Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepoteza mwelekeo na sasa linaonekana kama kituko kutokana na viongozi wake "kuwabeba" wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwabana wapinzani katika mijadala mbalimbali bungeni.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, katika tamko lililosomwa kwa niaba yake na Wakili Imelda Urio kutoka kituo hicho.
Dk. Bisimba alisema kwa sasa hakuna uwiano katika mijadala ya bajeti inayoendelea ndani ya Bunge mjini Dodoma kwa kuwa viongozi wanaowaogoza wabunge wameonekana wazi kufanya upendeleo kwa wabunge wa CCM.
Aliwataja viongozi hao kuwa Spika wa Bunge na Naibu wake pamoja na wenyeviti ambao wamepewa dhamana ya kuongoza vikao.
Aliwataka viongozi hao kubadili mitizamo yao ili kutoa fursa kwa wabunge kujadali kwa uwazi hoja kwa faida ya wananchi badala ya maslahi ya vyama vyao.
“Tunawataka wabunge watekeleze majukumu yao ipasavyo na kulirudishia heshima Bunge la 10 kama lilivyokuwa Bunge la Tisa, Bunge la sasa limepoteza mwelekeo na kuonekana kama kituko mbele ya jamii inayowaangalia,” alisema katika tamko hilo.
Aidha, LHRC kimewataka wabunge kuachana na utaratibu wa kutumia muda mwingi kutoa salaam pamoja na pole kwa kuwa jambo hilo ni kinyume cha kanuni namba 151(1)-(4).
Dk. Bisimba alisema kama kuna jambo la kutakiwa kutoa pole ama pongezi, Spika anaweza kufanya hivyo kwa niaba ya wabunge badala ya mbunge mmoja mmoja kufanya hivyo kiasi cha kutumia muda mwingi ambao angeutumia kutoa mchango wake katika mijadala.
Kasoro zingine zilizoainishwa katika tamko hilo la LHRC ni pamoja na wabunge kuendelea kutumia lugha za kuudhi, kuzomeana na kutaka miongozo bila sababu za msingi kinyume cha kanuni namba 64 (1) (g).
“Bado tunaona lugha za matusi na za kuudhi zikiendelea kutolewa na wabunge katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma na hili jambo linatakiwa kukomeshwa,” alisema.
Aidha, Dk. Bisimba alisema mahudhurio ya wabunge katika vikao vinavyoendelea bungeni ni hafifu na kwamba jambo hilo ni kinyume cha kanuni namba 143(1), na kwamba mara nyingi viti vimeonekana kuwa vitupu bila watu.
Jumatatu na Jumanne wiki hii hali ya hewa bungeni ilichafuka baada ya Mwenyekiti Sylvester Mabumba, kuonekana dhahiri akiyumba kwenye kiti wakati wa kikao cha Jumatatu jioni hali iliyozua msuguano mkali na baadhi ya wabunge.
Hali kama hiyo nusura itokee tena Jumanne katika kipindi cha baada ya maswali hadi mchana wakati wa mjadala wa makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment