Mbunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, ameitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanyia marekebisho katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kwanza kabla ya kukamilika kwa zoezi la kupatikana kwa katiba mpya.
Mnyika, aliyasema hayo jana jijini hapa katika viwanja vya ofisi ya kata ya Makurumla, wakati akichangia maoni yake mbele ya Tume hiyo.
“Kwa sasa Tume hii ina mapungufu hivyo haitawezekana kupatikana kwa katiba mpya na bora yenye maoni waliyoyatoa wananchi ifikapo mwaka 2014, hivyo tume iandike marekebisho kuhusu tume ya uchaguzi ili iwe na mfumo huru kwa sababu ndiyo inayosimamia kura ya maoni,” alisema Mnyika.
Alifafanua kwa ufupi baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni Tume ya uchaguzi kuteuliwa na Rais bila kuwapo kwa mapendekezo kutoka kwa wadau pamoja na kuwatumia watumishi wa Serikali.
Aidha, Mnyika ameitaka katiba mpya isisitize kuwa Bunge ni chombo kikuu na chenye kujisimamia chenyewe katika kupandisha kodi, kutumia fedha pamoja na kupitisha bajeti bila kusimamiwa na Rais.
“Bunge limekuwa kibogoyo ambalo halina meno ikiwa namaanisha halina mamlaka kuhusu bajeti kwani haliwezi kukataa bajeti ya serikali kwa kuhofia kuvunjwa, hivyo Bunge lipewe uhuru kutoa maamuzi yake,” alisema Mnyika.
Aliendelea kwa kusema kuwa wananchi wapewe madaraka ya kumwadhibu diwani au mbunge kwa kumvua uongozi kwa kupiga kura ya maoni ya kutokuwa na imani na kiongozi huyo hata kama muda wa kutoka madarakani haujaisha.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment