Tuesday, March 5, 2013

Mnyika kumvaa Prof. Maghembe


BAADA ya Bunge kuitupa hoja binafsi ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), sasa amepanga kufanya maandamano ya wananchi wa Jiji la Dar es Saalam Machi 16 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mnyika alisema maandamano hayo yataanza saa tano asubuhi eneo la Bakhresa, kata ya Manzese, hadi Wizara ya Maji Ubungo.
Alisema maandamano hayo yatakuwa ya amani ambayo yatapita barabara ya Morogoro hadi wizarani hapo, huku akidai ametoa taarifa mapema kwa wapenda haki kushiriki.
Mbunge huyo alisema lengo hasa ni kupata majibu ya hatua za haraka ambazo serikali itazichukua kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya upatikanaji wa maji safi na uondoaji wa maji taka.
Alisema katika maandamano hayo wananchi watapata majibu kutoka kwa Waziri Maghembe ambaye aliahidi kuwa Februari 20 mwaka huu, maji yangeweza kutoka.
Mnyika alisema maneno hayo waliambiwa wananchi wa kata ya Goba, Februari 17, mwaka huu, na Maghembe alipofanya mkutano wa hadhara lakini hadi sasa hakuna maji.
Alisema kwa kuwa anawafahamu watumishi wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) na Kampuni ya Maji Safi na Taka (Dawasa) wanaohusika na wizi wa maji sasa tunataka awataje siku hiyo.

No comments:

Post a Comment