MOTO uliowashwa bungeni
na wabunge kuibana serikali baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), sasa umewalazimu mawaziri wanane kutakiwa
kupima uzito wa makosa yao na kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kutakiwa
kung’oka.
Alhamisi
usiku, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alitoa wito kwa wabunge wote
kujiorodhesha kwa nia ya kupata saini za wabunge 71 ambao wangewasilisha
kutimiza matakwa ya kisheria kupata asilimia 20 ya wabunge kwa ajili ya
kumuondoa Waziri Mkuu.
Mawaziri
ambao usiku huu tayari wamejipinda kumuandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kwa
ushauri wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuikoa serikali ya chama hicho isianguke
kutokana na mpango wa wabunge kujirodhesha kutaka kumuondoa Waziri Mkuu,Mizengo
Pinda.
Wanaotakiwa
kuondoka ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara,
Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi,
Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika,
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk.
Haji Mponda.
Hata hivyo, baadhi ya Mawaziri hao, wameelezea kuwa wataandika barua kwa Rais
Kikwete kuelezea uozo wote uliosababisha kusakamwa kwao, baadhi wakidai kwamba
hawahusiki kwa lolote na mambo wanayotuhumiwa nayo, huku baadhi wakiona mambo
ni mazito na kuamua kujiondoa usiku huu.
Katibu wa Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao ambacho kimewashauri mawaziri wanane kujiuzulu.
Chanzo - Fikra Pevu


No comments:
Post a Comment