Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, amesema wimbi la vijana wa CCM kukikimbia na kujiunga na Chadema ni dalili mbaya na kukitaka chama hicho kuwavua magamba wanachama wao wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya ufisadi badala ya kusubiri wajivue wenyewe.
Dk. Bana, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam pembeni mwa mkutano wa mtengamano wa kisiasa wa Afrika Mashariki.
Alisema kuna watu wengi wanaotaka kukihama CCM na kujiunga na Chadema hivi sasa, lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na ugumu wa mioyo yao kisiasa.
“CCM isisubiri wanachama wao wenyewe kujivua gamba na kisha vigogo kuanza kusema kwamba watu wa aina hiyo walikuwa hawawahitaji badala yake chama kiwavue kabla,” alisema Dk. Bana.
Alifafanua kuwa wimbi hilo la vijana pamoja na watu wengine kutamani kuhama CCM na kujiunga na Chadema linatokana na chama hicho cha upinzani kwa sasa kuonekana kuwa na mvuto.
Aliongeza kuwa ni vigumu kwa baadhi ya wanachama wa CCM kukubali ukweli huo kwamba Chadema kina mvuto, lakini alisema watu wenye akili ndani ya CCM wanaijua dhana hiyo.
“Watu wenye akili ndani ya CCM wanajua Chadema kina mvuto na hili wimbi la vijana na watu wengine kukihama CCM siyo dalili nzuri hususani utakapofika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema.
Alisema Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ulidhihirisha kwamba Chadema kilipata mvuto mkubwa kwa wananchi baada ya kuibuka na ushindi katika majimbo mbalimbali na kuongeza idadi ya wabunge wake.
“Mwaka 1995 hadi mwaka 2000 wanachama wa upinzani walikuwa wanahama katika vyama vyao na kujiunga na CCM, lakini hivi sasa upepo umebadilika ambapo sasa wanahama kutoka CCM na kwenda Chadema, hii ni dalili kwamba wanakiona kama chama mbadala,” alisema.
CHANZO - Gazeti la Nipashe.
Friday, April 20, 2012
Thursday, April 19, 2012
Wanachama 2402 wa CCM Ngorongoro wakiwemo viongozi watimukia CHADEMA
Wanachama wa ccm wakiwemo wenyeviti wa vitongoji vitano wilayani ngorongoro, wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na chadema,na tayari wamebwaga kadi zao za ccm katika ofisi za chadema zilizopo wilayani humo na kukabidhiwa za chadema.
Tarifa hiyo imetolewa na katibu wa ccm mkoa wa Arusha Amani Golugwa.
Kwamujibu wa katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa, Wenyeviti haowalipiga simu asubuhi ya leo na kutoa taarifa za kuhama CCM. Chadema ilituma KikosiKazi ili kuthibitisha habari hizo na tayari imethibitishwa wanachama hao kuhamaCCM na Kuhamia CHADEMA kama inavyoainishwa hapa chini;
1. Saitabau Tereto - Mwenyekiti waCCM Kitongoji cha Esirwai,
Amerudisha Kadi yake na kuhamia Chadema,
Wanachama wengine 478 waCCM katika Kitongoji hiki wamerudisha KADI zao na kuhamia Chadema.
2. Kone Kema - Mwenyekiti wa CCM Kitongojicha Ndiyani,
AmerudishaKkadi na Kuhamia Chadema,
WanachamaWengine 590 (CCM) katika kitongoji hiki wamerudisha Kadi na kuhamia Chadema
3. Marko Mbene – Mwenyekiti wa CCM Kitongojicha Ngoyapase,
Amerudisha Kadi na kuhamia Chadema,
Wanachama wengine 320 katika Kitongoji hiki wamerudishaKadi na kuhamia CHADEMA
4. Saruni Meng'arana – Mwenyekiti wa CCM Kitongojicha Embarware –
Amerudisha kadi na Kuhamia Chadema,
Wanachama wengine 224 katika Kitongoji hikiwamerudisha Kadi zao za CCM na kuhamia CHADEMA
5. RobertEdward – Mwenyekiti wa CCM Kitongoji cha Madukani
Amerudisha Kadi na kuhamia Chadema,
Wanachama wengine 326 wa CCM katikakitongoji hiki wamerudisha Kadi na kuhamia CHADEMA
CHANZO Arusha Mambo

Diwani mwingine (CCM Mwanza) ahamia CHADEMA
UPEPO mbaya unaonekana kukikumba Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa viongozi wake kukihama chama hicho, umeingia katika Mkoa wa Mwanza, ambapo Diwani wa Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema mkoani hapa, Hamis Mwangao Tabasamu ametangaza kuihama CCM na kujiunga na Chadema.
Diwani huyo ambaye amejipambanua kwa kupiga vita ufisadi ndani ya wilaya hiyo, ametangaza azma yake hiyo katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika Ryan's hoteli, na kupokelewa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema).
Diwani Tabasamu ambaye jumamosi amepanga kuhudhuria na kuhutubia mkutano mkubwa utakaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kata ya Nyampulukano, amekuwa ni miongoni mwa viongozi wengine wa CCM kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema ndani ya muda wa wiki moja.
Hivi karibuni, aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mkoa wa Arusha, James Milya alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote kisha kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Mbali na Milya, viongozi wengine kadhaa akiwemo diwani wa Kata ya Sombetini mkoani Arusha, Alphonce Mawazo (CCM), juzi alikihama chama chake hicho kisha kujiunga na Chadema, chama ambacho kinaonekana kuiweka pabaya CCM na Serikali yake kwa ujumla.
Akizungumza mchana huu wa leo, katika kikao chake na waandishi mbele ya Lema ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, diwani Tabasamu ambaye aliwahi kuibua tuhuma za ufisadi katika halmashauri ya Wilaya ya Sengerema alisema: "Kuanzia leo (jana), natangaza rasmi kukuhama CCM na kujiunga na Chadema".
Alisema, lengo lake la kuhama kutoka ndani ya CCM si la kushawishiwa na mtu ama kiongozi yeyote, bali ni dhamira yake ya kweli kama Mtanzania halisi mwenye uhuru wa mawazo, na kwamba amechoshwa na siasa za 'majitaka' ndani ya CCM.
Kwa mujibu wa diwani huyo wa Nyampulukano wilayani Sengerema, kuondoka kwake CCM inatokana na kushindwa kuafikiana katika maslahi ya wananchi, ambapo alidai wapo baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo wanakumbatia vitendo vya kifisadi.
"Uamuzi wangu huu wa kuhamia Chadema kutoka CCM unatokana na kushindwa
kuafikiana katika mambo yanayogusa maslahi ya wananchi katika
halmashauri ya wilaya ya Sengerema.
"Mafisadi wameliteka baraza la Madiwani la Sengerema!. Kwa maana hiyo natangaza rasmi leo, najiuzulu nafasi zangu zote ndani ya CCM, na nahamia Chadema", alisema Tabasamu ambaye amewahi kuingia mgogoro na mkuu wa wilaya hiyo, Elinas Palagyo kwa kile kinachodaiwa msimamo wake wa kupiga vita ufisadi.
Alizitaja sababu nne za kuhama ndani ya chama hicho tawala kuwa ni pamoja na kuwepo kwa madiwani wengi wa CCM wasio wazalendo kwa kuruhusu kuhamishwa mnada wa ng'ombe kutoka Kijiji cha Ibondo Nyampulukano kisha kuhamishiwa Kata ya Sima.
Sababu nyingine ni ucheleweshaji wa makusudi kuunda halmashauri ya mji
wa Sengerema kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka huu, kupunguzwa kwa mipaka ya mji mdogo bila kufuata vikao halali vya kisheria.
Nyingine ni halmashauri ya wilaya hiyo ya Sengerema, iliyopo chini ya uenyekiti wake, Mathew Lubongeja (CCM), kushindwa kuwachukulia hatua watu aliowaita wezi waliotajwa na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), PPRA, ambapo alidai maelekezo ya CAG kuhusu kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa ufisadi kutotekelezwa hadi leo.
