Kwa kweli inasikitisha sana kuona ujenzi wa majumba makubwa ndani ya mbuga unaendelea kila kukicha kwa kisingizio eti ni uboreshaji wa sekta ya utalii.Unajua Tanzania tunacheza makida kwa kuchezea hii resources ya wanyama wa porini.Kunatakiwa kuwepo na plan maalum ya ujenzi wa mahoteli.Tusugue vichwa wapi mahoteli yajengwe na yawe kwa ktk mandhari gani?.Kwani tunatambua kuwa tumeingia kwenye mji wa wanyama. Na wao hawataki disturbance kama wewe husivyotaka. Sasa kwa upeo wangu mimi naona kuwa ujenzi uyoga ni hatari kwa uchumi endelevu wa nchi yetu, kwani unarahisha kukamatika kwa wanyama wengine kwa urahisi zaidi [predator]. Sasa hivi ujenzi ufanywa katika zile sehemu ambazo ni mapito kila mara. Majengo yanawatisha wanyama na kuwafanya wabadili njia na kupita sehemu ambazo ni hatari kwao. Kwani kuna maadui wa wanyama wengine wanaua for fun, na sio kwa ajili ya chakula. Watanzania inabidi tutambue kuwa kuna maadui wengi wa wanyama wetu wa porini.1 .Ongezeko la joto na badiliko la hali ya hewa duniani, hakuna mvua, hakuna chakula, hakuna maji. 2.majangiri[poachers] Ujenzi holela wa mahoteli ndani ya mbuga,3.Wanyama kuuana wenyewe kwa wenyewe. 4. Kuwinda wanyama [professional hunter] 5.Kuuza wanyama nje ya nchi. Watanzania hatupo tayari kuona kuna mji mpya umeanzishwa kimakosa ndani ya mbuga [eksidento city], na wakati tunaangalia. Imefika wakati sasa wa kusimama pale tunaona uchumi wetu wa sasa na wa vizazi vijavyo unaharibiwa na watu sio kwamba hawajui, hapana wanajua ila ni kwa sababu ya ulafi wao na tamaa kupata leo na kuharibu baadae. Imenisikitisha nilikwenda kwenye mji mmoja hapa USA, nikaona hawa jamaa zetu wana mazoo ya ajabu na wanyama. Na wanatoza dollar nyingi tu. Sasa Naomba niulize kweli watalii wataweza kuja hapa Tanzania kutalii??.Naomba angalii kwenye website hii hapa www.sdzsafaripark.org . Muda umefika wewe Mtanzania kusema" We deserve better ".Tunataka tuwe na green sustainable economy ili watoto wetu nao wasiangaike. MUNGU IBARIKI TANZANIA
Ludigo Mhagama[enviromentalist]
lmhagama@yahoo.co.uk
202 367 2761
No comments:
Post a Comment