TAARIFA KWA UMMA – KUUNGA MKONO MAANDAMANO YA TAREHE 25 MACHI 2013
Kufuatia tamko lililotolewa jana tarehe 11 Machi 2013
huko musoma na Mwenyekiti wa chama Mhe Freeman A. MBowe (MB), ambalo ni
msisitizo wa tamko lililotolewa wiki kadhaa zilizopita huko mbeya la azimio la
kutaka waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi na naibu wake kuwajibika
kufuatia matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha NNE, CHADEMA kanda ya
Kaskazini inaunga kwa mkono tamko hilo ambalo limebeba utashi wa wananchi ambao
ni wazazi wa vijana wetu ambao kwa sababu ya mfumo mbovu wa elimu, umeendelea
kupelekea matokeo kuwa mabaya na hasa ya mwaka na yenye kuleta fedheha na kilio
kikubwa sana kwa taifa letu. Ieleweke kuwa hili ni janga na serikali kwa
ukiziwi wake wa kutosikiliza sauti za watu itajikuta ikiingia kwenye gharama
kubwa ya kukabiliana na kundi kubwa la vijana waliopo mtaani ambao hawana jambo
la kufanya kwa sababu mfumo wa elimu umewafanya kuwa washindwaji kwa kiwango
ambacho hawataweza kujimudu kimaisha.
Hili si jambo dogo hata kidogo, tafsiri ya matokeo mabaya
haya inawalenga moja kwa moja mawaziri wenye dhamana na pasifanyike masihara
wala mizaha kuhusu jambo hili la kufeli huku kwa vijana wetu. Kauli zao za
awali zimeonyesha wao kutojali na kulitia umaanani kwa kutoa vijisababu visivyo
na mashiko wakati wao ndio wenye dhamana. Ni dhahiri kuwa takwimu za elimu
zimeshuka kutoka aslimia 89.3 ya mwaka 2005 hadi kufika asilimia 34.5 kwa
mahesabu haya kiwango cha elimu kimeporomoka kwa asilimia 54.8 (Chanzo: Hotuba ya Waziri Mkuu akizungumza na
waandishi wa habari tarehe 2 Machi 2013). Takwimu hii inazungumza mambo
mengi, maana yake ni kuwa mfumo mbovu unaosimamiwa na Chama Chama Mapinduzi kwa
asilimia hii 54.8 ya vijana wetu watakuwa wamewezeshwa tu kujua kusoma kwa
mashaka, kuandika na kuhesabu kwa shida kitu ambacho hakitawasaidia kupambana
na changamoto za kimaisha iwapo hawataweza kupata fursa za kujiendeleza kwa
ziada. Hili ni janga kubwa na wahusika ni lazima wawajibike maana ni dhahiri
kwa mfufulizo wa kuporomoka huku ni dhahiri wameshindwa kusimamia elimu ya
Tanzania.
CHADEMA kanda ya kaskazini, tunawaalika wazazi wote na
vijana wetu wote ambao wamekuwa wahanga wa matikeo haya mabovu siku ya tarehe
25 Machi 2013 kushiriki katika maandamano haya ya kushinikiza kuwajibika kwa
waziri elimu na mafunzo ya ufundi stadi na naibu wake. Zaida ya hapo ni kuitaka
pia serikali kufanya utaratibu wa kuwajibika kuwasaidia vijana hawa katika
kushughulikia janga hili. Aidha katika kuanzisha vituo vya masomo kuwawezesha
kusoma ili kurudia mitihani au lolote litakaloonekana lenye msaada. Maamuzi
mabaya ya hamaki na yasiyo ya kujali katika jambo hili yataweza kuzaa kizazi
kibovu ambacho kitakuwa ni mavuno ya matunda ya maamuzi yetu yasiyoonyesha
utashi wa kujali ya sasa.
Nawaomba wazazi wote katoka mikoa ya Tanga, Kilmanjaro,
Arusha na Manyara wafike katika ofisi za chama za wilaya zilizopo katika mikoa
yao au ofisi za wabunge (CHADEMA) kuandikisha majina yao na ya watoto wao ili
kupata idadi kamili. Siku ya tarehe 25 Machi kuanzia SAA NNE asubuhi kuanzia
mahali ambao tutawajulisha kutakuwa na maandamano makubwa katika JIJI la Arusha
yatakayokuwa na ujumbe huu na yatawashirikisha viongozi wote wa chama, wabunge
wote kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, wadau wa elimu, taasisi zisizo za
kiserikali zenye kujishughulisha na masuala ya elimu pamoja na watanzania wote
ambao kwa dhati ya moyo wameguswa na matokeo haya mabaya ya elimu, wazazi na
vijana wote waliopatwa na janga hili.
Taarifa nyingine zitawajia kama ambavyo tutawajulisha
kupitia vyombo vya habari na ofisi za wabunge na makatibu wa majimbo.
Niwaombe
Watanzania wote wakazi wa kanda ya Kaskazini tujitokeze kwa wingi katika
maandamano haya ya AMANI yatakayofanyaika katika JIJI la Arusha na tuonyeshe
Utanzania wetu na tuonyeshe kuwajali watoto wetu.
SIKU YA
MAANDAMANO NJOO NA KITAMBAA CHEUPE MKONONI.
Imetolewa leo
tarehe 12 Machi 2013.
Ofisi ya Kanda
ya Kaskazini
Amani Golugwa
Katibu – Kanda
ya Kaskazini
+255 754 912 914
golugwa@gmail.com
No comments:
Post a Comment