Awali, akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari, Lema alimpongeza diwani huyo wa Nyampulukano kwa kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na Chadema, na alisema huo ni uamuzi sahihi na wa kijasiri unaolenga kuikomboa nchi hii kutoka CCM.
"Nakupongeza sana mheshimiwa Tabasamu kwa kuondoka CCM na kuja Chadema chama makini. Nawaomba sana na madiwani, wabunge na viongozi wengine wa CCM wawahi kujiunga na Chadema kabla safina haijafungwa", alisema Lema.
Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma - FikraPevu.com, Mwanza
CHANZO JF

CCM itaanguka 2015 - Mbunge
KATIKA hatua isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kuanguka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ubadhilifu wa mali ya umma serikalini.
Zambi alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa anashangaa kwa nini Waziri Mkulo bado yuko ofisini licha ya tuhuma nzito zinazomkabili.
Zambi aliyekuwa akichangia hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, alisema ubadhirifu wa kutisha uliofanywa na Wizara ya Fedha na taasisi nyingine za serikali unakiweka rehani chama hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao na akadai hatashangaa kikishindwa.
Kauli ya mbunge huyo ilionekana kuwashitua baadhi ya wabunge wa CCM, lakini ikapokewa kwa shangwe kubwa na wabunge wa upinzani.
Zambi aliungana na Mbunge mpya wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ambaye alionesha kushangazwa kwake na utendaji wa serikali ambayo imekaa kimya ikiwaachia mafisadi kupora mali ya umma bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.
Mbunge huyo alidai kuwa ni jambo la kushangaza kuwa hadi sasa Waziri Mkulo bado yuko ofisini pamoja na tuhuma nzito zinazomkabili.
Akizungumza kwa kujiamini, Zambi alisema Wizara ya Fedha inanuka ubadhirifu na kutaja hatua ya Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali kutumia kiasi cha sh bilioni 49 bila kuwepo kwa maelezo ya kueleweka.
Mkulo ambaye jana aliwashangaza wabunge baada ya kushindwa kuhudhuria kikao cha Bunge cha jioni, huku akitambua kuwa hoja iliyokuwa ikijadiliwa inamhusu, alianza kushambuliwa kwa tuhuma nzito za kulihujumu Shirika Hodhi la Mali ya Umma (CHC) kwa masilahi yake binafsi.
Mbunge wa Mwibara, Kange Lugora (CCM), akichangia taarifa za Kamati ya Bunge inayosimamia fedha za umma alimtuhumu Waziri Mkulo kwa kuingilia utendaji wa shirika hilo kwa masilahi yake binafsi.
“Waziri Mkulo aliingilia CHC katika uuzaji wa Plot namba 10 ya Mohamed Enterprises. Mkurungenzi wa CHC alikataa. Pia aliingilia uuzaji wa Tanzania Motors Company kwa Murad Sadic lililokuwa liuzwe kwa sh bil. 3.9, Katibu Mkuu, Ramadhani Kijjah alifanya mazungumzo na kuidhinisha malipo kwa sh milioni 900,” alisema mbunge huyo.
Aliongeza kuwa kutokana na ubadhirifu huo, Mkulo aliwasilisha azimio bungeni la kutaka shirika hilo kufutwa, ili kuficha madhambi aliyoyafanya.
“Alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa CHC na kuvunja bodi ili kuficha madhambi aliyofanya na kisha kurudi bungeni na kusema wabunge wanaoitetea CHC wamehongwa.
“Zitto aliweka rehani ubunge wake na kumtaka Mkulo kuthibitisha madai hayo na kumtaka naye kuweka rehani uwaziri wake. Namtaka Waziri Mkulo afute hoja hiyo na kumsafisha Zitto,” alisema na kuongeza kuwa Wizara ya Fedha inaangamiza nchi.
Zitto, Nyerere wailipua TANESCO, TBS
Wabunge, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini - CHADEMA) na Vincent Nyerere (Musoma Mjini - CHADEMA), jana waliwalipua watendaji wa mashirika mawili ya umma kwa tuhuma nzito za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za Kitanzania.
Ufisadi huo uliibuliwa jana na Zitto wakati alipokuwa akiwasilisha taarira ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2010 ambapo alisema kuwa katika hali ya kushangaza, watendaji wa TANESCO walifanya manunuzi ya sh bilioni 600 kinyume cha sheria.
Zitto alisema fedha zilizotumiwa na shirika hilo ni nyingi, hivyo, ametaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya TANESCO na mashirika mengine yaliyolisababishia taifa hasara kubwa.
“Mifano ya wazi kuhusu upotevu wa fedha za umma kutokana ama na kutozingatiwa kwa sheria za manunuzi ya umma inaweza kuelezwa kwa ufasaha katika mashirika mengi yaliyojihusisha na vitendo hivyo,” alisema.
Mbali na kulishukia shirika hilo la umeme nchini, Zitto na kamati yake imeagiza kuwakamata na kuwafikisha mahakamani maofisa wa serikali walioingia mkataba wa ukodishaji wa ndege ya ATCL, Air Bus 420-214, mwaka 2007.
Zitto alisema ukodishaji huo wa ndege ni wa kutatanisha na uliojaa upungufu mkubwa ambao utaitia serikali hasara kubwa.
Alisema kamati ilibaini kuwa maofisa kadhaa wa shirika na serikali waliingia katika mkataba wa kukodisha ndege huku wakijua kuwa ingehitajika kwenda katika matengenezo nchini Ufaransa baada ya muda mfupi tangu itakapoanza kazi.
Alisema utata mwingine ni namna dhamana ya serikali ilivyotolewa, akibainisha kuwa Msajili wa Hazina kwa niaba ya serikali alitoa dhamana kwa ATCL mwaka 2007, ili ikodi ndege aina ya Air Bus 420-214 kutoka Kampuni ya Wallis Trading ya Lebanon kwa muda wa miaka sita, wakati dhamana ilitolewa mwaka uliofuata.
“Kamati ilikagua na kujiridhisha namna mchakato huo ulivyofanywa na kubaini mapungufu makubwa kuwa ukodishaji wa ndege hiyo ulifanywa Oktoba, 2007, wakati dhamana ya serikali kwa ATCL ilitolewa Aprili, 2008,” alisema.
Alisema ni wazi ndege hiyo ilikodiwa kabla ya kutolewa dhamana ya serikali wakati ni kinyume cha sheria inayosimamia utoaji wa dhamana za mikopo serikalini.
“Mkataba uliingiwa kinyume na ushauri wa wataalamu ambao katika taarifa yao walisema si sahihi kukodi ndege ambayo baada ya miezi sita itatakiwa kwenda Ufaransa kwa matengenezo makubwa, kamati ilibaini kuwa walioingia mkataba huo walijua ndege hiyo italazimika kufanyiwa matengenezo,” alisema.
Nyerere afichua madudu mengine ya TBS
Kwa upande wake, Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), ameibua ufisadi mwingine mzito unaodaiwa kufanyika katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Akiuliza swali bungeni jana, Nyerere aliibua na tuhuma nzito akidai kuwa baadhi ya vigogo wa serikali na wale wa TBS wana uhusiano na kampuni saba zinazofanya ukaguzi wa magari nchini.
Alisema anao ushahidi wa kutosha na yupo tayari kuutoa iwapo wahusika watakuwa tayari kujiuzulu.
Nyerere ambaye kauli yake ilizua hali ya kutotulia kwa baadhi ya watendaji wa serikali, baadaye alizitaja kampuni hizo kuwa ni JK Jabal Kilimanjaro (Sharjah UAE), WTN-Utility Service ya UK, EAA ya Japan, Total Automative-Dubai UAE, Quality Garage-Hong Kong na Sime Darby-Hong Kong.
Alisema Septemba 25, 2007, vigogo hao wa serikali walifanya kikao katika hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam na kugawana kampuni bila kuzingatia sheria ya manunuzi ya mwaka 2004.
Shutuma hizo zilisababisha mawaziri wa viwanda kujichanganya katika majibu yao, kiasi cha kumlazimisha Mbunge wa Mwibara, Kange Lugora (CCM) kutaka mwongozo wa Spika.
