YATANGAZA MKAKATI KUKABILI KASI YA M4C
CHAMa cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetawala mjadala wa mkutano mkuu wa nane wa Chama cha Mapinduzi (CCM), unaofanyika mjini hapa.
Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, mawaziri wa pande zote mbili za Muungano, viongozi wengine na baadhi ya wajumbe waliopata nafasi ya kuzungumza, walikuwa wakiilalamikia CHADEMA kwamba inaeneza uongo dhidi ya CCM.
Ingawa wazungumzaji wote, hawakutaja moja kwa moja jina la chama lengwa, ni dhahiri kwamba waliilenga CHADEMA, chama pekee kinachofanya ziara nyingi mikoani kupitia operesheni zake za Sangara na sasa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).
Aliyeibua mjadala wa CHADEMA kwenye mkutano mkuu huo wa CCM, alikuwa mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda, ambaye alialikwa kama mwakilishi wa Mpango wa Kujitathmini Kimaendeleo Afrika (APRM).
Shibuda akizungumza katika mkutano huo, aliishangaa CCM kwa kukaa kimya wakati CHADEMA inazunguka nchi nzima kuishambulia kwamba haifanya kitu.
Alisema ni makosa ya CCM kwani wajumbe hawafanyi mikutano ya hadhara kujibu mapigo ya CHADEMA.
“Mnasubiri viongozi wakija toka makao makuu ndipo mnajibu wakati wapinzani wanafanya mikutano, wananchi wanabaki na mihemko...na mnajua mtu akisema uongo mara saba wa sabini huwa ukweli...,” alisema Shibuda.
Huku akitumia misamiati migumu kama kawaida yake, Shibuda aliiambia CCM kuwa ndiyo daktari na wapinzani na maradhi, hivyo kila yanapotokea maradhi ni wajibu wao kuyatibu.
Kauli hiyo ya Shibuda ni kama iliiamsha usingizini CCM kwani Mwenyekiti wake, Rais Kikwete, mara kwa mara alirejea kauli ya Shibuda na kuwataka wajumbe waamke kujibu mapigo mara moja.
Rais Kikwete aliwataka wajumbe kutumia taarifa za utekelezaji zilizowasilishwa na baadhi ya mawaziri, kuwaeleza wananchi mambo yanayofanywa na CCM katika kutekeleza wajibu wao.
Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, aliwasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo iliainisha gharama, mahala ilipo na kasi ya ujenzi inavyoendelea.
Alieleza kuwa ujenzi wa daraja la Kigamboni, ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi, barabara za juu katika eneo la Tazara na miradi mingine ya ujenzi iko katika mikoa mingine nchini.
Baada ya kuwasilisha taarifa hizo, wajumbe walikusanyika katika makundi kuzijadili ambapo sehemu kubwa ya majadiliano, CHADEMA iliendelea kuwa gumzo kwa wajumbe.
Vikundi hivyo jana viliwasilisha taarifa za majadiliano hayo na kuwaeleza wajumbe namna ya kuzitumia kujibu mapigo ya CHADEMA.
Akieleza namna ya kufikisha taarifa hizo kwa wananchi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alieleza njia tatu za kufikisha ujumbe huo ili wananchi wajue ukweli.
Njia ya kwanza alisema ni kupitia vyombo vya habari vya chama na serikali, pili kuziweka kwenye CD, kutengenezea majirida maalumu kwa lengo la kufikisha taarifa hizo kwa wananchi.
Awali Pinda aliwasilisha taarifa ya serikali ya utekelezaji wa Ilani ya chama wakati Katibu Mkuu, Willson Mukama, aliwasilisha taarifa ya CCM.
Tanzania Daima
CCM NA JK WAZIVUNJA KATIBA ZA NCHI NA CCM. RAIA WA MAREKANI WAPIGA KURA DODOMA. MAJINA HAYA HAPA.
ReplyDeleteRAIA WA MAREKANI NA UINGEREZA WASHIRIKI MKUTANO WA CCM DODOMA, WATUMIWA NAULI KUSHIRIKI MKUTANO NA KUPIGA KURA. ZILITUMWA TICKETS 40 KWA MKOA WA DIASPORA, UINGEREZA, CHINA, INDIA MAREKANI N.K DMV TICKETS 8.
CCM na JK wazivunja katiba za nchi na chama. Mwenyekiti wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete na wanachama wa CCM wamewaruhusu RAIA wa MAREKANI na Uingereza kupiga kura DODOMA. CCM na uongozi wake vimekuwa vikilifumbia macho swala la uraia pacha, hapo hapo inawatumia raia wa nchi nyingine pesa za walipa kodi kwa ajili ya nauli ili wapate political points.
Kanuni za katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na ya CCM haziruhusu mtu mwenye uraia ambao sio wa Tanzania kushiriki shughuri za kisiasa nchini (HATUNA DUAL CITIZENSHIP). Hawa ni raia wa Marekani ambao wameshiriki uchaguzi DODOMA
-Phanuel Peter Ligate (USA citizen)
-Faraja Isingo (Raia wa kuzaliwa Marekani, alizaliwa Oklahoma)
-Maftah ambaye ni mwenyekiti wa New york CCM (USA citizen)
-Bashiri (Huyu ni Raia wa Uingereza na Burundi)
Kama hawa watu wanakanusha hili. Waonyeshe HATI zao za kusafilia na ziwe na STAMP ya entry na exit…Marekani na Tanzania
Hawa ni Green card holders sheria haiwabani
-Benjamini Mwaipaja
-Elizabeth Luhanga
-Loveness Mamuya (Huyu mara ya mwisho alikua anafanya process za uraia wa Marekani hatuna uhakika kafikia wapi)
TUNAWASHANGAA CMM NA JK WANAVYO ENDESHA MAMBO YAO YA KISIASA KWA KUWA FUMBA MACHO WANACHMA WAO NA WANACHI NA KUTUMIA PESA ZA WALIPA KODI KUWALIPIA NAULI RAIA WA NCHI ZA WATU.