayo kwa waandishi wa habari kwa kuwa alishayawasilisha kwa Tume.

‘’Mimi ni mtu wa nidhamu, siwezi kuzungumzia mambo niliyoyatoa mbele ya Tume kwa vyombo vya habari. Asante sana,’’ alisema Mwanasiasa huyo na kuondoka kwenye viwanja vya Tume.
No comments:
Post a Comment