Lugora alifanya hivyo, baada ya jibu la Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu aliyedai kuwa ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu suala hilo ipo wizarani na wahusika watachukuliwa hatua.
Wakati akijibu hivyo, juzi Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami aliliambia Bunge kuwa ripoti hiyo ilikuwa bado haijakamilika.
“Juzi Waziri wa Viwanda alipokuwa akijibu swali linalofanana na hilo alisema bado ripoti haijakamilika, lakini leo Naibu Waziri, Lazaro Nyarandu anasema kuwa ripoti hiyo imeshatoka. Sasa hapa nashindwa kuelewa kati ya Waziri na Naibu Waziri nani anasema kweli?” alihoji Lugora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema Ofisi ya Waziri Mkuu itakusanya maelezo yote kuhusiana na suala hilo na baadaye kutoa taarifa bungeni.
“Tunaomba kupatiwa muda ili tuweze kukusanya maelezo yote na baadaye tutatoa taarifa bungeni,” alisema.
Hata hivyo, majibu ya mawaziri hao yalizidi kuwakoroga wabunge, ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alisema suala hilo liliundiwa kamati maalumu na kulifanyia kazi kwa miezi minane.
“Tumeshakamilisha kazi hiyo na tumekabidhi taarifa kwa Spika ambaye pia amekabidhi ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu. Tunachosubiri ni kwa serikali kutoa taarifa ya utekelezaji wa suala hilo ili liweze kumalizika,” alisema Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Chami, Nyalandu wahaha
Majibu ya Zitto yalionekana kuwasha moto kwa wabunge wengi, ambapo baada ya kauli hiyo, Waziri Chami aliitwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alizungumza naye kwa takriban dakika saba huku Bunge likiwa linaendelea.
Wakati hayo yakiendelea Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) alionekana akiteta na Lugora ambaye ndiye aliyeibua mjadala huo, kabla ya kwenda kwa Waziri Nyalandu na kuteta naye kwa dakika kadhaa.
Vincent Nyerere naye aliinuka na kwenda kwa Waziri Lukuvi na kuzungumza naye kwa muda.
Lugora kwa upande wake alieleza kushangazwa kuendelea kuwapo kwa shirika hilo huku bidhaa zilizopo chini ya kiwango kuendelea kuingizwa nchini.
“TBS mnasubiri nini? Watanzania wanakufa kutokana na kuingizwa kwa matairi yasiyo ya viwango, mafuta yanachakachuliwa, inawezekana hata ile ndege ya ATC iliyoanguka ilitokana na mafuta kuchakachuliwa. Mungu atuepushe na ndege ya rais isije ikawekwa mafuta ya kuchakachuliwa,” alisema.
Aidha, alisema walikwenda Hong Kong kukagua kampuni zinazodaiwa kukagua magari kabla ya kuingizwa nchini, lakini kampuni hizo zilikuwa hewa.
Alisema katika wizara hiyo wabunge wa kamati ya Bunge walitumia fedha za umma na kusema kuwa alikasirika na kutamani kumpiga ngumi Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege.
“Vitendo vya Wizara ya Viwanda na Biashara vinaonyesha kumlinda Ekelege. Alikiri kutudanganya kuwapo kwa kampuni hizo Hong Kong, lakini hakuna hatua zozote alizochukuliwa,” alisema.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo, alisema kamati hiyo imebaini Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kutumia sh bilioni 1.1 katika maonyesho ya kimataifa kama Nanenane, Sabasaba na Utumishi.
Alisema fedha hizo zilitumika katika mwaka 2009/2010 na kwamba matumizi hayo hayakuwapo katika bajeti iliyopitishwa na serikali.
Joshua Nassari anguruma
Naye Mbunge mpya wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) jana alimshambulia Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kwa kuondoka bungeni wakati wa mjadala mzito wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Akichangia kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake, Nassari akionekana kutokuwa mgeni kabisa na vikao vya Bunge, alisema Waziri Mkulo ameonesha kutojali mambo mazito ya ubadhirifu wa fedha na ndiyo maana hakuwa ndani ya Bunge, lakini juzi wakati wa kuchagua wabunge wa Afrika Mashariki alikuwapo.
Nassari ambaye kwanza alimshukuru Mungu kwa kumjalia kuwemo katika Bunge hilo, aliianika serikali alipodai kuwa inamiliki magari yenye thamani ya sh trilioni tano, huku ikishindwa kununua magari ya wagonjwa katika hospitali zake.
Alisema kuwa katika kilele cha ubadhirifu, baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa wakipandisha bei ya manunuzi ya magari hayo huko Japan, kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya bei anayonunua mtu binafsi na ile ya serikali.
Mdee ataka Chavda akamatwe
Akichangia ripoti hiyo, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (CHADEMA) aliitaka serikali kumkamata na kumfikisha mahakamani, mfanyabiashara aliyemtaja kwa jina moja la Chavda anayetuhumiwa kuchota fedha benki kwa kuweka dhamana mashamba aliyokodishwa na serikali na kisha kuyatelekeza.
Akizungumza kwa uchungu, Mdee alisema kuwa mawaziri wengi wamekuwa wakifanya uzembe wakijua kuwa hakuna hatua zozote watakazochukuliwa.
Aliwataka wabunge bila kujali itikadi za kisiasa kuchukua hatua za kinidhamu na kuwawajibisha mawaziri wote ambao wamefanya uzembe uliosababisha taifa kuingia katika hasara kubwa. Mjadala kuhusiana na ripoti hiyo unatarajiwa kuhitimishwa leo.
CHANZO - Gazeti la Tanzania Daima
CHADEMA kuzoa vigogo CCM
WIMBI la viongozi na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutimkia upinzani, limeanza kushika kasi baada ya jana diwani mmoja na katibu mwenezi wa UVCCM kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mjini Dodoma, Diwani wa CCM Kata ya Sombetini jijini Arusha, Alphonce Mawazo, alitangaza kuachana na CCM na kujiunga na CHADEMA kwa madai ya kuchoshwa na uonevu na udharimu wa viongozi wa chama hicho.
Aidha, taarifa za uhakika zimebainisha kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kwa siku kadhaa sasa wamekuwa wakifanya mawasiliano na baadhi ya viongozi wa CHADEMA ili kujulishwa taratibu za kujiunga na chama hicho.
Mmoja wa watu waliotajwa kuwa katika maandalizi ya kukihama CCM ni mwenyekiti mmoja wa mkoa wa Kanda ya Ziwa ambaye, amedai kuwa msimamo wake umekuwa ukiwasumbua baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi mpya ya CHADEMA, Diwani Mawazo alisema kuwa ameamua kuachia nafasi yake na kujiunga na CHADEMA ili aweze kuendeleza harakati zake za kuwatetea Watanzania maskini ambao wananyonywa na viongozi wa CCM.
“Nimeondoka mwenyewe katika CCM , nimeachia nafasi ya udiwani, natangaza kujiunga rasmi na CHADEMA, sijalazimishwa na mtu yeyote wala kuahidiwa kitu chochote, ila mimetambua sehemu muhimu ambayo inaweza kuwa ya sauti ya ukombozi kwa Watanzania ni kupitia katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
“Nataka kusema kuwa hakuna kiongozi hata mmoja ndani ya CCM ambaye ana dhamira ya kweli ya kuwasaidia Watanzania na badala yake viongozi wengi ndani ya chama wamekuwa wakijinufaisha wenyewe.
Diwani huyo alidai kuwa viongozi wengi ndani ya CCM wapo kwa jili ya kujinufaisha wao, na kwamba chama hicho kimepoteza matumaini kwa Watanzania kutokana na kutotatua matatizo ya wananchi, ndiyo maana ameamua kuingia katika chama ambacho kinahangaika kutetea masilahi ya watu.
Alisema amekuwa akijengewa chuki na baadhi ya viongozi wa CCM, pale anapojaribu kuwatetea Watanzania ambao ni wanyonge.
Mawazo aliifananisha CHADEMA kama sauti ambayo inawalilia Watanzania wengi maskini ili waweze kuneemeka na rasilimali zilizopo.
Kwa upande wake aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) akitoa salamu zake kwa waandishi wa habari alisema kuwa kwa sasa CCM kinakaribia kufa.
“Nataka niwaambie kuwa katika Jiji la Arusha mambo ni shwari kabisa na msishangae kusikia hata Lukuvi anatuhunga mkono kwa kuwa mwanachama wetu,” alisema Lema.
Katibu mwenezi UVCCM naye atimka
Kutoka Arusha, Katibu wa Uhamsishaji wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) wilayani Longido, Yohana Laizer naye ametimka na kujiunga na CHADEMA.
Laizer alipewa kadi na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani hapa, Samson Mwigamba, yenye namba 0445402 baada ya kukabidhi ile ya CCM yenye namba 683025 iliyotolewa Mei 04, 2004 Tawi la Kiserian, Monduli.
Akiongea jana na waandishi wa habari kwenye ofisi za mkoa za CHADEMA, Laizer alisema kuwa alifikia hatua hiyo ya kujivua uanachama na nyadhifa zote alizokuwa akishikilia baada ya kutoridhishwa na utaratibu wa viongozi kubebana huku wakiwakandamiza wananchi wa kawaida.
Kwa upande wake Mwigamba alimkaribisha Laizer kujiunga na kundi la wapambanaji huku akiwataka wananchi wengine kujitokeza na kujiunga na chama hicho alichodai kuwa kinaendelea kuongeza nguvu kwa ajili ya kushika dola kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mwigamba alisema kuwa wao kama chama hawataacha kupokea watu wanaotaka kujiunga na CHADEMA ili mradi wawe na sifa za kufanya hivyo, ikiwemo kuhakikisha kuwa wana umri unaozidi miaka 18, akili timamu na wasiwe wanachama wa chama kingine cha siasa.
Alisema kuwa wanaelewa kuwa tatizo haliko kwa mwanachama mmoja mmoja bali ni mfumo wa chama hicho ambao umejikita katika misingi mibovu, ikiwamo kutafuta uongozi kwa kutumia rushwa na hila.
“CCM haiwezi kushinda uchaguzi wowote hapa nchini bila rushwa na hila kwani wananchi wamechoshwa nayo, maana hakuna jambo la kujivunia walilowafanyia wananchi hivyo inawalazimisha viongozi na wanachama wake kufanya mambo yasiyo halali ili iweze kushinda.
“Hawa wanaoamua kukataa kufanya kazi za kutumwa ndio wanakimbilia huku CHADEMA tufanye kazi ya kupigania wananchi, hivi mtu akiwa mpagani akaenda kanisani au msikitini kutubu na kubadilika watakataliwa eti kwa sababu alishakuwa mpagani?” alihoji Mwigamba.
Alisema kuwa yeye yuko tayari kumpokea hata mwenyekiti wa taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, na hata Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, endapo wataamua kufanya uamuzi wa kubadilika na kujiunga na CHADEMA.
“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,” alisema mwenyekiti huyo wa CHADEMA mkoani hapa.
Hata hivyo, aliwaponda viongozi mbalimbali wa CCM wanaotoa kauli za kumbeza aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa, James Millya, ambaye alijiunga na CHADEMA wakidai kuwa alikuwa mzigo ndani ya CCM, kwa kuhoji kuwa kama alikuwa ni mzigo kwanini hawakuutua mpaka alipoamua kuondoka yeye mwenyewe.
“Mimi leo niko ndani ya CHADEMA ni kamanda, si kwa mavazi, bali matendo ya kupigania wananchi lakini nikihamia CCM nageuka fisadi kwa matendo, kwani kuna mambo nitayapigania kwa masilahi ya CCM ambayo yatawaumiza wananchi walio wengi,” alisema Mwigamba.
CHANZO - Gazeti la Tanzania Daima
Wednesday, April 18, 2012
JOSHUA NASSARI BUNGENI
Waziri mkuu Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na mbunge wa Arumeru Mashariki mh Joshua Nassari nje ya ukumbi wa Bunge.
Subscribe to:
Posts (Atom)