Saturday, November 10, 2012

CHADEMA yavuna 17


WANACHAMA 174 kutoka vyama vya CCM, CUF na TLP wamevihama na kujiunga na Chama cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Mwibara.
Wanachama hao walijuinga na chama hicho jana na juzi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kijiji cha Kisorya na Kibara na kuendeshwa na viongozi wa juu toka mkoani Arusha.
Miongoni mwa waliojiunga ni pamoja na Mgaywa Toto ambaye mwaka juzi alikuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kupitia TLP, aliyesema kuwa ameamua kuachana na chama hicho baada ya kuona hakina mwelekeo.
Katika mkutano huo, wanachama 151 walikihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na CHADEMA ambapo walikabidhiwa kadi wakisema wamechoshwa na ulaghai wa chama hicho tawala.
Wanachama wengine 24 walitoka vyama vya TLP na CUF.
Awali, wakihutubia mkutano katika Kijiji cha Kibara, viongozi hao wa CHADEMA waliwataka wananchi wa jimbo hilo kufanya mabadiliko na kuacha kukichagua Chama Cha Mapinduzi ambacho kinawapa shida hadi sasa.
Lucas Webiro kutoka mkoani Arusha, alisema kuwa nchi hii imejaliwa rasilimali nyingi, lakini zimekuwa haziwanufaishi wananchi na badala yake vigogo wa CCM na watoto wao, na kuwaacha watoto wa walalahoi wakihangaika.
Naye Gabriel Lucas ambaye ni mwanachama wa chama hicho, alisema kuwa wananchi hawapaswi kuhangaika wakati nchi yao imejaliwa neema tele, ambazo sasa zinaliwa na wachache, na hivyo akawataka kuachana na kuendelea kuikumbatia CCM ambayo ndiyo imewafikisha hapa walipo.

Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment